Ruthu 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ruthu 1 (Swahili) Ruth 1 (English)

Ikawa zamani za Waamuzi walipoamua, kulikuwa na njaa katika nchi. Akaondoka mtu mmoja wa Bethlehemu ya Yuda, akaenda kukaa katika nchi ya Moabu, yeye na mkewe na wanawe wawili. Ruthu 1:1

It happened in the days when the judges judged, that there was a famine in the land. A certain man of Bethlehem Judah went to sojourn in the country of Moab, he, and his wife, and his two sons.

Na jina la mtu huyo aliitwa Elimeleki, na jina la mkewe Naomi, na majina ya wanawe wawili Maloni na Kilioni, Waefrathi wa Bethlehemu ya Yuda. Wakafika nchi ya Moabu, wakakaa huko. Ruthu 1:2

The name of the man was Elimelech, and the name of his wife Naomi, and the name of his two sons Mahlon and Chilion, Ephrathites of Bethlehem Judah. They came into the country of Moab, and continued there.

Akafa Elimeleki, mumewe Naomi; na yule mwanamke akasalia na wanawe wawili. Ruthu 1:3

Elimelech, Naomi's husband, died; and she was left, and her two sons.

Nao wakaoa wake katika wanawake wa Moabu; na jina la mmoja aliitwa Orpa, na jina la wa pili Ruthuu. Wakakaa huko yapata miaka kumi. Ruthu 1:4

They took them wives of the women of Moab; the name of the one was Orpah, and the name of the other Ruth: and they lived there about ten years.

Wakafa na Maloni na Kilioni wote wawili; na huyo mwanamke akawa amefiwa na wanawe wawili, na mumewe pia. Ruthu 1:5

Mahlon and Chilion died both of them; and the woman was left of her two children and of her husband.

Ndipo alipoondoka, yeye na wakweze, ili kurudi kutoka nchi ya Moabu; maana huko katika nchi ya Moabu amesikia ya kwamba Bwana amewajilia watu wake na kuwapa chakula. Ruthu 1:6

Then she arose with her daughters-in-law, that she might return from the country of Moab: for she had heard in the country of Moab how that Yahweh had visited his people in giving them bread.

Basi akatoka pale alipokuwapo, na wakweze wawili pamoja naye; wakashika njia ili kurudi mpaka nchi ya Yuda. Ruthu 1:7

She went forth out of the place where she was, and her two daughters-in-law with her; and they went on the way to return to the land of Judah.

Kisha Naomi akawaambia wakweze wawili, Nendeni sasa mkarejee kila mmoja nyumbani kwa mamaye; Bwana na awatendee mema ninyi, kama ninyi mlivyowatendea mema hao waliofariki na mimi pia. Ruthu 1:8

Naomi said to her two daughters-in-law, Go, return each of you to her mother's house: Yahweh deal kindly with you, as you have dealt with the dead, and with me.

Bwana na awajalie kuona raha kila mmoja nyumbani kwa mumewe. Kisha akawabusu; nao wakapaza sauti zao wakalia. Ruthu 1:9

Yahweh grant you that you may find rest, each of you in the house of her husband. Then she kissed them, and they lifted up their voice, and wept.

Wakamwambia, La, sivyo; lakini tutarudi pamoja nawe kwa watu wako. Ruthu 1:10

They said to her, No, but we will return with you to your people.

Naye Naomi akasema, Enyi wanangu, mrejee; kwani kufuatana na mimi? Je! Mimi ninao watoto wa kiume tena tumboni mwangu, hata wawe waume zenu? Ruthu 1:11

Naomi said, Turn again, my daughters: why will you go with me? have I yet sons in my womb, that they may be your husbands?

Enyi wanangu, mrejee; nendeni zenu; kwa kuwa mimi ni mzee, siwezi kupata mume tena. Kama ningesema, Natumaini; kama ningepata mume hata usiku huu, na kuzaa watoto wa kiume; Ruthu 1:12

Turn again, my daughters, go your way; for I am too old to have a husband. If I should say, I have hope, if I should even have a husband tonight, and should also bear sons;

je! Mngesubiri hata watakapokuwa watu wazima? Mngejizuia msiwe na waume? La, sivyo, wanangu; maana ni vigumu kwangu kuliko kwenu, kwa sababu mkono wa Bwana umetoka juu yangu. Ruthu 1:13

would you therefore wait until they were grown? would you therefore stay from having husbands? nay, my daughters, for it grieves me much for your sakes, for the hand of Yahweh is gone forth against me.

Nao wakapaza sauti zao, wakalia tena, na Orpa akambusu mkwewe, lakini Ruthuu akaambatana naye. Ruthu 1:14

They lifted up their voice, and wept again: and Orpah kissed her mother-in-law, but Ruth joined with her.

Naye akasema, Tazama, shemeji yako amerejea kwa watu wake, na kwa mungu wake; basi urejee wewe umfuate shemeji yako. Ruthu 1:15

She said, Behold, your sister-in-law is gone back to her people, and to her god: return you after your sister-in-law.

Naye Ruthuu akasema, Usinisihi nikuache, Nirejee nisifuatane nawe; Maana wewe uendako nitakwenda, Na wewe ukaapo nitakaa. Watu wako watakuwa watu wangu, Na Mungu wako atakuwa Mungu wangu; Ruthu 1:16

Ruth said, "Don't entreat me to leave you, and to return from following after you, for where you go, I will go; and where you lodge, I will lodge; your people shall be my people, and your God my God;

Pale utakapokufa nitakufa nami, Na papo hapo nitazikwa; Bwana anitende vivyo na kuzidi, Ila kufa tu kutatutenga wewe nami. Ruthu 1:17

where you die, will I die, and there will I be buried: Yahweh do so to me, and more also, if anything but death part you and me."

Basi alipomwona kuwa amekaza nia yake kufuatana naye, aliacha kusema naye. Ruthu 1:18

When she saw that she was steadfastly minded to go with her, she left off speaking to her.

Hivyo hao wakaendelea wote wawili hata walipofika Bethlehemu. Na ikawa walipofika Bethlehemu, mji wote ulitaharuki kwa habari zao. Nao wanawake wakasema, Je! Huyu ni Naomi? Ruthu 1:19

So they two went until they came to Bethlehem. It happened, when they were come to Bethlehem, that all the city was moved about them, and [the women] said, Is this Naomi?

Akawaambia, Msiniite Naomi niiteni Mara,kwa sababu Mwenyezi Mungu amenitenda mambo machungu sana. Ruthu 1:20

She said to them, "Don't call me Naomi, call me Mara; for the Almighty has dealt very bitterly with me.

Mimi nalitoka hali nimejaa, naye Bwana amenirudisha sina kitu, kwani kuniita Naomi, ikiwa Bwana ameshuhudia juu yangu, na Mwenyezi Mungu amenitesa? Ruthu 1:21

I went out full, and Yahweh has brought me home again empty; why do you call me Naomi, seeing Yahweh has testified against me, and the Almighty has afflicted me?"

Basi Naomi akarudi; pamoja na Ruthuu Mmoabi, mkwewe; ambao walirudi kutoka nchi ya Moabu; nao wakafika Bethlehemu mwanzo wa mavuno ya shayiri. Ruthu 1:22

So Naomi returned, and Ruth the Moabitess, her daughter-in-law, with her, who returned out of the country of Moab: and they came to Bethlehem in the beginning of barley harvest.