Nahumu 3 Swahili & English
Listen/Download AudioNahumu 3 (Swahili) | Nahum 3 (English) |
---|---|
Ole wake mji wa damu! Umejaa mambo ya uongo na unyang'anyi; mateka hayaondoki. Nahumu 3:1 |
Woe to the bloody city! It is all full of lies and robbery. The prey doesn't depart. |
Kelele za mjeledi, kelele za magurudumu yafanyayo kishindo; na farasi wenye kupara-para, na magari ya vita yenye kuruka-ruka; Nahumu 3:2 |
The noise of the whip, the noise of the rattling of wheels, prancing horses, and bounding chariots, |
mpanda farasi akipanda, na upanga ukimeta-meta, na mkuki ukimemetuka; na wingi wa waliouawa, na chungu kubwa ya mizoga; mizoga haina mwisho; wanajikwaa juu ya mizoga yao. Nahumu 3:3 |
the horseman mounting, and the flashing sword, the glittering spear, and a multitude of slain, and a great heap of corpses, and there is no end of the bodies. They stumble on their bodies, |
Kwa sababu ya wingi wa ukahaba wa yule kahaba mzuri, yule bibi wa mambo ya uchawi, auzaye mataifa kwa ukahaba wake, na jamaa za watu kwa uchawi wake. Nahumu 3:4 |
because of the multitude of the prostitution of the alluring prostitute, the mistress of witchcraft, who sells nations through her prostitution, and families through her witchcraft. |
Tazama, mimi ni juu yako, asema Bwana wa majeshi; nami nitafunua marinda yako mbele ya uso wako; nami nitawaonyesha mataifa uchi wako, na falme aibu yako. Nahumu 3:5 |
"Behold, I am against you," says Yahweh of Hosts, "and I will lift your skirts over your face. I will show the nations your nakedness, and the kingdoms your shame. |
Nami nitatupa uchafu uchukizao juu yako, kukufanya uwe mchafu, nami nitakufanya kuwa kitu cha kutazamwa kwa dharau. Nahumu 3:6 |
I will throw abominable filth on you, and make you vile, and will set you a spectacle. |
Hata itakuwa, wote wakutazamao watakukimbia, wakisema, Ninawi umeharibika; ni nani atakayeuhurumia? Nikutafutie wapi wafariji? Nahumu 3:7 |
It will happen that all those who look at you will flee from you, and say, 'Nineveh is laid waste Who will mourn for her?' Where will I seek comforters for you?" |
Je! Wewe u mwema kuliko No-amoni, uliowekwa kati ya mito, uliozungukwa na maji; ambao boma lake lilikuwa bahari, na bahari ilikuwa ukuta wake. Nahumu 3:8 |
Are you better than No-Amon,{or, Thebes} who was situated among the rivers, who had the waters around her; whose rampart was the sea, and her wall was of the sea? |
Kushi na Misri walikuwa nguvu zake, nazo zilikuwa hazina mpaka; Putu na Walibia walikuwa wasaidizi wake. Nahumu 3:9 |
Cush and Egypt were her boundless strength. Put and Libya were her helpers. |
Hata hivyo alichukuliwa mbali, alikwenda utumwani; watoto wake wachanga walisetwa kwenye maachano ya njia kuu zote; watu wake wenye heshima wakapigiwa kura, na wakuu wake wote wakafungwa kwa minyororo. Nahumu 3:10 |
Yet was she carried away. She went into captivity. Her young children also were dashed in pieces at the head of all the streets, and they cast lots for her honorable men, and all her great men were bound in chains. |
Tena utalewa, utafichwa; tena utatafuta ngome kwa sababu ya adui. Nahumu 3:11 |
You also will be drunken. You will be hidden. You also will seek a stronghold because of the enemy. |
Ngome zako zote zitakuwa kama mitini yenye tini zilizoiva kwanza; ikitikisika zaanguka katika kinywa chake alaye. Nahumu 3:12 |
All your fortresses will be like fig trees with the first-ripe figs: if they are shaken, they fall into the mouth of the eater. |
Tazama, watu wako walio ndani yako ni wanawake; malango ya nchi yako yamekuwa wazi kabisa mbele ya adui zako; moto umeteketeza mapingo yako. Nahumu 3:13 |
Behold, your troops in your midst are women. The gates of your land are set wide open to your enemies. The fire has devoured your bars. |
Teka maji yawe tayari kwa kuzingirwa kwako; Zitie nguvu ngome zako; Ingia katika udongo, yakanyage matope, Itie nguvu tanuru ya kuokea matofali. Nahumu 3:14 |
Draw water for the siege. Strengthen your fortresses. Go into the clay, and tread the mortar. Make the brick kiln strong. |
Huko moto utakuteketeza; Upanga utakukatilia mbali; Utakumeza kama tunutu alavyo; Jifanye kuwa wengi kama tunutu! Jifanye kuwa wengi kama nzige! Nahumu 3:15 |
There the fire will devour you. The sword will cut you off. It will devour you like the grasshopper. Multiply like grasshoppers. Multiply like the locust. |
Umeongeza wafanya biashara wako kuwa wengi kuliko nyota za mbinguni; tunutu huharibu; kisha huruka juu na kwenda zake. Nahumu 3:16 |
You have increased your merchants more than the stars of the skies. The grasshopper strips, and flees away. |
Watu wako waliotiwa taji ni kama nzige, na majemadari wako ni kama makundi ya mapanzi, watuao katika vitalu siku ya baridi, lakini jua lipandapo huruka juu na kwenda zao, na mahali pao walipo hapajulikani. Nahumu 3:17 |
Your guards are like the locusts, and your officials like the swarms of locusts, which settle on the walls on a cold day, but when the sun appears, they flee away, and their place is not known where they are. |
Wachungaji wako wanalala usingizi, Ee mfalme wa Ashuru; watu wako wenye heshima wamepumzika; watu wako wametawanyika juu ya milima, wala hapana mtu wa kuwakusanya. Nahumu 3:18 |
Your shepherds slumber, king of Assyria. Your nobles lie down. Your people are scattered on the mountains, and there is no one to gather them. |
Jeraha yako haipunguziki; jeraha yako ni nzito sana; wote wasikiao habari zako wapiga makofi juu yako; kwa maana ni nani ambaye uovu wako haukupita juu yake daima? Nahumu 3:19 |
There is no healing your wound, for your injury is fatal. All who hear the report of you clap their hands over you; for who hasn't felt your endless cruelty? |