Habakuki 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
Habakuki 3 (Swahili) Habakkuk 3 (English)

Sala ya nabii Habakuki. Habakuki 3:1

A prayer of Habakkuk, the prophet, set to victorious music.

Ee Bwana, nimesikia habari zako, nami naogopa; Ee Bwana, fufua kazi yako katikati ya miaka; Katikati ya miaka tangaza habari yake; Katika ghadhabu kumbuka rehema. Habakuki 3:2

Yahweh, I have heard of your fame. I stand in awe of your deeds, Yahweh. Renew your work in the midst of the years. In the midst of the years make it known. In wrath, you remember mercy.

Mungu alikuja kutoka Temani, Yeye aliye mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake ukazifunika mbingu, Nayo dunia ikajaa sifa yake. Habakuki 3:3

God came from Teman, The Holy One from Mount Paran. Selah. His glory covered the heavens, And his praise filled the earth.

Mwangaza wake ulikuwa kama nuru; Alikuwa na mishale ya nuru ubavuni pake; Ndipo ulipofichwa uweza wake. Habakuki 3:4

His splendor is like the sunrise. Rays shine from his hand, where his power is hidden.

Mbele zake ilikwenda tauni, Na makaa ya moto yakatoka miguuni pake. Habakuki 3:5

Plague went before him, And pestilence followed his feet.

Akasimama, akaitetemesha dunia; Akatazama, akawasitusha mataifa; Na milima ya zamani ikatawanyika; Vilima vya kale vikainama; Miendo yake ilikuwa kama siku za kale. Habakuki 3:6

He stood, and shook the earth. He looked, and made the nations tremble. The ancient mountains were crumbled. The age-old hills collapsed. His ways are eternal.

Naliziona hema za Kushani katika taabu; Mapazia ya nchi ya Midiani yakatetemeka. Habakuki 3:7

I saw the tents of Cushan in affliction. The dwellings of the land of Midian trembled.

Je! Bwana aliikasirikia mito? Je! Hasira yako ilikuwa juu ya mito, Au ghadhabu yako juu ya bahari, Hata ukapanda farasi zako, Katika magari yako ya wokovu? Habakuki 3:8

Was Yahweh displeased with the rivers? Was your anger against the rivers, Or your wrath against the sea, That you rode on your horses, On your chariots of salvation?

Uta wako ukafanywa wazi kabisa; Viapo walivyopewa kabila vilikuwa neno thabiti; Ukaipasua nchi kwa mito. Habakuki 3:9

You uncovered your bow. You called for your sworn arrows. Selah. You split the earth with rivers.

Milima ilikuona, ikaogopa; Gharika ya maji ikapita; Vilindi vikatoa sauti yake, Vikainua juu mikono yake. Habakuki 3:10

The mountains saw you, and were afraid. The tempest of waters passed by. The deep roared and lifted up its hands on high.

Jua na mwezi vikasimama makaoni mwao; Mbele ya nuru ya mishale yako ilipotapakaa, Mbele ya mwangaza wa mkuki wako umeremetao. Habakuki 3:11

The sun and moon stood still in the sky, At the light of your arrows as they went, At the shining of your glittering spear.

Ulikwenda katikati ya nchi kwa ghadhabu; Ukawapura mataifa kwa hasira. Habakuki 3:12

You marched through the land in wrath. You threshed the nations in anger.

Ukatokea kwa ajili ya wokovu wa watu wako, Kwa ajili ya wokovu wa masihi wako; Ukakiponda kichwa cha nyumba ya waovu, Ukiuweka wazi msingi hata mwambani. Habakuki 3:13

You went forth for the salvation of your people, For the salvation of your anointed. You crushed the head of the land of wickedness. You stripped them head to foot. Selah.

Ukakichoma kichwa cha mashujaa wake kwa fimbo zao wenyewe; Wakaja kama kisulisuli ili kunitawanya; Kama wakifurahi kuwameza maskini kwa siri. Habakuki 3:14

You pierced the heads of his warriors with their own spears. They came as a whirlwind to scatter me, Gloating as if to devour the wretched in secret.

Ukaikanyaga bahari kwa farasi zako, Chungu ya maji yenye nguvu. Habakuki 3:15

You trampled the sea with your horses, Churning mighty waters.

Nikasikia, na tumbo langu likatetemeka, Midomo yangu ikatikisika kwa sauti ile; Ubovu ukaingia mifupani mwangu, Nikatetemeka katika mahali pangu; Ili nipate kuingoja ile siku ya dhiki, Kundi lao washambuliao wakweapo juu ya watu. Habakuki 3:16

I heard, and my body trembled. My lips quivered at the voice. Rottenness enters into my bones, and I tremble in my place, Because I must wait quietly for the day of trouble, For the coming up of the people who invade us.

Maana mtini hautachanua maua, Wala mizabibuni hamtakuwa na matunda; Taabu ya mzeituni itakuwa bure, Na mashamba hayatatoa chakula; Zizini hamtakuwa na kundi, Wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng'ombe; Habakuki 3:17

For though the fig tree doesn't flourish, Nor fruit be in the vines; The labor of the olive fails, The fields yield no food; The flocks are cut off from the fold, And there is no herd in the stalls:

Walakini nitamfurahia Bwana Nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu. Habakuki 3:18

Yet I will rejoice in Yahweh. I will be joyful in the God of my salvation!

YEHOVA, aliye Bwana, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka.

Habakuki 3:19

Yahweh, the Lord, is my strength. He makes my feet like deer's feet, And enables me to go in high places. For the music director, on my stringed instruments.