Waefeso 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
Waefeso 3 (Swahili) Ephesians 3 (English)

Kwa sababu hiyo mimi Paulo ni mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi Mataifa; Waefeso 3:1

For this cause I, Paul, am the prisoner of Christ Jesus on behalf of you Gentiles,

ikiwa mmesikia habari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu; Waefeso 3:2

if it is so that you have heard of the administration of that grace of God which was given me toward you;

ya kwamba kwa kufunuliwa nalijulishwa siri hiyo, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache. Waefeso 3:3

how that by revelation the mystery was made known to me, as I wrote before in few words,

Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo. Waefeso 3:4

by which, when you read, you can perceive my understanding in the mystery of Christ;

Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho; Waefeso 3:5

which in other generations was not made known to the children of men, as it has now been revealed to his holy apostles and prophets in the Spirit;

ya kwamba Mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi wa ahadi yake iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili; Waefeso 3:6

that the Gentiles are fellow heirs, and fellow members of the body, and fellow partakers of his promise in Christ Jesus through the Gospel,

Injili hiyo ambayo nalifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake. Waefeso 3:7

of which I was made a servant, according to the gift of that grace of God which was given me according to the working of his power.

Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nalipewa neema hii ya kuwahubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika; Waefeso 3:8

To me, the very least of all saints, was this grace given, to preach to the Gentiles the unsearchable riches of Christ,

na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote; Waefeso 3:9

and to make all men see what is the administration{TR reads "fellowship" instead of "administration"} of the mystery which for ages has been hidden in God, who created all things through Jesus Christ;

ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho; Waefeso 3:10

to the intent that now through the assembly the manifold wisdom of God might be made known to the principalities and the powers in the heavenly places,

kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana wetu. Waefeso 3:11

according to the eternal purpose which he purposed in Christ Jesus our Lord;

Katika yeye tunao ujasiri na uwezo wa kukaribia katika tumaini kwa njia ya kumwamini. Waefeso 3:12

in whom we have boldness and access in confidence through our faith in him.

Basi naomba msikate tamaa kwa sababu ya dhiki zangu kwa ajili yenu, zilizo utukufu kwenu. Waefeso 3:13

Therefore I ask that you may not lose heart at my troubles for you, which are your glory.

Kwa hiyo nampigia Baba magoti, Waefeso 3:14

For this cause, I bow my knees to the Father of our Lord Jesus Christ,

ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa, Waefeso 3:15

from whom every family in heaven and on earth is named,

awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani. Waefeso 3:16

that he would grant you, according to the riches of his glory, that you may be strengthened with power through his Spirit in the inward man;

Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; Waefeso 3:17

that Christ may dwell in your hearts through faith; to the end that you, being rooted and grounded in love,

ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; Waefeso 3:18

may be strengthened to comprehend with all the saints what is the breadth and length and height and depth,

na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu. Waefeso 3:19

and to know Christ's love which surpasses knowledge, that you may be filled with all the fullness of God.

Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; Waefeso 3:20

Now to him who is able to do exceedingly abundantly above all that we ask or think, according to the power that works in us,

naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina. Waefeso 3:21

to him be the glory in the assembly and in Christ Jesus to all generations forever and ever. Amen.