Angela Chibalonza - Msalaba ndio asili ya mema Lyrics

Msalaba ndio asili ya mema Lyrics

Sioni haya kwa Bwana,
Kwake nitang’ara!
Mti wake sitakana,
Ni neno imara.

(Chorus)
Msalaba ndio asili ya mema,
Nikatua mzigo hapo;
Nina uzima, furaha daima,
Njoni kafurahini papo.

Kama kiti chake vivyo,
Ni yake ahadi;
Alivyowekewa navyo,
Kamwe, havirudi.

Bwana wangu, tena Mungu,
Ndilo lake jina!
Hataacha roho yangu,
Wala kunikana.

Atakiri langu jina,
Mbele za Babaye,
Anipe pahali tena,
Mbinguni nikae

# At the Cross



Msalaba ndio asili ya mema Video

Msalaba ndio asili ya mema Lyrics -  Angela Chibalonza

Angela Chibalonza Songs

Related Songs