1 Timotheo 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Timotheo 5 (Swahili) 1st Timothy 5 (English)

Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba; na vijana kama ndugu; 1 Timotheo 5:1

Don't rebuke an older man, but exhort him as a father; the younger men as brothers;

wanawake wazee kama mama; wanawake vijana kama ndugu wa kike; katika usafi wote. 1 Timotheo 5:2

the elder women as mothers; the younger as sisters, in all purity.

Uwaheshimu wajane walio wajane kweli kweli. 1 Timotheo 5:3

Honor widows who are widows indeed.

Lakini mjane akiwa ana watoto au wajukuu, na wajifunze kwanza kuyatenda yaliyo wajibu wao kwa jamaa zao wenyewe, na kuwalipa wazazi wao. Kwa kuwa hili lakubalika mbele za Mungu. 1 Timotheo 5:4

But if any widow has children or grandchildren, let them learn first to show piety towards their own family, and to repay their parents, for this is{TR adds "good and"} acceptable in the sight of God.

Basi yeye aliye mjane kweli kweli, ameachwa peke yake, huyo amemwekea Mungu tumaini lake, naye hudumu katika maombi na sala mchana na usiku. 1 Timotheo 5:5

Now she who is a widow indeed, and desolate, has her hope set on God, and continues in petitions and prayers night and day.

Bali, yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hai. 1 Timotheo 5:6

But she who gives herself to pleasure is dead while she lives.

Mambo hayo pia uyaagize, ili wasiwe na lawama. 1 Timotheo 5:7

Also command these things, that they may be without reproach.

Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini. 1 Timotheo 5:8

But if anyone doesn't provide for his own, and especially his own household, he has denied the faith, and is worse than an unbeliever.

Mjane asiandikwe isipokuwa umri wake amepata miaka sitini; naye amekuwa mke wa mume mmoja; 1 Timotheo 5:9

Let no one be enrolled as a widow under sixty years old, having been the wife of one man,

naye ameshuhudiwa kwa matendo mema; ikiwa amelea watoto, ikiwa amekaribisha wageni, ikiwa amewaosha watakatifu miguu, ikiwa amewasaidia wateswao, ikiwa amefuata kwa bidii kila tendo jema. 1 Timotheo 5:10

being approved by good works, if she has brought up children, if she has been hospitable to strangers, if she has washed the saints' feet, if she has relieved the afflicted, and if she has diligently followed every good work.

Bali wajane walio vijana ukatae kuwaandika hao, maana, wakizidiwa na tamaa kinyume cha Kristo, wataka kuolewa; 1 Timotheo 5:11

But refuse younger widows, for when they have grown wanton against Christ, they desire to marry;

nao wana hukumu kwa kuwa wameiacha imani yao ya kwanza. 1 Timotheo 5:12

having condemnation, because they have rejected their first pledge.

Tena, pamoja na hayo, hujifunza kuwa wavivu, wakizunguka-zunguka nyumba kwa nyumba; wala si wavivu tu, lakini ni wachongezi na wadadisi, wakinena maneno yasiyowapasa. 1 Timotheo 5:13

Besides, they also learn to be idle, going about from house to house. Not only idle, but also gossips and busybodies, saying things which they ought not.

Basi napenda wajane, ambao si wazee, waolewe, wazae watoto, wawe na madaraka ya nyumbani; ili wasimpe adui nafasi ya kulaumu. 1 Timotheo 5:14

I desire therefore that the younger widows marry, bear children, rule the household, and give no occasion to the adversary for reviling.

Kwa maana wengine wamekwisha kugeuka na kumfuata Shetani. 1 Timotheo 5:15

For already some have turned aside after Satan.

Mwanamke aaminiye, akiwa ana wajane, na awasaidie mwenyewe, Kanisa lisilemewe; ili liwasaidie wale walio wajane kweli kweli. 1 Timotheo 5:16

If any man or woman who believes has widows, let them relieve them, and don't let the assembly be burdened; that it might relieve those who are widows indeed.

Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha. 1 Timotheo 5:17

Let the elders who rule well be counted worthy of double honor, especially those who labor in the word and in teaching.

Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng'ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake. 1 Timotheo 5:18

For the Scripture says, "You shall not muzzle the ox when it treads out the grain." And, "The laborer is worthy of his wages."

Usikubali mashitaka juu ya mzee, ila kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu. 1 Timotheo 5:19

Don't receive an accusation against an elder, except at the word of two or three witnesses.

Wale wadumuo kutenda dhambi uwakemee mbele ya wote, ili na wengine waogope. 1 Timotheo 5:20

Those who sin, reprove in the sight of all, that the rest also may be in fear.

Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, na mbele za malaika wateule, uyatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lo lote kwa upendeleo. 1 Timotheo 5:21

I charge you in the sight of God, and Christ Jesus, and the chosen angels, that you observe these things without prejudice, doing nothing by partiality.

Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengine. Ujilinde nafsi yako uwe safi. 1 Timotheo 5:22

Lay hands hastily on no one, neither be a participant in other men's sins. Keep yourself pure.

Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara. 1 Timotheo 5:23

Be no longer a drinker of water only, but use a little wine for your stomach's sake and your frequent infirmities.

Dhambi za watu wengine zi dhahiri, zatangulia kwenda hukumuni; wengine dhambi zao zawafuata. 1 Timotheo 5:24

Some men's sins are evident, preceding them to judgment, and some also follow later.

Vivyo hivyo matendo yaliyo mazuri ya dhahiri; wala yale yasiyo dhahiri hayawezi kusitirika. 1 Timotheo 5:25

In the same way also there are good works that are obvious, and those that are otherwise can't be hidden.