Ufunuo wa Yohana 15 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ufunuo wa Yohana 15 (Swahili) Revelation 15 (English)

Kisha nikaona ishara nyingine katika mbingu, iliyo kubwa, na ya ajabu; malaika saba wenye mapigo saba ya mwisho; maana katika hayo ghadhabu ya Mungu imetimia. Ufunuo wa Yohana 15:1

I saw another great and marvelous sign in the sky: seven angels having the seven last plagues, for in them God's wrath is finished.

Tena nikaona kitu kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto, na wale wenye kushinda, watokao kwa yule mnyama, na sanamu yake, na kwa hesabu ya jina lake, walikuwa wamesimama kando-kando ya hiyo bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu. Ufunuo wa Yohana 15:2

I saw something like a sea of glass mixed with fire, and those who overcame the beast, his image,{TR adds "his mark,"} and the number of his name, standing on the sea of glass, having harps of God.

Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa. Ufunuo wa Yohana 15:3

They sang the song of Moses, the servant of God, and the song of the Lamb, saying, "Great and marvelous are your works, Lord God, the Almighty; Righteous and true are your ways, you King of the nations.

Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele zako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa. Ufunuo wa Yohana 15:4

Who wouldn't fear you, Lord, And glorify your name? For you only are holy. For all the nations will come and worship before you. For your righteous acts have been revealed."

Na baada ya hayo nikaona, na hekalu la hema ya ushuhuda mbinguni lilifunguliwa; Ufunuo wa Yohana 15:5

After these things I looked, and the temple of the tabernacle of the testimony in heaven was opened.

na wale malaika saba, wenye mapigo saba, wakatoka katika hekalu, wamevikwa mavazi ya kitani safi, ya kung'aa, wamefungwa vifuani mwao mishipi ya dhahabu. Ufunuo wa Yohana 15:6

The seven angels who had the seven plagues came out, clothed with pure, bright linen, and wearing golden sashes around their breasts.

Na mmoja wa wale wenye uhai wanne akawapa wale malaika saba vitasa saba vya dhahabu, vimejaa ghadhabu ya Mungu, aliye hai hata milele na milele. Ufunuo wa Yohana 15:7

One of the four living creatures gave to the seven angels seven golden bowls full of the wrath of God, who lives forever and ever.

Hekalu likajazwa moshi uliotoka kwenye utukufu wa Mungu na uweza wake. Wala hapakuwa na mtu aliyeweza kuingia ndani ya hekalu, hata yatimizwe mapigo saba ya wale malaika saba. Ufunuo wa Yohana 15:8

The temple was filled with smoke from the glory of God, and from his power. No one was able to enter into the temple, until the seven plagues of the seven angels would be finished.