Sifa Lyrics

Bwana Umeinuliwa Katika Kiti Chako Cha Enzi by Faith Mbugua cover art

Faith Mbugua - Bwana Umeinuliwa Katika Kiti Chako Cha Enzi Lyrics

Artist:
Faith Mbugua

Lyrics

Bwana Umeinuliwa katika kiti chako cha enzi
Bwana Umeinuliwa aah, katika kiti chako cha enzi

Maserafi, wako mbele zako Mungu uu
wazikabithi heshima zako mbele zako,
Wanalia mtakatifu, ni wewe Mungu
Mtakatifu mtakatifu, ni wewe Mungu

Bwana Umeinuliwa katika kiti chako cha enzi
Bwana Umeinuliwa aah, katika kiti chako cha enzi

Makerubi pia wako mbele zako ooh,
hata nao wazikabithi heshima zao
Wanazivua taji zao za dhahabu uuh,
wakiinama, mtakatifu ni wewe Mungu.

Bwana Umeinuliwa katika kiti chako cha enzi
Bwana Umeinuliwa aah, katika kiti chako cha enzi

Wazee wale ishirini na wanne, eeh,
hata nao wazikabidhi heshima zao,
Wanainama, mtakatifu ni wewe Mungu uu,
mtakatifu, mtakatifu ni wewe Mungu.

Bwana Umeinuliwa aa, katika kiti chako cha enzi
Bwana Umeinuliwa aah, katika kiti chako cha enzi

Viumbe wale walio hai ii,
hata nao wazikabithi heshima zao.
Wapeperusha, mabawa yao mbele zako, ooh,
wajifunika, mtakatifu ni wewe Mungu

Bwana Umeinuliwa aa, katika kiti chako cha enzi
Bwana Umeinuliwa aah, katika kiti chako cha enzi

Nafsi yangu naiinua mbele zako ooh,
Naungamana na hilo jeshi la mbinguni,
mataifa yote nayo yajue, eeh,
ya kwamba wewe, wewe mungu ni mtakatifu

Bwana Umeinuliwa aaah, katika kiti chako cha enzi
Bwana Umeinuliwa aah, katika kiti chako cha enzi

Video