Ufunuo wa Yohana 9 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ufunuo wa Yohana 9 (Swahili) Revelation 9 (English)

Malaika wa tano akapiga baragumu, nikaona nyota iliyotoka mbinguni, imeanguka juu ya nchi; naye akapewa ufunguo wa shimo la kuzimu. Ufunuo wa Yohana 9:1

The fifth angel sounded, and I saw a star from the sky which had fallen to the earth. The key to the pit of the abyss was given to him.

Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuru kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni. Ufunuo wa Yohana 9:2

He opened the pit of the abyss, and smoke went up out of the pit, like the smoke from a{TR adds "great"} burning furnace. The sun and the air were darkened because of the smoke from the pit.

Nzige wakatoka katika ule moshi, wakaenda juu ya nchi, wakapewa nguvu kama nguvu waliyo nayo nge wa nchi. Ufunuo wa Yohana 9:3

Then out of the smoke came forth locusts on the earth, and power was given to them, as the scorpions of the earth have power.

Wakaambiwa wasiyadhuru majani ya nchi, wala kitu cho chote kilicho kibichi, wala mti wo wote, ila wale watu wasio na muhuri ya Mungu katika vipaji vya nyuso zao. Ufunuo wa Yohana 9:4

They were told that they should not hurt the grass of the earth, neither any green thing, neither any tree, but only those people who don't have God's seal on their foreheads.

Wakapewa amri kwamba wasiwaue, bali wateswe miezi mitano. Na maumivu yao yalikuwa kama kuumwa na nge, aumapo mwanadamu. Ufunuo wa Yohana 9:5

They were given power not to kill them, but to torment them for five months. Their torment was like the torment of a scorpion, when it strikes a person.

Na siku zile wanadamu watatafuta mauti, wala hawataiona kamwe. Nao watatamani kufa, nayo mauti itawakimbia. Ufunuo wa Yohana 9:6

In those days people will seek death, and will in no way find it. They will desire to die, and death will flee from them.

Na maumbo ya hao nzige yalikuwa kama farasi waliowekwa tayari kwa vita, na juu ya vichwa vyao kama taji, mfano wa dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama nyuso za wanadamu. Ufunuo wa Yohana 9:7

The shapes of the locusts were like horses prepared for war. On their heads were something like golden crowns, and their faces were like people's faces.

Nao walikuwa na nywele kama nywele za wanawake. Na meno yao yalikuwa kama meno ya simba. Ufunuo wa Yohana 9:8

They had hair like women's hair, and their teeth were like those of lions.

Nao walikuwa na dirii kifuani kama dirii za chuma. Na sauti ya mabawa yao ilikuwa kama sauti ya magari, ya farasi wengi waendao kasi vitani. Ufunuo wa Yohana 9:9

They had breastplates, like breastplates of iron. The sound of their wings was like the sound of chariots, or of many horses rushing to war.

Nao wana mikia kama ya nge, na miiba; na nguvu yao ya kuwadhuru wanadamu miezi mitano ilikuwa katika mikia yao. Ufunuo wa Yohana 9:10

They have tails like those of scorpions, and stings. In their tails they have power to harm men for five months.

Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani analo jina lake Apolioni. Ufunuo wa Yohana 9:11

They have over them as king the angel of the abyss. His name in Hebrew is "Abaddon,"{"Abaddon" is a Hebrew word that means ruin, destruction, or the place of destruction} but in Greek, he has the name "Apollyon."{"Apollyon" means "Destroyer."}

Ole wa kwanza umekwisha pita. Tazama, bado ziko ole mbili, zinakuja baadaye. Ufunuo wa Yohana 9:12

The first woe is past. Behold, there are still two woes coming after this.

Malaika wa sita akapiga baragumu, nikasikia sauti moja iliyotoka katika zile pembe za madhabahu ya dhahabu iliyo mbele za Mungu, Ufunuo wa Yohana 9:13

The sixth angel sounded. I heard a voice from the horns of the golden altar which is before God,

ikimwambia yule malaika wa sita aliyekuwa na baragumu, Wafungue nao malaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa Frati. Ufunuo wa Yohana 9:14

saying to the sixth angel who had one trumpet, "Free the four angels who are bound at the great river Euphrates!"

Wale malaika wanne wakafunguliwa, waliokuwa wamewekwa tayari kwa ile saa na siku na mwezi na mwaka, ili kwamba waue theluthi ya wanadamu. Ufunuo wa Yohana 9:15

The four angels were freed who had been prepared for that hour and day and month and year, so that they might kill one third of mankind.

Na hesabu ya majeshi ya wapanda farasi ilikuwa elfu ishirini mara elfu kumi; nilisikia hesabu yao. Ufunuo wa Yohana 9:16

The number of the armies of the horsemen was two hundred million{literally, "ten thousands of ten thousands"}. I heard the number of them.

Hiyo ndivyo nilivyowaona hao farasi katika maono yangu, nao waliokaa juu yao, wana dirii kifuani, kama za moto, na za samawi, na za kiberiti; na vichwa vya farasi hao ni kama vichwa vya simba, na katika vinywa vyao hutoka moto na moshi na kiberiti. Ufunuo wa Yohana 9:17

Thus I saw the horses in the vision, and those who sat on them, having breastplates of fiery red, hyacinth blue, and sulfur yellow; and the heads of lions. Out of their mouths proceed fire, smoke, and sulfur.

Theluthi ya wanadamu wakauawa kwa mapigo matatu hayo, kwa moto huo na moshi huo na kiberiti hicho, yaliyotoka katika vinywa vyao. Ufunuo wa Yohana 9:18

By these three plagues were one third of mankind killed: by the fire, the smoke, and the sulfur, which proceeded out of their mouths.

Kwa maana nguvu za hao farasi ni katika vinywa vyao, na katika mikia yao; maana mikia yao ni mfano wa nyoka, ina vichwa, nao wanadhuru kwa hivyo. Ufunuo wa Yohana 9:19

For the power of the horses is in their mouths, and in their tails. For their tails are like serpents, and have heads, and with them they harm.

Na wanadamu waliosalia, wasiouawa kwa mapigo hayo, hawakuzitubia zile kazi za mikono yao, hata wasiwasujudie mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za miti, zisizoweza kuona wala kusikia wala kuenenda. Ufunuo wa Yohana 9:20

The rest of mankind, who were not killed with these plagues, didn't repent of the works of their hands, that they wouldn't worship demons, and the idols of gold, and of silver, and of brass, and of stone, and of wood; which can neither see, nor hear, nor walk.

Wala hawakuutubia uuaji wao, wala uchawi wao, wala uasherati wao, wala wivi wao. Ufunuo wa Yohana 9:21

They didn't repent of their murders, nor of their sorceries,{The word for "sorceries" (pharmakeia) also implies the use of potions, poisons, and drugs} nor of their sexual immorality, nor of their thefts.