Yakobo 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yakobo 1 (Swahili) James 1 (English)

Yakobo, mtumwa wa Mungu, na wa Bwana Yesu Kristo, kwa kabila kumi na mbili waliotawanyika; salamu. Yakobo 1:1

James, a servant of God and of the Lord Jesus Christ, to the twelve tribes which are in the Dispersion: Greetings.

Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; Yakobo 1:2

Count it all joy, my brothers{The word for "brothers" here and where context allows may also be correctly translated "brothers and sisters" or "siblings."}, when you fall into various temptations,

mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Yakobo 1:3

knowing that the testing of your faith produces endurance.

Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno. Yakobo 1:4

Let endurance have its perfect work, that you may be perfect and complete, lacking in nothing.

Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. Yakobo 1:5

But if any of you lacks wisdom, let him ask of God, who gives to all liberally and without reproach; and it will be given to him.

Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. Yakobo 1:6

But let him ask in faith, without any doubting, for he who doubts is like a wave of the sea, driven by the wind and tossed.

Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana. Yakobo 1:7

For let that man not think that he will receive anything from the Lord.

Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote. Yakobo 1:8

He is a double-minded man, unstable in all his ways.

Lakini ndugu asiye na cheo na afurahi kwa kuwa ametukuzwa; Yakobo 1:9

But let the brother in humble circumstances glory in his high position;

bali tajiri kwa kuwa ameshushwa; kwa maana kama ua la majani atatoweka. Yakobo 1:10

and the rich, in that he is made humble, because like the flower in the grass, he will pass away.

Maana jua huchomoza kwa hari, huyakausha majani; ua lake huanguka, uzuri wa umbo lake hupotea; vivyo hivyo naye tajiri atanyauka katika njia zake. Yakobo 1:11

For the sun arises with the scorching wind, and withers the grass, and the flower in it falls, and the beauty of its appearance perishes. So also will the rich man fade away in his pursuits.

Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao. Yakobo 1:12

Blessed is the man who endures temptation, for when he has been approved, he will receive the crown of life, which the Lord promised to those who love him.

Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu. Yakobo 1:13

Let no man say when he is tempted, "I am tempted by God," for God can't be tempted by evil, and he himself tempts no one.

Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. Yakobo 1:14

But each one is tempted, when he is drawn away by his own lust, and enticed.

Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti. Yakobo 1:15

Then the lust, when it has conceived, bears sin; and the sin, when it is full grown, brings forth death.

Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike. Yakobo 1:16

Don't be deceived, my beloved brothers.

Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka. Yakobo 1:17

Every good gift and every perfect gift is from above, coming down from the Father of lights, with whom can be no variation, nor turning shadow.

Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyake. Yakobo 1:18

Of his own will he brought us forth by the word of truth, that we should be a kind of first fruits of his creatures.

Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika; Yakobo 1:19

So, then, my beloved brothers, let every man be swift to hear, slow to speak, and slow to anger;

kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu. Yakobo 1:20

for the anger of man doesn't produce the righteousness of God.

Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu. Yakobo 1:21

Therefore, putting away all filthiness and overflowing of wickedness, receive with humility the implanted word, which is able to save your souls{or, preserve your life.}.

Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. Yakobo 1:22

But be doers of the word, and not only hearers, deluding your own selves.

Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. Yakobo 1:23

For if anyone is a hearer of the word and not a doer, he is like a man beholding his natural face in a mirror;

Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo. Yakobo 1:24

for he sees himself, and goes away, and immediately forgets what kind of man he was.

Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake. Yakobo 1:25

But he who looks into the perfect law, the law of freedom, and continues, not being a hearer who forgets but a doer of the work, this man will be blessed in what he does.

Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai. Yakobo 1:26

If anyone among you thinks himself to be religious while he doesn't bridle his tongue, but deceives his heart, this man's religion is worthless.

Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa. Yakobo 1:27

Pure religion and undefiled before our God and Father is this: to visit the fatherless and widows in their affliction, and to keep oneself unstained by the world.