Usinipite Mwokozi Unisikue

Usinipite mwokozi, unisikie;
unapozuru wengine usinipite

Yesu, Yesu, unisikie;
unapozuru wengine, usinipite.

Kiti chako cha rehema, nakitazama;
Magoti napiga pale, nisamehewe.


Yesu, Yesu, unisikie;
unapozuru wengine, usinipite.

Sina ya kutegemea, ila wewe tu;
Uso wako uwe kwangu; Nakuabudu.


Yesu, Yesu, unisikie;
unapozuru wengine, usinipite.

U mfariji peke yako; sina Mbinguni,
wala duniani pote, Bwana mwingine.


Yesu, Yesu, unisikie;
unapozuru wengine, usinipite.

# This is the official swahili version of
pass me not Oh Gracious saviour hymn
0 Comments

  • {{ item.name }}

Share your ThoughtsShare:

Sifa Lyrics

Social Links