2 Wathesalonike Mlango 3 2dThessalonians

2 Wathesalonike 3:1

Hatimaye, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, na kutukuzwa vile vile kama ilivyo kwenu;

2 Wathesalonike 3:2

tukaokolewe na watu wasio haki, wabaya; maana si wote walio na imani.

2 Wathesalonike 3:3

Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda na yule mwovu.

2 Wathesalonike 3:4

Nasi tumemtumaini Bwana kwa mambo yenu, kwamba mnayafanya tulivyowaagiza, tena kwamba mtayafanya.

2 Wathesalonike 3:5

Bwana awaongoze mioyo yenu mkapate pendo la Mungu, na saburi ya Kristo.

2 Wathesalonike 3:6

Ndugu, twawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu.

2 Wathesalonike 3:7

Mwajua wenyewe jinsi iwapasavyo kutufuata; kwa sababu hatukuenda bila utaratibu kwenu;

2 Wathesalonike 3:8

wala hatukula chakula kwa mtu ye yote bure; bali kwa taabu na masumbufu, usiku na mchana tulitenda kazi, ili tusimlemee mtu wa kwenu awaye yote.

2 Wathesalonike 3:9

Si kwamba hatuna amri, lakini makusudi tufanye nafsi zetu kuwa kielelezo kwenu, mtufuate.

2 Wathesalonike 3:10

Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula.

2 Wathesalonike 3:11

Maana twasikia kwamba wako watu kwenu waendao bila utaratibu, hawana shughuli zao wenyewe, lakini wanajishughulisha na mambo ya wengine.

2 Wathesalonike 3:12

Basi twawaagiza hao, na kuwaonya katika Bwana Yesu Kristo, watende kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe.

2 Wathesalonike 3:13

Lakini ninyi, ndugu, msikate tamaa katika kutenda mema.

2 Wathesalonike 3:14

Na ikiwa mtu awaye yote halishiki neno letu la waraka huu, jihadharini na mtu huyo, wala msizungumze naye, apate kutahayari;

2 Wathesalonike 3:15

lakini msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu.

2 Wathesalonike 3:16

Sasa, Bwana wa amani mwenyewe na awape amani daima kwa njia zote. Bwana awe pamoja nanyi nyote.

2 Wathesalonike 3:17

Salamu zangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndiyo alama katika kila waraka, ndio mwandiko wangu.

2 Wathesalonike 3:18

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote.