2 Wakorintho 13 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wakorintho 13 (Swahili) 2nd Corinthians 13 (English)

Hii ndiyo mara ya tatu ya mimi kuja kwenu. Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa. 2 Wakorintho 13:1

This is the third time I am coming to you. "At the mouth of two or three witnesses shall every word established."

Nimetangulia kuwaambia; na, kama vile nilipokuwapo mara ya pili, vivyo hivyo sasa nisipokuwapo, nawaambia wazi wao waliotenda dhambi tangu hapo, na wengine wote, ya kwamba, nikija, sitahurumia; 2 Wakorintho 13:2

I have said beforehand, and I do say beforehand, as when I was present the second time, so now, being absent, I write to those who have sinned before now, and to all the rest, that, if I come again, I will not spare;

kwa kuwa mnatafuta dalili ya Kristo, asemaye ndani yangu, ambaye si dhaifu kwenu, bali ana uweza ndani yenu. 2 Wakorintho 13:3

seeing that you seek a proof of Christ who speaks in me; who toward you is not weak, but is powerful in you.

Maana, alisulibiwa katika udhaifu, lakini anaishi kwa nguvu za Mungu. Maana sisi nasi tu dhaifu katika yeye; lakini tutaishi pamoja naye kwa uweza wa Mungu ulio kwenu. 2 Wakorintho 13:4

For he was crucified through weakness, yet he lives through the power of God. For we also are weak in him, but we will live with him through the power of God toward you.

Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa. 2 Wakorintho 13:5

Test your own selves, whether you are in the faith. Test your own selves. Or don't you know as to your own selves, that Jesus Christ is in you?--unless indeed you are disqualified.

Lakini natumaini kama mtajua ya kuwa sisi hatukukataliwa. 2 Wakorintho 13:6

But I hope that you will know that we aren't disqualified.

Nasi twamwomba Mungu, msifanye lo lote lililo baya; si kwamba sisi tuonekane tumekubaliwa, lakini ninyi mfanye lile lililo jema, tujapokuwa sisi tu kama waliokataliwa. 2 Wakorintho 13:7

Now I pray to God that you do no evil; not that we may appear approved, but that you may do that which is honorable, though we are as reprobate.

Maana hatuwezi kutenda neno lo lote kinyume cha kweli, bali kwa ajili ya kweli. 2 Wakorintho 13:8

For we can do nothing against the truth, but for the truth.

Maana twafurahi, iwapo sisi tu dhaifu, nanyi mmekuwa hodari. Tena twaomba hili nalo, kutimilika kwenu. 2 Wakorintho 13:9

For we rejoice when we are weak and you are strong. And this we also pray for, even your perfecting.

Kwa sababu hiyo, naandika haya nisipokuwapo, ili, nikiwapo, nisiutumie ukali kwa kadiri ya uwezo ule niliopewa na Bwana, kwa kujenga wala si kwa kubomoa. 2 Wakorintho 13:10

For this cause I write these things while absent, that I may not deal sharply when present, according to the authority which the Lord gave me for building up, and not for tearing down.

Hatimaye, ndugu, kwaherini; mtimilike, mfarijike, nieni mamoja, mkae katika amani; na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi. 2 Wakorintho 13:11

Finally, brothers, rejoice. Be perfected, be comforted, be of the same mind, live in peace, and the God of love and peace will be with you.

Salimianeni kwa busu takatifu. 2 Wakorintho 13:12

Greet one another with a holy kiss.

Watakatifu wote wawasalimu. 2 Wakorintho 13:13

All the saints greet you.

Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote. 2 Wakorintho 13:14

The grace of the Lord Jesus Christ, the love of God, and the communion of the Holy Spirit, be with you all. Amen.