1 Yohana 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Yohana 5 (Swahili) 1st John 5 (English)

Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa, ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye. 1 Yohana 5:1

Whoever believes that Jesus is the Christ is born of God. Whoever loves the father also loves the child who is born of him.

Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake. 1 Yohana 5:2

By this we know that we love the children of God, when we love God and keep his commandments.

Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito. 1 Yohana 5:3

For this is the love of God, that we keep his commandments. His commandments are not grievous.

Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu. 1 Yohana 5:4

For whatever is born of God overcomes the world. This is the victory that has overcome the world: your faith.

Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu? 1 Yohana 5:5

Who is he who overcomes the world, but he who believes that Jesus is the Son of God?

Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu. 1 Yohana 5:6

This is he who came by water and blood, Jesus Christ; not with the water only, but with the water and the blood. It is the Spirit who testifies, because the Spirit is the truth.

Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli. 1 Yohana 5:7

For there are three who testify{Only a few recent manuscripts add "in heaven: the Father, the Word, and the Holy Spirit; and these three are one. And there are three that testify on earth"}:

Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja. 1 Yohana 5:8

the Spirit, and the water, and the blood; and the three agree as one.

Kisha wako watatu washuhudiao duniani], Roho, na maji, na damu; na watatu hawa hupatana kwa habari moja. Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, kwamba amemshuhudia Mwanawe. 1 Yohana 5:9

If we receive the witness of men, the witness of God is greater; for this is God's testimony which he has testified concerning his Son.

Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe. 1 Yohana 5:10

He who believes in the Son of God has the testimony in himself. He who doesn't believe God has made him a liar, because he has not believed in the testimony that God has given concerning his Son.

Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe. 1 Yohana 5:11

The testimony is this, that God gave to us eternal life, and this life is in his Son.

Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima. 1 Yohana 5:12

He who has the Son has the life. He who doesn't have God's Son doesn't have the life.

Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu. 1 Yohana 5:13

These things I have written to you who believe in the name of the Son of God, that you may know that you have eternal life, and that you may continue to believe in the name of the Son of God.

Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. 1 Yohana 5:14

This is the boldness which we have toward him, that, if we ask anything according to his will, he listens to us.

Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba. 1 Yohana 5:15

And if we know that he listens to us, whatever we ask, we know that we have the petitions which we have asked of him.

Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo. 1 Yohana 5:16

If anyone sees his brother sinning a sin not leading to death, he shall ask, and God will give him life for those who sin not leading to death. There is a sin leading to death. I don't say that he should make a request concerning this.

Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti. 1 Yohana 5:17

All unrighteousness is sin, and there is a sin not leading to death.

Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi. 1 Yohana 5:18

We know that whoever is born of God doesn't sin, but he who was born of God keeps himself, and the evil one doesn't touch him.

Twajua ya kuwa sisi tu wa Mungu; na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu. 1 Yohana 5:19

We know that we are of God, and the whole world lies in the power of the evil one.

Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele. 1 Yohana 5:20

We know that the Son of God has come, and has given us an understanding, that we know him who is true, and we are in him who is true, in his Son Jesus Christ. This is the true God, and eternal life.

Watoto wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu. 1 Yohana 5:21

Little children, keep yourselves from idols.