Habakuki 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
Habakuki 1 (Swahili) Habakkuk 1 (English)

Ufunuo aliouona nabii Habakuki. Habakuki 1:1

The oracle which Habakkuk the prophet saw.

Ee Bwana, nilie hata lini, wewe usitake kusikia? Nakulilia kwa sababu ya udhalimu, ila hutaki kuokoa. Habakuki 1:2

Yahweh, how long will I cry, and you will not hear? I cry out to you "Violence!" and will you not save?

Mbona wanionyesha uovu, na kunitazamisha ukaidi? Maana uharibifu na udhalimu u mbele yangu; kuna ugomvi, na mashindano yatokea. Habakuki 1:3

Why do you show me iniquity, and look at perversity? For destruction and violence are before me. There is strife, and contention rises up.

Kwa sababu hiyo sheria imelegea, wala hukumu haipatikani; kwa maana watu wabaya huwazunguka wenye haki; kwa sababu hiyo hukumu ikipatikana imepotoka. Habakuki 1:4

Therefore the law is paralyzed, and justice never goes forth; for the wicked surround the righteous; therefore justice goes forth perverted.

Angalieni, enyi mlio kati ya mataifa, katazameni, kastaajabuni sana; kwa maana mimi natenda tendo siku zenu, ambalo hamtaliamini hata mkiambiwa. Habakuki 1:5

"Look among the nations, watch, and wonder marvelously; for I am working a work in your days, which you will not believe though it is told you.

Kwa maana, angalieni, nawaondokesha Wakaldayo, taifa lile kali, lenye haraka kupita kiasi; wapitao katikati ya dunia, ili wayamiliki makao yasiyo yao. Habakuki 1:6

For, behold, I raise up the Chaldeans, that bitter and hasty nation, that march through the breadth of the earth, to possess dwelling places that are not theirs.

Hao ni watu wa kutisha sana, wa kuogofya sana; hukumu yao na ukuu wao hutoka katika nafsi zao wenyewe. Habakuki 1:7

They are feared and dreaded. Their judgment and their dignity proceed from themselves.

Farasi zao ni wepesi kuliko chui, ni wakali kuliko mbwa-mwitu wa jioni; na wapanda farasi wao hujitapa naam, wapanda farasi wao watoka mbali sana; huruka kama tai afanyaye haraka ale. Habakuki 1:8

Their horses also are swifter than leopards, and are more fierce than the evening wolves. Their horsemen press proudly on. Yes, their horsemen come from afar. They fly as an eagle that hurries to devour.

Waja wote ili kufanya udhalimu; nyuso zao zimeelekezwa kwa bidii yao kama upepo wa mashariki, nao hukusanya mateka kama mchanga. Habakuki 1:9

All of them come for violence. Their hordes face the desert. He gathers prisoners like sand.

Naam, huwadhihaki wafalme, na wakuu ni kitu cha kudharauliwa kwake; huidharau kila ngome; kwa maana hufanya chungu ya mavumbi, na kuitwaa. Habakuki 1:10

Yes, he scoffs at kings, and princes are a derision to him. He laughs at every stronghold, for he builds up an earthen ramp, and takes it.

Kisha atapita kwa kasi, kama upepo, atapita na kuwa ana hatia; yeye ambaye nguvu zake ni mungu wake. Habakuki 1:11

Then he sweeps by like the wind, and goes on. He is indeed guilty, whose strength is his god."

Ee Bwana, Mungu wangu, mtakatifu wangu, wewe si wa milele? Hatutakufa. Ee Bwana, umemwandikia hukumu, nawe, Ee Jabali, umemweka imara ili aadhibishwe. Habakuki 1:12

Aren't you from everlasting, Yahweh my God, my Holy One? We will not die. Yahweh, you have appointed him for judgment. You, Rock, have established him to punish.

Wewe uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu, wewe usiyeweza kutazama ukaidi, mbona unawaangalia watendao kwa hila; na kunyamaza kimya, hapo mtu mwovu ammezapo mtu aliye mwenye haki kuliko yeye; Habakuki 1:13

You who have purer eyes than to see evil, and who cannot look on perversity, why do you tolerate those who deal treacherously, and keep silent when the wicked swallows up the man who is more righteous than he,

na kufanya wanadamu kuwa kama samaki wa baharini, kama vitu vitambaavyo, ambavyo havina mtawala? Habakuki 1:14

and make men like the fish of the sea, like the creeping things, that have no ruler over them?

Yeye huwatoa wote kwa ndoana yake, huwakamata katika wavu wake, na kuwakusanya katika juya lake; ndiyo sababu afurahi na kupendezwa. Habakuki 1:15

He takes up all of them with the hook. He catches them in his net, and gathers them in his dragnet. Therefore he rejoices and is glad.

Kwa sababu hiyo huutolea wavu wake sadaka, na kulifukizia uvumba juya lake; kwa sababu kwa vitu vile fungu lake limenona, na chakula chake kimekuwa tele. Habakuki 1:16

Therefore he sacrifices to his net, and burns incense to his dragnet, because by them his life is luxurious, and his food is good.

Je! Atawatoa walio katika wavu wake, asiache kuwaua watu wa mataifa daima? Habakuki 1:17

Will he therefore continually empty his net, and kill the nations without mercy?