1 Yohana 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Yohana 2 (Swahili) 1st John 2 (English)

Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, 1 Yohana 2:1

My little children, I write these things to you so that you may not sin. If anyone sins, we have a Counselor{Greek Parakleton: Counselor, Helper, Intercessor, Advocate, and Comfortor.} with the Father, Jesus Christ, the righteous.

naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote. 1 Yohana 2:2

And he is the atoning sacrifice{"atoning sacrifice" is from the Greek "hilasmos," an appeasing, propitiating, or the means of appeasement or propitiation-- the sacrifice that turns away God's wrath because of our sin.} for our sins, and not for ours only, but also for the whole world.

Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake. 1 Yohana 2:3

This is how we know that we know him: if we keep his commandments.

Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. 1 Yohana 2:4

One who says, "I know him," and doesn't keep his commandments, is a liar, and the truth isn't in him.

Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake. 1 Yohana 2:5

But whoever keeps his word, God's love has most assuredly been perfected in him. This is how we know that we are in him:

Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda. 1 Yohana 2:6

he who says he remains in him ought himself also to walk just like he walked.

Wapenzi, siwaandikii amri mpya, ila amri ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo. Na hiyo amri ya zamani ni neno lile mlilolisikia. 1 Yohana 2:7

Brothers, I write no new commandment to you, but an old commandment which you had from the beginning. The old commandment is the word which you heard from the beginning.

Tena nawaandikia amri mpya, neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu; kwa kuwa giza linapita na ile nuru ya kweli imekwisha kung'aa. 1 Yohana 2:8

Again, I write a new commandment to you, which is true in him and in you; because the darkness is passing away, and the true light already shines.

Yeye asemaye kwamba yumo nuruni, naye amchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa. 1 Yohana 2:9

He who says he is in the light and hates his brother, is in the darkness even until now.

Yeye ampendaye ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo. 1 Yohana 2:10

He who loves his brother remains in the light, and there is no occasion for stumbling in him.

Bali yeye amchukiaye ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho. 1 Yohana 2:11

But he who hates his brother is in the darkness, and walks in the darkness, and doesn't know where he is going, because the darkness has blinded his eyes.

Nawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake. 1 Yohana 2:12

I write to you, little children, because your sins are forgiven you for his name's sake.

Nawaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu. Nimewaandikia ninyi, watoto, kwa sababu mmemjua Baba. 1 Yohana 2:13

I write to you, fathers, because you know him who is from the beginning. I write to you, young men, because you have overcome the evil one. I write to you, little children, because you know the Father.

Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu. 1 Yohana 2:14

I have written to you, fathers, because you know him who is from the beginning. I have written to you, young men, because you are strong, and the word of God remains in you, and you have overcome the evil one.

Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. 1 Yohana 2:15

Don't love the world, neither the things that are in the world. If anyone loves the world, the Father's love isn't in him.

Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. 1 Yohana 2:16

For all that is in the world, the lust of the flesh, the lust of the eyes, and the pride of life, isn't the Father's, but is the world's.

Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele. 1 Yohana 2:17

The world is passing away with its lusts, but he who does God's will remains forever.

Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho. 1 Yohana 2:18

Little children, these are the end times, and as you heard that the Antichrist is coming, even now many antichrists have arisen. By this we know that it is the end times.

Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu. 1 Yohana 2:19

They went out from us, but they didn't belong to us; for if they had belonged to us, they would have continued with us. But they left, that they might be revealed that none of them belong to us.

Nanyi mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu nanyi mnajua nyote. 1 Yohana 2:20

You have an anointing from the Holy One, and you know the truth.

Sikuwaandikia ninyi kwa sababu hamwijui iliyo kweli, bali kwa sababu mwaijua, tena kwamba hapana uongo wo wote utokao katika hiyo kweli. 1 Yohana 2:21

I have not written to you because you don't know the truth, but because you know it, and because no lie is of the truth.

Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpinga Kristo, yeye amkanaye Baba na Mwana. 1 Yohana 2:22

Who is the liar but he who denies that Jesus is the Christ? This is the Antichrist, he who denies the Father and the Son.

Kila amkanaye Mwana, hanaye Baba; amkiriye Mwana anaye Baba pia. 1 Yohana 2:23

Whoever denies the Son, the same doesn't have the Father. He who confesses the Son has the Father also.

Ninyi basi, hilo mlilolisikia tangu mwanzo na likae ndani yenu. Ikiwa hilo mlilolisikia tangu mwanzo linakaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya Mwana, na ndani ya Baba. 1 Yohana 2:24

Therefore, as for you, let that remain in you which you heard from the beginning. If that which you heard from the beginning remains in you, you also will remain in the Son, and in the Father.

Na hii ndiyo ahadi aliyotuahidia, yaani, uzima wa milele. 1 Yohana 2:25

This is the promise which he promised us, the eternal life.

Nimewaandikia haya katika habari za watu wale wanaotaka kuwapoteza. 1 Yohana 2:26

These things I have written to you concerning those who would lead you astray.

Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake. 1 Yohana 2:27

As for you, the anointing which you received from him remains in you, and you don't need for anyone to teach you. But as his anointing teaches you concerning all things, and is true, and is no lie, and even as it taught you, you will remain in him.

Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake, ili kusudi, atakapofunuliwa, mwe na ujasiri, wala msiaibike mbele zake katika kuja kwake. 1 Yohana 2:28

Now, little children, remain in him, that when he appears, we may have boldness, and not be ashamed before him at his coming.

Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa kila atendaye haki amezaliwa na yeye. 1 Yohana 2:29

If you know that he is righteous, you know that everyone who practices righteousness is born of him.