1 Wathesalonike 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wathesalonike 3 (Swahili) 1st Thessalonians 3 (English)

Basi kwa hiyo, tulipokuwa hatuwezi kuvumilia zaidi, tuliona vema kuachwa Athene peke yetu. 1 Wathesalonike 3:1

Therefore, when we couldn't stand it any longer, we thought it good to be left behind at Athens alone,

Tukamtuma Timotheo ndugu yetu, mtumishi wa Mungu katika Injili ya Kristo, ili kuwafanya ninyi imara na kuwafariji kwa habari ya imani yenu; 1 Wathesalonike 3:2

and sent Timothy, our brother and God's servant in the Gospel of Christ, to establish you, and to comfort you concerning your faith;

mtu asifadhaishwe na dhiki hizi; maana ninyi wenyewe mnajua ya kuwa twawekewa hizo. 1 Wathesalonike 3:3

that no one be moved by these afflictions. For you know that we are appointed to this task.

Kwa kuwa tulipokuwapo kwenu tulitangulia kuwaambia kwamba tutapata dhiki, kama ilivyotukia, nanyi mwajua. 1 Wathesalonike 3:4

For most assuredly, when we were with you, we told you beforehand that we are to suffer affliction, even as it happened, and you know.

Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nalituma mtu ili niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, na taabu yetu ikawa haina faida. 1 Wathesalonike 3:5

For this cause I also, when I couldn't stand it any longer, sent that I might know your faith, for fear that by any means the tempter had tempted you, and our labor would have been in vain.

Lakini Timotheo alipotujia hivi sasa kutoka kwenu, alituletea habari njema za imani yenu na upendo wenu, na ya kwamba mnatukumbuka vema siku zote; mkitamani kutuona sisi vile vile kama sisi kuwaona ninyi. 1 Wathesalonike 3:6

But when Timothy came just now to us from you, and brought us glad news of your faith and love, and that you have good memories of us always, longing to see us, even as we also long to see you;

Kwa sababu hiyo, ndugu, tulifarijiwa kwa habari zenu, katika msiba na dhiki yetu yote, kwa imani yenu. 1 Wathesalonike 3:7

for this cause, brothers, we were comforted over you in all our distress and affliction through your faith.

Kwa kuwa sasa twaishi, ikiwa ninyi mnasimama imara katika Bwana. 1 Wathesalonike 3:8

For now we live, if you stand fast in the Lord.

Maana ni shukrani gani tuwezayo kumlipa Mungu kwa ajili yenu, kwa furaha ile yote tunayoifurahia, kwa sababu yenu mbele za Mungu wetu; 1 Wathesalonike 3:9

For what thanksgiving can we render again to God for you, for all the joy with which we rejoice for your sakes before our God;

usiku na mchana tunapoomba kwa juhudi tupate kuwaona nyuso zenu, na kuyatengeneza mapungufu ya imani yenu? 1 Wathesalonike 3:10

night and day praying exceedingly that we may see your face, and may perfect that which is lacking in your faith?

Basi Mungu mwenyewe, Baba yetu, na Bwana wetu Yesu, atuongoze njia yetu tufike kwenu. 1 Wathesalonike 3:11

Now may our God and Father himself, and our Lord Jesus Christ, direct our way to you;

Bwana na awaongeze na kuwazidisha katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu; 1 Wathesalonike 3:12

and the Lord make you to increase and abound in love one toward another, and toward all men, even as we also do toward you,

apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote. 1 Wathesalonike 3:13

to the end he may establish your hearts blameless in holiness before our God and Father, at the coming of our Lord Jesus with all his saints.