Filemoni 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
Filemoni 1 (Swahili) Philemon 1 (English)

Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu, na Timotheo aliye ndugu yetu, kwa Filemoni mpendwa wetu, mtenda kazi pamoja nasi, Filemoni 1:1

Paul, a prisoner of Christ Jesus, and Timothy our brother, to Philemon, our beloved fellow worker,

na kwa Afia, ndugu yetu, na kwa Arkipo askari mwenzetu, na kwa kanisa lililo katika nyumba yako. Filemoni 1:2

to the beloved Apphia, to Archippus, our fellow soldier, and to the assembly in your house:

Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu, Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo. Filemoni 1:3

Grace to you and peace from God our Father and the Lord Jesus Christ.

Namshukuru Mungu wangu sikuzote, nikikukumbuka katika maombi yangu; Filemoni 1:4

I thank my God always, making mention of you in my prayers,

nikisikia habari za upendo wako na imani uliyo nayo kwa Bwana Yesu na kwa watakatifu wote; Filemoni 1:5

hearing of your love, and of the faith which you have toward the Lord Jesus, and toward all the saints;

ili kwamba ushirika wa imani yako ufanye kazi yake, katika ujuzi wa kila kitu chema kilicho kwetu, katika Kristo. Filemoni 1:6

that the fellowship of your faith may become effective, in the knowledge of every good thing which is in us in Christ Jesus.

Maana nalikuwa na furaha nyingi na faraja kwa sababu ya upendo wako, kwa kuwa mioyo ya watakatifu imeburudishwa nawe, ndugu yangu. Filemoni 1:7

For we have much joy and comfort in your love, because the hearts of the saints have been refreshed through you, brother.

Kwa hiyo, nijapokuwa nina ujasiri katika Kristo kukuagiza likupasalo; Filemoni 1:8

Therefore, though I have all boldness in Christ to command you that which is appropriate,

lakini, kwa ajili ya upendo nakusihi, kwa kuwa ni kama nilivyo, Paulo mzee, na sasa mfungwa wa Kristo Yesu pia. Filemoni 1:9

yet for love's sake I rather beg, being such a one as Paul, the aged, but also a prisoner of Jesus Christ.

Nakusihi kwa ajili ya mtoto wangu niliyemzaa katika vifungo vyangu, yaani, Onesimo; Filemoni 1:10

I beg you for my child, whom I have become the father of in my chains, Onesimus,{Onesimus means "useful."}

ambaye zamani alikuwa hakufai, bali sasa akufaa sana, wewe na mimi pia; Filemoni 1:11

who once was useless to you, but now is useful to you and to me.

niliyemtuma kwako, yeye mwenyewe, maana ni moyo wangu hasa; Filemoni 1:12

I am sending him back. Therefore receive him, that is, my own heart,

ambaye mimi nalitaka akae kwangu, apate kunitumikia badala yako katika vifungo vya Injili. Filemoni 1:13

whom I desired to keep with me, that on your behalf he might serve me in my chains for the Gospel.

Lakini sikutaka kutenda neno lo lote isipokuwa kwa shauri lako, ili kwamba wema wako usiwe kama kwa lazima, bali kwa hiari. Filemoni 1:14

But I was willing to do nothing without your consent, that your goodness would not be as of necessity, but of free will.

Maana, labda ndiyo sababu alitengwa nawe kwa muda, ili uwe naye tena milele; Filemoni 1:15

For perhaps he was therefore separated from you for a while, that you would have him forever,

tokea sasa, si kama mtumwa, bali zaidi ya mtumwa, ndugu mpendwa; kwangu mimi sana, na kwako wewe zaidi sana, katika mwili na katika Bwana. Filemoni 1:16

no longer as a slave, but more than a slave, a beloved brother, especially to me, but how much rather to you, both in the flesh and in the Lord.

Basi kama ukiniona mimi kuwa mshirika nawe, mpokee huyu kama mimi mwenyewe. Filemoni 1:17

If then you count me a partner, receive him as you would receive me.

Na kama amekudhulumu, au unamwia kitu, ukiandike hicho juu yangu. Filemoni 1:18

But if he has wronged you at all, or owes you anything, put that to my account.

Mimi Paulo nimeandika kwa mkono wangu mwenyewe, mimi nitalipa. Sikuambii kwamba nakuwia hata nafsi yako. Filemoni 1:19

I, Paul, write this with my own hand: I will repay it (not to mention to you that you owe to me even your own self besides).

Naam, ndugu yangu, nipate faida kwako katika Bwana; uniburudishe moyo wangu katika Kristo. Filemoni 1:20

Yes, brother, let me have joy from you in the Lord. Refresh my heart in the Lord.

Kwa kuwa nakuamini kutii kwako ndiyo maana nimekuandikia, nikijua ya kuwa utafanya zaidi ya hayo nisemayo. Filemoni 1:21

Having confidence in your obedience, I write to you, knowing that you will do even beyond what I say.

Na pamoja na hayo uniwekee tayari mahali pa kukaa; maana nataraji ya kwamba kwa maombi yenu mtajaliwa kunipata. Filemoni 1:22

Also, prepare a guest room for me, for I hope that through your prayers I will be restored to you.

Epafra, aliyefungwa pamoja nami katika Kristo Yesu, akusalimu; Filemoni 1:23

Epaphras, my fellow prisoner in Christ Jesus, greets you,

na Marko, na Aristarko, na Dema, na Luka, watendao kazi pamoja nami. Filemoni 1:24

as do Mark, Aristarchus, Demas, and Luke, my fellow workers.

Neema ya Bwana Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu. Filemoni 1:25

The grace of our Lord Jesus Christ be with your spirit. Amen.