Obadia BSB

Obadia 1

Obadiah Chapter 1

1
Maono yake Obadia. Ndivyo asemavyo Bwana MUNGU juu ya Edomu; Tumepata habari kwa Bwana, Na mjumbe ametumwa kati ya mataifa, Akisema,Haya,inukeni ninyi;Na tuinuke tupigane naye.
This is the vision of Obadiah: This is what the Lord GOD says about Edom—We have heard a message from the LORD; an envoy has been sent among the nations to say, “Rise up, and let us go to battle against her!”—
2
Tazama, nimekufanya mdogo kati ya mataifa; Umedharauliwa sana.
“Behold, I will make you small among the nations; you will be deeply despised.
3
Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Mwenye makao yako juu sana; Asemaye moyoni, Ni nani atakayenishusha mimi?
The pride of your heart has deceived you, O dwellers in the clefts of the rocks whose habitation is the heights, who say in your heart, ‘Who can bring me down to the ground?’
4
Ujapopanda juu kama tai, Ijapokuwa kioto chako kimewekwa kati ya nyota, Nitakushusha kutoka huko; asema Bwana.
Though you soar like the eagle and make your nest among the stars, even from there I will bring you down,” declares the LORD.
5
Kama wevi wangekujilia, kama wanyang'anyi wangekujilia usiku, (jinsi ulivyokatiliwa mbali!) Je! Wasingeiba kiasi cha kuwatosha? Kama wachumao zabibu wangekujilia, je! Wasingeacha baadhi ya zabibu, ziokotwe?
“If thieves came to you, if robbers by night—oh, how you will be ruined—would they not steal only what they wanted? If grape gatherers came to you, would they not leave some gleanings?
6
Jinsi watu wa Esau wanavyotafutwa-tafutwa! Jinsi hazina zake zilizofichwa zinavyoulizwa-ulizwa!
But how Esau will be pillaged, his hidden treasures sought out!
7
Watu wote wa mapatano yako Wamekufukuza, hata mipakani; Wale waliofanya amani nawe Wamekudanganya, na kukushinda; Walao mkate wako wameweka mtego chini yako; Wala hana ufahamu wa hayo ndani yake.
All the men allied with you will drive you to the border; the men at peace with you will deceive and overpower you. Those who eat your bread will set a trap for you without your awareness of it.
8
Siku hiyo, je! Sitawaangamiza watu wenye akili katika Edomu, na wenye ufahamu katika kilima cha Esau? Asema Bwana.
In that day, declares the LORD, will I not destroy the wise men of Edom and the men of understanding in the mountains of Esau?
9
Na mashujaa wako, Ee Temani, watafadhaika, hata iwe kila mtu akatiliwe mbali kwa kuuawa katika kilima cha Esau.
Then your mighty men, O Teman, will be terrified, so that everyone in the mountains of Esau will be cut down in the slaughter.
10
Kwa sababu ya udhalimu aliotendwa ndugu yako Yakobo, aibu itakufunika, nawe utakatiliwa mbali hata milele.
Because of the violence against your brother Jacob, you will be covered with shame and cut off forever.
11
Siku ile uliposimama upande, siku ile wageni walipochukua mali zake, na watu wa kabila nyingine walipoingia katika malango yake, na kumpa kura juu ya Yerusalemu, wewe nawe ulikuwa kama mmoja wao.
On the day you stood aloof while strangers carried off his wealth and foreigners entered his gate and cast lots for Jerusalem, you were just like one of them.
12
Lakini usiitazame siku ya ndugu yako, siku ya mashaka yake, wala usisimange juu ya wana wa Yuda siku ya kuangamizwa kwao; wala usinene maneno ya kiburi katika siku ya shida yao.
But you should not gloat in that day, your brother’s day of misfortune, nor rejoice over the people of Judah in the day of their destruction, nor boast proudly in the day of their distress.
13
Usiingie katika lango la watu wangu, siku ya msiba wao; naam, usiyatazame mateso yao, siku ya msiba wao; wala usitie mikono yako juu ya mali zao, siku ya msiba wao.
You should not enter the gate of My people in the day of their disaster, nor gloat over their affliction in the day of their disaster, nor loot their wealth in the day of their disaster.
14
Wala usisimame penye njia panda, ili kuwakatilia mbali watu wake wakimbiao; wala usiwatoe watu wake waliosalia, katika siku ya dhiki.
Nor should you stand at the crossroads to cut off their fugitives, nor deliver up their survivors in the day of their distress.
15
Kwa maana hiyo siku ya Bwana i karibu juu ya mataifa yote; kama ulivyotenda, ndivyo utakavyotendwa; malipo yako yatakurudia juu ya kichwa chako mwenyewe.
For the Day of the LORD is near for all the nations. As you have done, it will be done to you; your recompense will return upon your own head.
16
Kwa maana kama vile mlivyokunywa juu ya mlima wangu mtakatifu, ndivyo mataifa yote watakavyokunywa daima; naam, watakunywa na kubabaika, nao watakuwa kana kwamba hawakuwa kamwe.
For as you drank on My holy mountain, so all the nations will drink continually. They will drink and gulp it down; they will be as if they had never existed.
17
Bali katika mlima Sayuni watakuwako wenye kuokoka, nao utakuwa mtakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki milki zao.
But on Mount Zion there will be deliverance, and it will be holy, and the house of Jacob will reclaim their possession.
18
Na nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu itakuwa mwali wa moto, na nyumba ya Esau itakuwa mabua makavu, nao watawaka kati yao, na kuwateketeza; wala hatasalia mtu awaye yote katika nyumba ya Esau; kwa kuwa Bwana amesema hayo.
Then the house of Jacob will be a blazing fire, and the house of Joseph a burning flame; but the house of Esau will be stubble—Jacob will set it ablaze and consume it. Therefore no survivor will remain from the house of Esau.” For the LORD has spoken.
19
Na watu wa Negebu wataumiliki mlima wa Esau; na watu wa Shefela watawamiliki Wafilisti; nao watalimiliki konde la Efraimu, na konde la Samaria, na Benyamini atamiliki Gileadi.
Those from the Negev will possess the mountains of Esau; those from the foothills will possess the land of the Philistines. They will occupy the fields of Ephraim and Samaria, and Benjamin will possess Gilead.
20
Na watu wa jeshi hili la wana wa Israeli waliotekwa, walio kati ya Wakanaani, watamiliki mpaka Sarepta; na hao watu wa Yerusalemu waliotekwa, waliomo Sefaradi, wataimiliki miji ya Negebu.
And the exiles of this host of the Israelites will possess the land of the Canaanites as far as Zarephath; and the exiles from Jerusalem who are in Sepharad will possess the cities of the Negev.
21
Tena waokozi watakwea juu ya mlima Sayuni ili kuuhukumu mlima wa Esau; na huo ufalme utakuwa ni mali ya Bwana. </p>
The deliverers will ascend Mount Zion to rule over the mountains of Esau. And the kingdom will belong to the LORD.

Chagua Sura

1