2 Timotheo 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Timotheo 1 (Swahili) 2nd Timothy 1 (English)

Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu; kwa ajili ya ahadi ya uzima ulio katika Kristo Yesu; 2 Timotheo 1:1

Paul, an apostle of Jesus Christ through the will of God, according to the promise of the life which is in Christ Jesus,

kwa Timotheo, mwanangu mpendwa. Neema na iwe kwako, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu. 2 Timotheo 1:2

to Timothy, my beloved child: Grace, mercy, and peace, from God the Father and Christ Jesus our Lord.

Namshukuru Mungu, nimwabuduye kwa dhamiri safi tangu zamani za wazee wangu, kama vile nikukumbukavyo wewe daima, katika kuomba kwangu usiku na mchana. 2 Timotheo 1:3

I thank God, whom I serve as my forefathers did, with a pure conscience. How unceasing is my memory of you in my petitions, night and day

Nami natamani sana kukuona, nikiyakumbuka machozi yako, ili nijae furaha; 2 Timotheo 1:4

longing to see you, remembering your tears, that I may be filled with joy;

nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo. 2 Timotheo 1:5

having been reminded of the unfeigned faith that is in you; which lived first in your grandmother Lois, and your mother Eunice, and, I am persuaded, in you also.

Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu. 2 Timotheo 1:6

For this cause, I remind you that you should stir up the gift of God which is in you through the laying on of my hands.

Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi. 2 Timotheo 1:7

For God didn't give us a spirit of fear, but of power, love, and self-control.

Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wala usinionee haya mimi mfungwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu; 2 Timotheo 1:8

Therefore don't be ashamed of the testimony of our Lord, nor of me his prisoner; but endure hardship for the Gospel according to the power of God,

ambaye alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisi, bali kwa kadiri ya makusudi yake yeye na neema yake. Neema hiyo tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele, 2 Timotheo 1:9

who saved us and called us with a holy calling, not according to our works, but according to his own purpose and grace, which was given to us in Christ Jesus before times eternal,

na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa ile Injili; 2 Timotheo 1:10

but has now been revealed by the appearing of our Savior, Christ Jesus, who abolished death, and brought life and immortality to light through the Gospel.

ambayo kwa ajili ya hiyo naliwekwa niwe mhubiri na mtume na mwalimu. 2 Timotheo 1:11

For this, I was appointed as a preacher, an apostle, and a teacher of the Gentiles.

Kwa sababu hiyo nimepatikana na mateso haya, wala sitahayari; kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile. 2 Timotheo 1:12

For this cause I suffer also these things. Yet I am not ashamed, for I know him whom I have believed, and I am persuaded that he is able to guard that which I have committed to him against that day.

Shika kielelezo cha maneno yenye uzima uliyoyasikia kwangu, katika imani na upendo ulio katika Kristo Yesu. 2 Timotheo 1:13

Hold the pattern of sound words which you have heard from me, in faith and love which is in Christ Jesus.

Ilinde ile amana nzuri kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu. 2 Timotheo 1:14

That good thing which was committed to you, guard through the Holy Spirit who dwells in us.

Waijua habari hii, ya kuwa wote walio wa Asia waliniepuka, ambao miongoni mwao wamo Figelo na Hermogene. 2 Timotheo 1:15

This you know, that all who are in Asia turned away from me; of whom are Phygelus and Hermogenes.

Bwana awape rehema wale walio wa mlango wake Onesiforo; maana mara nyingi aliniburudisha, wala hakuuonea haya mnyororo wangu; 2 Timotheo 1:16

May the Lord grant mercy to the house of Onesiphorus, for he often refreshed me, and was not ashamed of my chain,

bali, alipokuwapo hapa Rumi, alinitafuta kwa bidii akanipata. 2 Timotheo 1:17

but when he was in Rome, he sought me diligently, and found me

Bwana na ampe kuona rehema machoni pa Bwana siku ile. Na jinsi alivyonihudumia kwa mengi huko Efeso, wewe unajua sana. 2 Timotheo 1:18

(the Lord grant to him to find the Lord's mercy in that day); and in how many things he served at Ephesus, you know very well.