Mkono Wa Bwana - Tumeuona Mkono Wako Bwana

Mp3

Tumeuona mkono wake Bwana

Mengi mazuri tumeyaona, Mungu umetenda
Ni kweli we muweza
Ulitamka vitu vikawa
Neno tu latosha
Ukisema umetenda
Bahari shamu Isiraeli
Ah uliwavusha
Kawatoa utumwani
Watumishi wako umewapa
Yote waombayo
Ikiwa umependezwa

Uamulo hakuna wa kulipinga
Hakika we ni Mungu, wa vyote
Unatawala dunia na vilivyomo
Makuu umeyatenda, Jehova

Refrain:
Tumeuona, mkono wako Bwana
Matendo yako Bwana ni makuu mno
Umetutoa mbali, ukatushika mkono
Mahali uliona pekee hatuwezi
Chini hata juu, watu unawainua
Sifa na utukufu ni zako milele
Twasifu jina lako, milele tutakusifu
Daima we u mwema tutaishi kwako

Tumeuona, mkono wako Bwana
Matendo yako Bwana ni makuu mno
Umetutoa mbali, ukatushika mkono
Mahali uliona pekee hatuwezi
Chini hata juu, watu unawainua
Sifa na utukufu ni zako milele
Twasifu jina lako, milele tutakusifu
Daima we u mwema tutaishi kwako

Ona ona ona ona
Msalabani ulitufia, hm ulitupenda
Dhambi zetu ukabeba
Baraka zako tuliziomba kweli tumeona
Hakika unabariki
Hata vipaji we ndo hutoa umetuwezesha
Tunaimba na kusifu
Walio haki hutowaacha, uliwaahidi
Hata mwisho wa dahari

Hm watu wako umewapa mamlaka
kwa jina lako Yesu
Waponye
Na huna ubaguzi
Wote ni sawa kwako
Umetuita Yesu, tupone

(Refrain)

Ona ona ona
Daima we umwema tutaishi kwako
(Repeat)


Top Songs United States
Share:

Write a review/comment/correct the lyrics of Mkono Wa Bwana - Tumeuona Mkono Wako Bwana :

6 Comments/Reviews

 • Laiser Magrison

  ubarikiwe sana mtumishi 2 months ago

 • Hazel Elizabeth

  So amazing 3 months ago


  Replies:
  • Laiser Magrison

   Actually dear

 • Catherine

  Was my theme song during my wedding in May 31st, 2019 and I shall forever sing and dance along wherever I hear it in jubilation cause the message being sent forward touches on my life - AMEN. 7 months ago

 • Carolyne Wanjala

  a encouraging song
  8 months ago

 • Paul Juma

  Nyimbo yakutia moyo kweli kweli mbarikiwe sana 8 months ago

 • Madovena Mbawala

  Wimbo mzuri, unafariji sana! Mungu awabariki 9 months ago