Danieli 12 Swahili & English

Listen/Download Audio
Danieli 12 (Swahili) Daniel 12 (English)

Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile. Danieli 12:1

"At that time shall Michael stand up, the great prince who stands for the children of your people; and there shall be a time of trouble, such as never was since there was a nation even to that same time: and at that time your people shall be delivered, everyone who shall be found written in the book.

Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele. Danieli 12:2

Many of those who sleep in the dust of the earth shall awake, some to everlasting life, and some to shame and everlasting contempt.

Na walio na hekima watang'aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang'aa kama nyota milele na milele. Danieli 12:3

Those who are wise shall shine as the brightness of the expanse; and those who turn many to righteousness as the stars forever and ever.

Lakini wewe, Ee Danielii, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka. Danieli 12:4

But you, Daniel, shut up the words, and seal the book, even to the time of the end: many shall run back and forth, and knowledge shall be increased."

Ndipo mimi, Danielii, nikatazama, na kumbe, wamesimama wengine wawili, mmoja ukingoni mwa mto upande huu, na mmoja ukingoni mwa mto upande wa pili. Danieli 12:5

Then I, Daniel, looked, and, behold, there stood other two, the one on the brink of the river on this side, and the other on the brink of the river on that side.

Na mmoja akamwuliza yule mtu aliyevikwa nguo za kitani, aliyekuwa juu ya maji ya mto, Je! Itakuwa muda wa miaka mingapi hata mwisho wa mambo haya ya ajabu? Danieli 12:6

One said to the man clothed in linen, who was above the waters of the river, How long shall it be to the end of these wonders?

Nami nikamsikia yule mtu aliyevikwa nguo za kitani, aliyekuwa juu ya maji ya mto, hapo alipoinua mkono wake wa kuume na mkono wake wa kushoto kuelekea mbinguni; akaapa kwa yeye aliye hai milele na milele, ya kwamba itakuwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati; tena watakapokuwa wamekwisha kuvunja nguvu za hao watu watakatifu, ndipo mambo hayo yote yatakapotimizwa. Danieli 12:7

I heard the man clothed in linen, who was above the waters of the river, when he held up his right hand and his left hand to heaven, and swore by him who lives forever that it shall be for a time, times, and a half; and when they have made an end of breaking in pieces the power of the holy people, all these things shall be finished.

Nami nikasikia, lakini sikuelewa; ndipo nikasema, Ee Bwana wangu, mwisho wa mambo haya utakuwaje? Danieli 12:8

I heard, but I didn't understand: then said I, my lord, what shall be the issue of these things?

Akasema, Enenda zako, Danielii; maana maneno haya yamefungwa, na kutiwa muhuri, hata wakati wa mwisho. Danieli 12:9

He said, Go your way, Daniel; for the words are shut up and sealed until the time of the end.

Wengi watajitakasa, na kujifanya weupe, na kusafika; bali wabaya watatenda mabaya; wala hataelewa mtu mbaya awaye yote; bali wao walio na hekima ndio watakaoelewa. Danieli 12:10

Many shall purify themselves, and make themselves white, and be refined; but the wicked shall do wickedly; and none of the wicked shall understand; but those who are wise shall understand.

Na tangu wakati ule ambapo sadaka ya kuteketezwa ya daima itaondolewa, na hilo chukizo la uharibifu litakaposimamishwa, itapata siku elfu na mia mbili na tisini. Danieli 12:11

From the time that the continual [burnt offering] shall be taken away, and the abomination that makes desolate set up, there shall be one thousand two hundred ninety days.

Heri angojaye, na kuzifikilia siku hizo elfu na mia tatu na thelathini na tano. Danieli 12:12

Blessed is he who waits, and comes to the one thousand three hundred thirty-five days.

Lakini enenda zako hata utakapokuwa mwisho ule; maana wewe utastarehe, nawe utasimama katika kura yako mwisho wa siku hizo. Danieli 12:13

But go you your way until the end be; for you shall rest, and shall stand in your lot, at the end of the days.