Tito 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
Tito 1 (Swahili) Titus 1 (English)

Paulo, mtumwa wa Mungu, na mtume wa Yesu Kristo; kwa ajili ya imani ya wateule wa Mungu, na ujuzi wa kweli ile iletayo utauwa; Tito 1:1

Paul, a servant of God, and an apostle of Jesus Christ, according to the faith of God's chosen ones, and the knowledge of the truth which is according to godliness,

katika tumaini la uzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema uongo aliuahidi tangu milele; Tito 1:2

in hope of eternal life, which God, who can't lie, promised before eternal times;

akalifunua neno lake kwa majira yake katika ule ujumbe niliowekewa amana mimi kwa amri ya Mwokozi wetu Mungu; Tito 1:3

but in his own time revealed his word in the message with which I was entrusted according to the commandment of God our Savior;

kwa Tito, mwanangu hasa katika imani tuishirikiyo. Neema na iwe kwako na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Mwokozi wetu. Tito 1:4

to Titus, my true child according to a common faith: Grace, mercy, and peace from God the Father and the Lord Jesus Christ our Savior.

Kwa sababu hii nalikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuweka wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru; Tito 1:5

I left you in Crete for this reason, that you would set in order the things that were lacking, and appoint elders in every city, as I directed you;

ikiwa mtu hakushitakiwa neno, naye ni mume wa mke mmoja, ana watoto waaminio, wasioshitakiwa kuwa ni wafisadi wala wasiotii. Tito 1:6

if anyone is blameless, the husband of one wife, having children who believe, who are not accused of loose or unruly behavior.

Maana imempasa askofu awe mtu asiyeshitakiwa neno ,kwa kuwa ni wakili wa MUNGU;asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake,asiwe mwepesi wa hasira,asiwe mlevi wala mgomvi,asiwe mpenda mapato ya aibu. Tito 1:7

For the overseer must be blameless, as God's steward; not self-pleasing, not easily angered, not given to wine, not violent, not greedy for dishonest gain;

bali awe mkaribishaji, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye haki, mtakatifu, mwenye kudhibiti nafsi yake; Tito 1:8

but given to hospitality, as a lover of good, sober-minded, fair, holy, self-controlled;

akilishika lile neno la imani vile vile kama alivyofundishwa, apate kuweza kuwaonya watu kwa mafundisho yenye uzima, na kuwashinda wenye kupinga. Tito 1:9

holding to the faithful word which is according to the teaching, that he may be able to exhort in the sound doctrine, and to convict those who contradict him.

Kwa maana kuna wengi wasiotii, wenye maneno yasiyo na maana, wadanganyaji, na hasa wale wa tohara, ambao yapasa wazibwe vinywa vyao. Tito 1:10

For there are also many unruly men, vain talkers and deceivers, especially those of the circumcision,

Hao wanapindua watu wa nyumba nzima, wakifundisha yasiyowapasa kwa ajili ya mapato ya aibu. Tito 1:11

whose mouths must be stopped; men who overthrow whole houses, teaching things which they ought not, for dishonest gain's sake.

Mtu wa kwao, nabii wao wenyewe, amesema, Wakrete ni waongo siku zote, hayawani wabaya, walafi wavivu. Tito 1:12

One of them, a prophet of their own, said, "Cretans are always liars, evil beasts, and idle gluttons."

Ushuhuda huo ni kweli. Kwa sababu hiyo uwakemee kwa ukali, ili wapate kuwa wazima katika imani; Tito 1:13

This testimony is true. For this cause, reprove them sharply, that they may be sound in the faith,

wasisikilize hadithi za Kiyahudi, wala maagizo ya watu wajiepushao na yaliyo kweli. Tito 1:14

not paying attention to Jewish fables and commandments of men who turn away from the truth.

Vitu vyote ni safi kwa hao walio safi; lakini hakuna kilicho safi kwao walio wanajisi, wasioamini; bali akili zao zimekuwa najisi, na nia zao pia. Tito 1:15

To the pure, all things are pure; but to those who are defiled and unbelieving, nothing is pure; but both their mind and their conscience are defiled.

Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala kwa kila tendo jema hawafai. Tito 1:16

They profess that they know God, but by their works they deny him, being abominable, disobedient, and unfit for any good work.