Yoeli 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yoeli 2 (Swahili) Joel 2 (English)

Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Pigeni na kelele katika mlima wangu mtakatifu; Wenyeji wote wa nchi na watetemeke; Kwa maana siku ya Bwana inakuja. Kwa sababu inakaribia; Yoeli 2:1

Blow you the trumpet in Zion, And sound an alarm in my holy mountain! Let all the inhabitants of the land tremble, For the day of Yahweh comes, For it is close at hand:

siku ya giza na weusi, siku ya mawingu na giza kuu. Kama mapambazuko yakitandazwa juu ya milima, hao ni wakuu, tena wenye nguvu, mfano wao haukuwako kamwe, wala hautakuwako baada ya hao, hata katika miaka ya vizazi vingi. Yoeli 2:2

A day of darkness and gloominess, A day of clouds and thick darkness. As the dawn spreading on the mountains, A great and strong people; There has never been the like, Neither will there be any more after them, Even to the years of many generations.

Moto unakula mbele yao; na nyuma yao miali ya moto inateketeza; hiyo nchi inafanana na bustani ya Adeni mbele yao, na nyuma yao imekuwa jangwa tupu; naam, hakuna aliyeokoka asipatikane nao. Yoeli 2:3

A fire devours before them, And behind them, a flame burns. The land is as the garden of Eden before them, And behind them, a desolate wilderness. Yes, and no one has escaped them.

Kuonekana kwao ni kama kuonekana kwa farasi; na kama wapanda farasi ndivyo wanavyopiga mbio. Yoeli 2:4

The appearance of them is as the appearance of horses, And as horsemen, so do they run.

Kama mshindo wa magari ya vita juu ya vilele vya milima, ndivyo warukavyo; kama mshindo wa miali ya moto ilapo mabua makavu, kama mashujaa waliopangwa tayari kwa vita. Yoeli 2:5

Like the noise of chariots on the tops of the mountains do they leap, Like the noise of a flame of fire that devours the stubble, As a strong people set in battle array.

Mbele yao watu wanahangaika; nyuso zote zimegeuka kuwa nyeupe kwa hofu. Yoeli 2:6

At their presence the peoples are in anguish. All faces have grown pale.

Hupiga mbio kama mashujaa; huupanda ukuta kama watu wa vita; nao huendelea mbele kila mmoja katika njia zake, wala hawapotoshi safu zao. Yoeli 2:7

They run like mighty men. They climb the wall like warriors. They each march in his line, and they don't swerve off course.

Wala hapana mmoja amsukumaye mwenzake; huendelea mbele kila mmoja katika njia yake; hujifanyizia njia kwa nguvu kati ya silaha, wala hawaachi kuifuata njia yao. Yoeli 2:8

Neither does one jostle another; They march everyone in his path, And they burst through the defenses, And don't break ranks.

Huurukia mji; hupiga mbio juu ya ukuta; hupanda na kuingia ndani ya nyumba; huingia madirishani kama aingiavyo mwivi. Yoeli 2:9

They rush on the city. They run on the wall. They climb up into the houses. They enter in at the windows like thieves.

Nchi inatetemeka mbele yao; mbingu zinatetemeka; jua na mwezi hutiwa giza, na nyota huacha kuangaza; Yoeli 2:10

The earth quakes before them. The heavens tremble. The sun and the moon are darkened, And the stars withdraw their shining.

naye Bwana anatoa sauti yake mbele ya jeshi lake; maana matuo yake ni makubwa sana; kwa maana yeye ni hodari atekelezaye neno lake; kwa kuwa siku ya Bwana ni kuu, yenye kitisho sana; naye ni nani awezaye kuistahimili? Yoeli 2:11

Yahweh thunders his voice before his army; For his forces are very great; For he is strong who obeys his command; For the day of Yahweh is great and very awesome, And who can endure it?

Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea; Yoeli 2:12

"Yet even now," says Yahweh, "turn to me with all your heart, And with fasting, and with weeping, and with mourning."

rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya. Yoeli 2:13

Tear your heart, and not your garments, And turn to Yahweh, your God; For he is gracious and merciful, Slow to anger, and abundant in loving kindness, And relents from sending calamity.

N'nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka, na kutuachia baraka nyuma yake, naam, sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji, kwa Bwana, Mungu wenu? Yoeli 2:14

Who knows? He may turn and relent, And leave a blessing behind him, Even a meal offering and a drink offering to Yahweh, your God.

Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Takaseni saumu, kusanyeni kusanyiko kuu; Yoeli 2:15

Blow the trumpet in Zion! Sanctify a fast. Call a solemn assembly.

Kusanyeni watu, litakaseni kusanyiko, Kusanyeni wazee, kusanyeni watoto, Na hao wanyonyao maziwa; Bwana arusi na atoke chumbani mwake, Na bibi arusi katika hema yake. Yoeli 2:16

Gather the people. Sanctify the assembly. Assemble the elders. Gather the children, and those who suck the breasts. Let the bridegroom go forth from his room, And the bride out of her chamber.

Hao makuhani, wahudumu wa Bwana, na walie Kati ya patakatifu na madhabahu, Na waseme, Uwaachilie watu wako, Ee Bwana, Wala usiutoe urithi wako upate aibu, Hata mataifa watawale juu yao; Kwani waseme kati ya watu, Yuko wapi Mungu wao? Yoeli 2:17

Let the priests, the ministers of Yahweh, weep between the porch and the altar, And let them say, "Spare your people, Yahweh, And don't give your heritage to reproach, That the nations should rule over them. Why should they say among the peoples, 'Where is their God?'"

Hapo ndipo Bwana alipoona wivu kwa ajili ya nchi yake, akawahurumia watu wake. Yoeli 2:18

Then Yahweh was jealous for his land, And had pity on his people.

Bwana akajibu, akawaambia watu wake; Tazameni, nitawaletea nafaka, na divai, na mafuta, nanyi mtashiba kwa vitu hivyo; wala sitawafanya tena kuwa aibu kati ya mataifa; Yoeli 2:19

Yahweh answered his people, "Behold, I will send you grain, new wine, and oil, And you will be satisfied with them; And I will no more make you a reproach among the nations.

lakini jeshi lililotoka kaskazini nitaliondolea mbali nanyi, nami nitalifukuza mpaka nchi ya ukame na ukiwa; sehemu yake iliyo mbele itaingia katika bahari ya mashariki, na sehemu yake iliyo nyuma itaingia katika bahari ya magharibi; na uvundo wake utapanda juu, na harufu yake mbaya itapanda juu, kwa sababu ametenda mambo makubwa. Yoeli 2:20

But I will remove the northern army far away from you, And will drive it into a barren and desolate land, Its front into the eastern sea, And its back into the western sea; And its stench will come up, And its bad smell will rise." Surely he has done great things.

Ee nchi, usiogope; furahi na kushangilia; kwa kuwa Bwana ametenda mambo makuu. Yoeli 2:21

Land, don't be afraid. Be glad and rejoice, for Yahweh has done great things.

Msiogope, enyi wanyama wa kondeni; maana malisho ya jangwani yanatoa miche, na huo mti unazaa matunda yake, mtini na mzabibu inatoa nguvu zake. Yoeli 2:22

Don't be afraid, you animals of the field; For the pastures of the wilderness spring up, For the tree bears its fruit. The fig tree and the vine yield their strength.

Furahini, basi, enyi wana wa Sayuni, mkamfurahie Bwana, Mungu wenu; kwa kuwa yeye huwapa ninyi mvua ya masika, kwa kipimo cha haki, naye huwanyeshea mvua, mvua ya masika, na mvua ya vuli, kama kwanza. Yoeli 2:23

"Be glad then, you children of Zion, And rejoice in Yahweh, your God; For he gives you the former rain in just measure, And he causes the rain to come down for you, The former rain and the latter rain, As before.

Na sakafu za kupepetea zitajaa ngano, na mashinikizo yatafurika kwa divai na mafuta. Yoeli 2:24

The threshing floors will be full of wheat, And the vats will overflow with new wine and oil.

Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu. Yoeli 2:25

I will restore to you the years that the swarming locust has eaten, The great locust, the grasshopper, and the caterpillar, My great army, which I sent among you.

Nanyi mtakula chakula tele na kushiba, na kulihimidi jina la Bwana, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu; na watu wangu hawatatahayari kamwe. Yoeli 2:26

You will have plenty to eat, and be satisfied, And will praise the name of Yahweh, your God, Who has dealt wondrously with you; And my people will never again be disappointed.

Nanyi mtajua ya kuwa mimi ni katikati ya Israeli, na ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, wala hakuna mwingine; na watu wangu hawatatahayari kamwe. Yoeli 2:27

You will know that I am in the midst of Israel, And that I am Yahweh, your God, and there is no one else; And my people will never again be disappointed.

Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; Yoeli 2:28

"It will happen afterward, that I will pour out my Spirit on all flesh; And your sons and your daughters will prophesy. Your old men will dream dreams. Your young men will see visions.

tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu. Yoeli 2:29

And also on the servants and on the handmaids in those days, I will pour out my Spirit.

Nami nitaonyesha mambo ya ajabu katika mbingu na katika dunia, damu, na moto, na minara ya moshi. Yoeli 2:30

I will show wonders in the heavens and in the earth: Blood, fire, and pillars of smoke.

Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo. Yoeli 2:31

The sun will be turned into darkness, And the moon into blood, Before the great and terrible day of Yahweh comes.

Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la Bwana ataponywa; kwa kuwa katika mlima Sayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama Bwana alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao Bwana. Yoeli 2:32

It will happen that whoever will call on the name of Yahweh shall be saved; For in Mount Zion and in Jerusalem there will be those who escape, As Yahweh has said, And among the remnant, those whom Yahweh calls.