Yoeli 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yoeli 3 (Swahili) Joel 3 (English)

Kwa maana, angalieni, siku zile, na wakati ule, nitakapowarudisha mateka wa Yuda na Yerusalemu, Yoeli 3:1

"For, behold, in those days, And in that time, When I restore the fortunes of Judah and Jerusalem,

nitakusanya mataifa yote, nami nitawaleta chini katika bonde la Yehoshafau, na huko nitawahukumu kwa ajili ya watu wangu, na kwa ajili ya urithi wangu, Israeli, ambao wamewatawanya kati ya mataifa, na kuigawanya nchi yangu. Yoeli 3:2

I will gather all nations, And will bring them down into the valley of Jehoshaphat; And I will execute judgment on them there for my people, And for my heritage, Israel, whom they have scattered among the nations. They have divided my land,

Nao wamewapigia kura watu wangu; na mtoto mwanamume wamemtoa ili kupata kahaba, na mtoto mwanamke wamemwuza ili kupata divai, wapate kunywa. Yoeli 3:3

And have cast lots for my people, And have given a boy for a prostitute, And sold a girl for wine, that they may drink.

Naam, na ninyi ni kitu gani kwangu, enyi Tiro, na Sidoni, na nchi zote za Filisti? Je! Mtanirudishia malipo? Au mtanitenda neno lo lote? Upesi na kwa haraka nitawarudishia malipo yenu juu ya vichwa vyenu wenyewe. Yoeli 3:4

"Yes, and what are you to me, Tyre, and Sidon, And all the regions of Philistia? Will you repay me? And if you repay me, I will swiftly and speedily return your repayment on your own head.

Kwa kuwa mmetwaa fedha yangu na dhahabu yangu, nanyi mmevichukua vitu vyangu vyema vipendezavyo, na kuviingiza katika hekalu zenu; Yoeli 3:5

Because you have taken my silver and my gold, And have carried my finest treasures into your temples,

tena watoto wa Yuda na watoto wa Yerusalemu mmewauzia Wayunani, mpate kuwahamisha mbali na mipaka yao; Yoeli 3:6

And have sold the children of Judah and the children of Jerusalem to the sons of the Greeks, That you may remove them far from their border.

tazameni, nitawaamsha wapatoke mahali mlipowauza, nami nitawarudishia malipo yenu juu ya vichwa vyenu wenyewe. Yoeli 3:7

Behold, I will stir them up out of the place where you have sold them, And will return your repayment on your own head;

Na mimi nitawauza wana wenu na binti zenu, na kuwatia katika mikono ya wana wa Yuda, nao watawauzia watu wa Sheba, taifa lililo mbali kabisa; kwa maana Bwana ndiye aliyesema neno hili. Yoeli 3:8

And I will sell your sons and your daughters into the hands of the children of Judah, And they will sell them to the men of Sheba, To a faraway nation, For Yahweh has spoken it."

Tangazeni haya kati ya mataifa; takaseni vita; waamsheni mashujaa; watu wa vita na wakaribie; na wapande juu. Yoeli 3:9

Proclaim this among the nations: Prepare war. Stir up the mighty men. Let all the warriors draw near. Let them come up.

Yafueni majembe yenu yawe panga, na miundu yenu iwe mikuki; aliye dhaifu na aseme, Mimi ni hodari. Yoeli 3:10

Beat your plowshares into swords, And your pruning hooks into spears. Let the weak say, "I am strong."

Fanyeni haraka, mje, enyi mataifa yote, wa pande zote, jikusanyeni pamoja; na huko watelemshe mashujaa wako wote, Ee Bwana. Yoeli 3:11

Hurry and come, all you surrounding nations, And gather yourselves together." Cause your mighty ones to come down there, Yahweh.

Mataifa na wajihimize, wakapande juu katika bonde la Yehoshafau; maana huko ndiko nitakakoketi niwahukumu mataifa yote yaliyo pande zote. Yoeli 3:12

"Let the nations arouse themselves, And come up to the valley of Jehoshaphat; For there will I sit to judge all the surrounding nations.

Haya! Utieni mundu, maana mavuno yameiva; njoni, kanyageni; kwa maana shinikizo limejaa, mapipa nayo yanafurika; kwani uovu wao ni mwingi sana. Yoeli 3:13

Put in the sickle; For the harvest is ripe. Come, tread, for the winepress is full, The vats overflow, for their wickedness is great."

Makutano makubwa, makutano makubwa, wamo katika bonde la kukata maneno! Kwa maana siku ya Bwana i karibu, katika bonde la kukata maneno. Yoeli 3:14

Multitudes, multitudes in the valley of decision! For the day of Yahweh is near, in the valley of decision.

Jua na mwezi vimetiwa giza, na nyota zimeacha kuangaza. Yoeli 3:15

The sun and the moon are darkened, And the stars withdraw their shining."

Naye Bwana atanguruma toka Sayuni, atatoa sauti yake toka Yerusalemu; na mbingu na nchi zitatetemeka; lakini Bwana atakuwa kimbilio la watu wake, na ngome ya wana wa Israeli. Yoeli 3:16

Yahweh will roar from Zion, And thunder from Jerusalem; And the heavens and the earth will shake; But Yahweh will be a refuge to his people, And a stronghold to the children of Israel.

Hivyo ndivyo mtakavyojua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, nikaaye Sayuni, mlima wangu mtakatifu; ndipo Yerusalemu utakapokuwa mtakatifu, wala wageni hawatapita tena ndani yake kamwe. Yoeli 3:17

"So you will know that I am Yahweh, your God, Dwelling in Zion, my holy mountain. Then Jerusalem will be holy, And no strangers will pass through her any more.

Tena itakuwa siku ile, ya kwamba milima itadondoza divai tamu, na vilima vitatiririka maziwa, na vijito vyote vya Yuda vitatoa maji tele; na chemchemi itatokea katika nyumba ya Bwana, na kulinywesha bonde la Shitimu. Yoeli 3:18

It will happen in that day, That the mountains will drop down sweet wine, The hills will flow with milk, All the brooks of Judah will flow with waters; And a fountain will come forth from the house of Yahweh, And will water the valley of Shittim.

Misri itakuwa ukiwa, na Edomu itakuwa jangwa tupu, kwa sababu ya dhuluma waliowatenda wana wa Yuda; kwa sababu wamemwaga damu isiyo na hatia katika nchi yao. Yoeli 3:19

Egypt will be a desolation, And Edom will be a desolate wilderness, For the violence done to the children of Judah, Because they have shed innocent blood in their land.

Bali Yuda atadumu milele, na Yerusalemu tangu kizazi hata kizazi. Yoeli 3:20

But Judah will be inhabited forever, And Jerusalem from generation to generation.

Nami nitaitakasa damu yao ambayo sijaitakasa; kwa maana Bwana ndiye akaaye Sayuni. Yoeli 3:21

I will cleanse their blood, That I have not cleansed: For Yahweh dwells in Zion."