Sefania 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
Sefania 1 (Swahili) Zephaniah 1 (English)

Neno la Bwana lililomjia Sefania, mwana wa Kushi, mwana wa Gedalia, mwana wa Amaria, mwana wa Hezekia; katika siku za Yosia, mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda. Sefania 1:1

The word of Yahweh which came to Zephaniah, the son of Cushi, the son of Gedaliah, the son of Amariah, the son of Hezekiah, in the days of Josiah, the son of Amon, king of Judah.

Nitavikomesha kabisa vitu vyote, visionekane juu ya uso wa nchi, asema Bwana. Sefania 1:2

I will utterly sweep away everything off of the surface of the earth, says Yahweh.

Nitamkomesha mwanadamu na mnyama; nitakomesha ndege wa angani, na samaki wa baharini, na hayo makwazo pamoja na wabaya; nami nitamkatilia mbali mwanadamu, asionekane juu ya uso wa nchi, asema Bwana. Sefania 1:3

I will sweep away man and animal. I will sweep away the birds of the sky, the fish of the sea, and the heaps of rubble with the wicked. I will cut off man from the surface of the earth, says Yahweh.

Nami nitaunyosha mkono wangu juu ya Yuda, na juu ya watu wote wakaao Yerusalemu; nami nitayakatilia mbali mabaki ya Baali, yasionekane mahali hapa, na hilo jina la Wakemari pamoja na makuhani; Sefania 1:4

I will stretch out my hand against Judah, and against all the inhabitants of Jerusalem. I will cut off the remnant of Baal from this place: the name of the idolatrous and pagan priests,

na wale walisujudiao jeshi la mbinguni juu ya dari za nyumba; na hao waabuduo, waapao kwa Bwana na kuapa pia kwa Malkamu; Sefania 1:5

those who worship the host of the sky on the housetops, those who worship and swear by Yahweh and also swear by Malcam,

na hao waliorudi nyuma, na kuacha kumfuata Bwana; na hao wasiomtafuta Bwana, wala kumwulizia. Sefania 1:6

those who have turned back from following Yahweh, and those who haven't sought Yahweh nor inquired after him.

Nyamaza kimya mbele za Bwana MUNGU; Kwa maana siku ya Bwana i karibu; Kwa kuwa Bwana ameweka tayari dhabihu, Amewatakasa wageni wake. Sefania 1:7

Be silent at the presence of the Lord Yahweh, for the day of Yahweh is at hand. For Yahweh has prepared a sacrifice. He has consecrated his guests.

Na itakuwa, katika siku ile ya dhabihu ya Bwana, nitawaadhibu wakuu, na wana wa mfalme, na watu wote waliovaa mavazi ya kigeni. Sefania 1:8

It will happen in the day of Yahweh's sacrifice, that I will punish the princes, the king's sons, and all those who as are clothed with foreign clothing.

Na katika siku ile nitawaadhibu hao wote warukao juu ya kizingiti, waijazao nyumba ya bwana wao udhalimu na udanganyifu. Sefania 1:9

In that day, I will punish all those who leap over the threshold, who fill their master's house with violence and deceit.

Na katika siku ile, asema Bwana kutakuwako sauti ya kilio kutoka lango la samaki, na mlio mkuu katika mtaa wa pili, na mshindo mkuu kutoka milimani. Sefania 1:10

In that day, says Yahweh, there will be the noise of a cry from the fish gate, a wailing from the second quarter, and a great crashing from the hills.

Haya! Lieni, ninyi mkaao katika Makteshi, maana wafanya biashara wote wameangamia; hao wote waliokuwa na mizigo ya fedha wamekatiliwa mbali. Sefania 1:11

Wail, you inhabitants of Maktesh, for all the people of Canaan are undone! All those who were loaded with silver are cut off.

Kisha itakuwa wakati ule, nitauchunguza Yerusalemu kwa taa; nami nitawaadhibu watu walioganda juu ya sira zao; wasemao katika mioyo yao, Bwana hatatenda mema, wala hatatenda mabaya. Sefania 1:12

It will happen at that time, that I will search Jerusalem with lamps, and I will punish the men who are settled on their dregs, who say in their heart, "Yahweh will not do good, neither will he do evil."

Na huko utajiri wao utakuwa mateka, na nyumba zao zitakuwa ukiwa; naam, watajenga nyumba, lakini hawatakaa ndani yake; nao watapanda mizabibu, lakini hawatakunywa divai yake. Sefania 1:13

Their wealth will become a spoil, and their houses a desolation. Yes, they will build houses, but won't inhabit them. They will plant vineyards, but won't drink their wine.

Hiyo siku ya Bwana iliyo kuu i karibu; I karibu, nayo inafanya haraka sana; Naam, sauti ya siku ya Bwana; Shujaa hulia kwa uchungu mwingi huko! Sefania 1:14

The great day of Yahweh is near. It is near, and hurries greatly, the voice of the day of Yahweh. The mighty man cries there bitterly.

Siku ile ni siku ya ghadhabu, Siku ya fadhaa na dhiki, Siku ya uharibifu na ukiwa, Siku ya giza na utusitusi, Siku ya mawingu na giza kuu, Sefania 1:15

That day is a day of wrath, a day of distress and anguish, a day of trouble and ruin, a day of darkness and gloom, a day of clouds and blackness,

Siku ya tarumbeta na ya kamsa, Juu ya miji yenye maboma, Juu ya buruji zilizo ndefu sana. Sefania 1:16

a day of the trumpet and alarm, against the fortified cities, and against the high battlements.

Nami nitawaletea wanadamu dhiki, hata watakwenda kama vipofu, kwa sababu wamemtenda Bwana dhambi; na damu yao itamwagwa kama mavumbi, na nyama yao kama mavi. Sefania 1:17

I will bring distress on men, that they will walk like blind men, because they have sinned against Yahweh, and their blood will be poured out like dust, and their flesh like dung.

Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya Bwana; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, ukomo wa kutisha. Sefania 1:18

Neither their silver nor their gold will be able to deliver them in the day of Yahweh's wrath, but the whole land will be devoured by the fire of his jealousy; for he will make an end, yes, a terrible end, of all those who dwell in the land.