2 Yohana 1 Swahili & English
Listen/Download Audio2 Yohana 1 (Swahili) | 2nd John 1 (English) |
---|---|
Mzee, kwa mama mteule na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke yangu, bali na wote waijuao ile kweli; 2 Yohana 1:1 |
The elder, to the chosen lady and her children, whom I love in truth; and not I only, but also all those who know the truth; |
kwa ajili ya hiyo kweli ikaayo ndani yetu, nayo itakuwa pamoja nasi hata milele. 2 Yohana 1:2 |
for the truth's sake, which remains in us, and it will be with us forever: |
Neema, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Yesu Kristo Mwana wa Baba, zitakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo. 2 Yohana 1:3 |
Grace, mercy, and peace will be with us, from God the Father, and from the Lord Jesus Christ, the Son of the Father, in truth and love. |
Nalifurahi mno kwa kuwa nimewaona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile tulivyopokea amri kwa Baba. 2 Yohana 1:4 |
I rejoice greatly that I have found some of your children walking in truth, even as we have been commanded by the Father. |
Na sasa mama, nakuomba, si kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo, kwamba tupendane. 2 Yohana 1:5 |
Now I beg you, dear lady, not as though I wrote to you a new commandment, but that which we had from the beginning, that we love one another. |
Na huu ndio upendo: tuenende kwa kuzifuata amri zake. Hii ndiyo ile amri, kama mlivyosikia tangu mwanzo kwamba mwenende katika hiyo. 2 Yohana 1:6 |
This is love, that we should walk according to his commandments. This is the commandment, even as you heard from the beginning, that you should walk in it. |
Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, wasiokiri ya kuwa Yesu Kristo yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na mpinga Kristo. 2 Yohana 1:7 |
For many deceivers have gone out into the world, those who don't confess that Jesus Christ came in the flesh. This is the deceiver and the Antichrist. |
Jiangalieni nafsi zenu msiyapoteze mliyoyatenda, bali mpokee thawabu timilifu. 2 Yohana 1:8 |
Watch yourselves, that we don't lose the things which we have accomplished, but that we receive a full reward. |
Kila apitaye cheo, wala asidumu katika mafundisho ya Kristo, yeye hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho hayo, huyo ana Baba na Mwana pia. 2 Yohana 1:9 |
Whoever transgresses and doesn't remain in the teaching of Christ, doesn't have God. He who remains in the teaching, the same has both the Father and the Son. |
Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu. 2 Yohana 1:10 |
If anyone comes to you, and doesn't bring this teaching, don't receive him into your house, and don't welcome him, |
Maana yeye ampaye salamu azishiriki kazi zake mbovu. 2 Yohana 1:11 |
for he who welcomes him participates in his evil works. |
Kwa kuwa ninayo mambo mengi, sitaki kuyaandika kwa karatasi na wino; lakini nataraji kuja kwenu, na kusema nanyi uso kwa uso, ili furaha yetu iwe imetimizwa. 2 Yohana 1:12 |
Having many things to write to you, I don't want to do so with paper and ink, but I hope to come to you, and to speak face to face, that our joy may be made full. |
Watoto wa ndugu yako aliye mteule, wakusalimu. 2 Yohana 1:13 |
The children of your chosen sister greet you. Amen. |