Danieli 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
Danieli 1 (Swahili) Daniel 1 (English)

Katika mwaka wa tatu wa kumiliki kwake Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, Nebukadreza mfalme wa Babeli,alikwenda Yerusalemu akauhusuru. Danieli 1:1

In the third year of the reign of Jehoiakim king of Judah came Nebuchadnezzar king of Babylon to Jerusalem, and besieged it.

Bwana akamtia Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, katika mkono wake, pamoja na baadhi ya vyombo vya nyumba ya Mungu; naye akavichukua mpaka nchi ya Shinari, mpaka nyumba ya mungu wake; akaviingiza vile vyombo katika nyumba ya hazina ya mungu wake. Danieli 1:2

The Lord gave Jehoiakim king of Judah into his hand, with part of the vessels of the house of God; and he carried them into the land of Shinar to the house of his god: and he brought the vessels into the treasure-house of his god.

Mfalme akamwambia Ashpenazi, mkuu wa matowashi wake, awalete baadhi ya wana wa Israeli, wa uzao wa kifalme, na wa uzao wa kiungwana; Danieli 1:3

The king spoke to Ashpenaz the master of his eunuchs, that he should bring in [certain] of the children of Israel, even of the seed royal and of the nobles;

vijana wasio na mawaa, wazuri wa uso, wajuzi wa hekima, werevu kwa sababu ya maarifa yao, wenye kufahamu elimu, watakaoweza kusimama katika jumba la mfalme; tena alimwambia awafundishe elimu ya Wakaldayo, na lugha yao. Danieli 1:4

youths in whom was no blemish, but well-favored, and skillful in all wisdom, and endowed with knowledge, and understanding science, and such as had ability to stand in the king's palace; and that he should teach them the learning and the language of the Chaldeans.

Huyo mfalme akawaagizia posho ya chakula cha mfalme, na ya divai aliyokunywa, akaagiza walishwe hivyo muda wa miaka mitatu; ili kwamba hatimaye wasimame mbele ya mfalme. Danieli 1:5

The king appointed for them a daily portion of the king's dainties, and of the wine which he drank, and that they should be nourished three years; that at the end of it they should stand before the king.

Basi katika hao walikuwapo baadhi ya wana wa Yuda, Danielii, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria. Danieli 1:6

Now among these were, of the children of Judah, Daniel, Hananiah, Mishael, and Azariah.

Mkuu wa matowashi akawapa majina; alimwita Danielii, Belteshaza; na Hanania akamwita Shadraka; na Mishaeli akamwita Meshaki; na Azaria akamwita Abednego. Danieli 1:7

The prince of the eunuchs gave names to them: to Daniel he gave [the name of] Belteshazzar; and to Hananiah, [of] Shadrach; and to Mishael, [of] Meshach; and to Azariah, [of] Abednego.

Lakini Danielii aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme, wala kwa divai aliyokunywa; basi akamwomba yule mkuu wa matowashi ampe ruhusa asijitie unajisi. Danieli 1:8

But Daniel purposed in his heart that he would not defile himself with the king's dainties, nor with the wine which he drank: therefore he requested of the prince of the eunuchs that he might not defile himself.

Basi Mungu alimjalia Danielii kupata kibali na huruma machoni pa huyo mkuu wa matowashi. Danieli 1:9

Now God made Daniel to find kindness and compassion in the sight of the prince of the eunuchs.

Mkuu wa matowashi akamwambia Danielii, Mimi namwogopa bwana wangu, mfalme, aliyewaagizia ninyi chakula chenu na kinywaji chenu; kwa nini azione nyuso zenu kuwa hazipendezi kama nyuso za vijana hirimu zenu? Basi kwa kufanya hivyo mtahatirisha kichwa changu mbele ya mfalme. Danieli 1:10

The prince of the eunuchs said to Daniel, I fear my lord the king, who has appointed your food and your drink: for why should he see your faces worse looking than the youths who are of your own age? so would you endanger my head with the king.

Ndipo Danielii akamwambia yule msimamizi, ambaye mkuu wa matowashi amemweka juu ya Danielii, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria, Danieli 1:11

Then said Daniel to the steward whom the prince of the eunuchs had appointed over Daniel, Hananiah, Mishael, and Azariah:

Tafadhali utujaribu sisi watumishi wako muda wa siku kumi; na watupe mtama tule, na maji tunywe. Danieli 1:12

Prove your servants, I beg you, ten days; and let them give us pulse to eat, and water to drink.

Kisha nyuso zetu zitazamwe mbele yako, na nyuso za wale vijana wanaokula chakula cha mfalme; ukatutendee sisi watumishi wako kadiri ya utakavyoona. Danieli 1:13

Then let our faces be looked on before you, and the face of the youths who eat of the king's dainties; and as you see, deal with your servants.

Basi akawasikiliza katika jambo hilo, akawajaribu siku kumi. Danieli 1:14

So he listened to them in this matter, and proved them ten days.

Hata mwisho wa zile siku kumi nyuso zao zilikuwa nzuri zaidi, na miili yao ilikuwa imenenepa zaidi, kuliko wale vijana wote waliokula chakula cha mfalme. Danieli 1:15

At the end of ten days their faces appeared fairer, and they were fatter in flesh, than all the youths who ate of the king's dainties.

Basi yule msimamizi akaiondoa posho yao ya chakula, na ile divai waliyopewa wanywe, akawapa mtama tu. Danieli 1:16

So the steward took away their dainties, and the wine that they should drink, and gave them pulse.

Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danielii naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto. Danieli 1:17

Now as for these four youths, God gave them knowledge and skill in all learning and wisdom: and Daniel had understanding in all visions and dreams.

Hata mwisho wa siku zile alizoziagiza mfalme za kuwaingiza, mkuu wa matowashi akawaingiza mbele ya mfalme Nebukadreza. Danieli 1:18

At the end of the days which the king had appointed for bringing them in, the prince of the eunuchs brought them in before Nebuchadnezzar.

Naye mfalme akazungumza nao; na miongoni mwao wote hawakuonekana waliokuwa kama Danielii, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria; kwa hiyo wakasimama mbele ya mfalme. Danieli 1:19

The king talked with them; and among them all was found none like Daniel, Hananiah, Mishael, and Azariah: therefore stood they before the king.

Na katika kila jambo la hekima na ufahamu alilowauliza mfalme, akawaona kuwa walifaa mara kumi zaidi ya waganga na wachawi waliokuwa katika ufalme wake. Danieli 1:20

In every matter of wisdom and understanding, concerning which the king inquired of them, he found them ten times better than all the magicians and enchanters who were in all his realm.

Tena, Danielii huyo akadumu huko hata mwaka wa kwanza wa mfalme Koreshi. Danieli 1:21

Daniel continued even to the first year of king Cyrus.