2 Wakorintho 9 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wakorintho 9 (Swahili) 2nd Corinthians 9 (English)

Kwa habari za kuwahudumia watakatifu sina haja ya kuwaandikia. 2 Wakorintho 9:1

It is indeed unnecessary for me to write to you concerning the service to the saints,

Maana najua utayari wenu, ninaojisifia kwa ajili yenu kwa Wamakedonia, kwamba Akaya ilikuwa tayari tangu mwaka mzima; na bidii yenu imewatia moyo wengi wao. 2 Wakorintho 9:2

for I know your readiness, of which I boast on your behalf to them of Macedonia, that Achaia has been prepared for a year past. Your zeal has stirred up very many of them.

Lakini naliwatuma hao ndugu, ili kujisifu kwetu kwa ajili yenu kusibatilike katika jambo hili; mpate kuwa tayari, kama nilivyosema; 2 Wakorintho 9:3

But I have sent the brothers that our boasting on your behalf may not be in vain in this respect, that, just as I said, you may be prepared,

kusudi, wakija Wamakedonia pamoja nami, na kuwakuta hamjawa tayari, tusije tukatahayarika sisi, (tusiseme ninyi), katika hali hiyo ya kutumaini. 2 Wakorintho 9:4

so that I won't by any means, if there come with me any of Macedonia and find you unprepared, we (to say nothing of you) should be disappointed in this confident boasting.

Basi naliona ya kuwa ni lazima niwaonye ndugu hawa watangulie kufika kwenu, na kutengeneza mapema karama yenu mliyoahidi tangu zamani, ili iwe tayari, na hivi iwe kama kipawa, wala si kama kitu kitolewacho kwa unyimivu. 2 Wakorintho 9:5

I thought it necessary therefore to entreat the brothers that they would go before to you, and arrange ahead of time the generous gift that you promised before, that the same might be ready as a matter of generosity, and not of greediness.

Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. 2 Wakorintho 9:6

Remember this: he who sows sparingly will also reap sparingly. He who sows bountifully will also reap bountifully.

Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. 2 Wakorintho 9:7

Let each man give according as he has determined in his heart; not grudgingly, or under compulsion; for God loves a cheerful giver.

Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema; 2 Wakorintho 9:8

And God is able to make all grace abound to you, that you, always having all sufficiency in everything, may abound to every good work.

kama ilivyoandikwa, Ametapanya, amewapa maskini, Haki yake yakaa milele. 2 Wakorintho 9:9

As it is written, "He has scattered abroad, he has given to the poor. His righteousness remains forever."

Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu; 2 Wakorintho 9:10

Now may he who supplies seed to the sower and bread for food, supply and multiply your seed for sowing, and increase the fruits of your righteousness;

mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu. 2 Wakorintho 9:11

you being enriched in everything to all liberality, which works through us thanksgiving to God.

Maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu; 2 Wakorintho 9:12

For this service of giving that you perform not only makes up for lack among the saints, but abounds also through many givings of thanks to God;

kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huo, wanamtukuza Mungu kwa ajili ya utii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote. 2 Wakorintho 9:13

seeing that through the proof given by this service, they glorify God for the obedience of your confession to the Gospel of Christ, and for the liberality of your contribution to them and to all;

Nao wenyewe, wakiomba dua kwa ajili yenu, wawaonea shauku kwa sababu ya neema ya Mungu iliyozidi sana ndani yenu. 2 Wakorintho 9:14

while they themselves also, with supplication on your behalf, yearn for you by reason of the exceeding grace of God in you.

Mungu ashukuriwe kwa sababu ya kipawa chake, tusichoweza kukisifu kama ipasavyo. 2 Wakorintho 9:15

Now thanks be to God for his unspeakable gift!