Yona 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yona 1 (Swahili) Jonah 1 (English)

Basi neno la Bwana lilimjia Yona, mwana wa Amitai, kusema, Yona 1:1

Now the word of Yahweh came to Jonah the son of Amittai, saying,

Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukapige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu. Yona 1:2

"Arise, go to Nineveh, that great city, and preach against it, for their wickedness has come up before me."

Lakini Yona akaondoka akimbilie Tarshishi, apate kujiepusha na uso wa Bwana; akatelemka hata Yafa, akaona merikebu inayokwenda Tarshishi; basi, akatoa nauli, akapanda merikebuni, aende pamoja nao Tarshishi, ajiepushe na uso wa Bwana. Yona 1:3

But Jonah rose up to flee to Tarshish from the presence of Yahweh. He went down to Joppa, and found a ship going to Tarshish; so he paid its fare, and went down into it, to go with them to Tarshish from the presence of Yahweh.

Lakini Bwana alituma upepo mkuu baharini, ikawa tufani kubwa baharini, hata merikebu ikawa karibu na kuvunjika. Yona 1:4

But Yahweh sent out a great wind on the sea, and there was a mighty tempest on the sea, so that the ship was likely to break up.

Basi wale mabaharia wakaogopa, kila mtu akamwomba mungu wake; nao wakatupa baharini shehena iliyokuwa merikebuni, ili kuupunguza uzito wake. Lakini Yona alikuwa ameshuka hata pande za ndani za merikebu; akajilaza, akapata usingizi. Yona 1:5

Then the mariners were afraid, and cried every man to his god. They threw the cargo that was in the ship into the sea, to lighten it. But Jonah had gone down into the innermost parts of the ship, and he was laying down, and was fast asleep.

Basi nahodha akamwendea, akamwambia, Una nini, Ewe ulalaye usingizi? Amka, ukamwombe Mungu wako; labda Mungu huyo atatukumbuka, tusipotee. Yona 1:6

So the shipmaster came to him, and said to him, "What do you mean, sleeper? Arise, call on your gods! Maybe the gods will notice us, so that we won't perish."

Wakasemezana kila mtu na mwenzake, Haya, na mpige kura, mpate kujua mabaya haya yametupata kwa sababu ya nani. Basi wakapiga kura, nayo kura ikamwangukia Yona. Yona 1:7

They all said to each other, "Come, let us cast lots, that we may know for whose cause this evil is on us." So they cast lots, and the lot fell on Jonah.

Ndipo wakamwambia, Tafadhali utuambie, wewe ambaye mabaya haya yametupata kwa sababu yako; kazi yako ni kazi gani? Nawe umetoka wapi? Nchi yako ni nchi ipi? Nawe u mtu wa kabila gani? Yona 1:8

Then they asked him, "Tell us, please, for whose cause this evil is on us. What is your occupation? Where do you come from? What is your country? Of what people are you?"

Akawaambia, Mimi ni Mwebrania; nami namcha Bwana, Mungu wa mbingu, aliyeziumba bahari na nchi kavu. Yona 1:9

He said to them, "I am a Hebrew, and I fear Yahweh, the God of heaven, who has made the sea and the dry land."

Ndipo watu wale wakaogopa mno, wakamwambia, Ni jambo gani hili ulilolitenda! Kwa maana watu wale walijua ya kuwa amekimbia, ajiepushe na uso wa Bwana, kwa sababu alikuwa amewajulisha. Yona 1:10

Then were the men exceedingly afraid, and said to him, "What is this that you have done?" For the men knew that he was fleeing from the presence of Yahweh, because he had told them.

Basi wakamwambia, Tukutende nini, ili bahari itulie? Kwa maana bahari ilikuwa inazidi kuchafuka. Yona 1:11

Then said they to him, "What shall we do to you, that the sea may be calm to us?" For the sea grew more and more tempestuous.

Naye akawaambia, Nikamateni, mnitupe baharini; basi bahari itatulia; kwa maana najua ya kuwa ni kwa ajili yangu tufani hii imewapata. Yona 1:12

He said to them, "Take me up, and throw me into the sea. Then the sea will be calm for you; for I know that because of me this great tempest is on you."

Lakini wale watu wakavuta makasia kwa nguvu, ili wapate kurudi pwani, wasiweze; kwa maana bahari ilizidi kuwachafukia sana. Yona 1:13

Nevertheless the men rowed hard to get them back to the land; but they could not, for the sea grew more and more tempestuous against them.

Basi wakamlilia Bwana, wakasema, Twakuomba, Ee Bwana, twakuomba, tusiangamie kwa ajili ya uhai wa mtu huyu, wala usitupatilize kwa ajili ya damu isiyo na hatia; kwa maana wewe, Bwana, umefanya kama ulivyopenda. Yona 1:14

Therefore they cried to Yahweh, and said, "We beg you, Yahweh, we beg you, let us not perish for this man's life, and don't lay on us innocent blood; for you, Yahweh, have done as it pleased you."

Basi wakamkamata Yona, wakamtupa baharini, nayo bahari ikaacha kuchafuka. Yona 1:15

So they took up Jonah, and threw him into the sea; and the sea ceased its raging.

Ndipo wale watu wakamwogopa Bwana mno, wakamtolea Bwana sadaka, na kuweka nadhiri. Yona 1:16

Then the men feared Yahweh exceedingly; and they offered a sacrifice to Yahweh, and made vows.

Bwana akaweka tayari samaki mkubwa ili ammeze Yona, naye Yona akawa ndani ya tumbo la samaki yule muda wa siku tatu, mchana na usiku. Yona 1:17

Yahweh prepared a great fish to swallow up Jonah, and Jonah was in the belly of the fish three days and three nights.