Nyimbo za Kuabudu (Popular swahili worship songs)

Jina la Yesu ni ngome Yangu

Jina la Yesu ni ngome Yangu Jina la Yesu ni ngome Yangu
nitamkampo Jina Hilo, ngome lingine sina nitamkampo Jina Hilo, ngome lingine sina

Hakuna wa kufanana na Yesu

Hakuna wa kufanana na Yesu, hakuna wa kufanana Naye
Hakuna wa kufanana na Yesu, hakuna wa kufanana Naye
Yeye ni Bwana, Yeye ni Bwana
Yeye ni Bwana, Yeye ni Bwana
Hakuna wa kufanana na Yesu, hakuna wa kufanana Naye

Hakuna Mungu kama wewe

Hakuna Mungu kama wewe, hakuna popote
Hakuna mwenye ishara kubwa, kama wewe ewe Mungu
Si kwa majeshi, wala silaha ni kwa roho, mtakatifu
nguvu za giza zimeshindwa kwa jina la bwana Yesu
mapepo yote yameshindwa kwa jina la bwana Yesu

Natamani kufanana nawe

Natamani kufanana nawe, natamani kufanana nawe
Siku zote za maisha yangu
Natamani kushiriki nawe, natamani kushiriki nawe
Siku zote za maisha yangu

Ni wewe, niwewe Bwana

Ni wewe ni niwewe ni wewe Bwana

Sisi wana wako tumekusanyika angalia

Sisi wana wako tumekusanyika, angalia Jehova angalia Bwana
Sisi wana wako tumekusanyika, angalia Jehova angalia Bwana

Heri ni Jina La Yesu

Heri ni Jina, heri ni Jina Heri ni Jina, La Yesu Bwana

Nasema Asante Kwa Mungu wangu

Nasema Asante Kwa Mungu wangu
Nasema Asante Kwa wema wako
Kwa maana fadhili zako zidumu
milele na milele amina

Full Swahili Worship Songs Lyrics


From the Bible

Hakuna kama wewe Katika Biblia

Zaburi 86: 8

Katikati ya miungu hakuna kama Wewe, Bwana, Wala matendo mfano wa matendo yako.

2 Samweli 7: 22

Kwa hiyo, wewe ndiwe mkuu, Ee Bwana Mungu, kwa maana hakuna kama wewe, wala hapana Mungu mwingine ila wewe, kwa kadiri tulivyosikia kwa masikio yetu.

Abudu Mungu Katika Biblia

Waebrania 9: 14

basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?

Ufunuo wa Yohana 19: 4

Na wale wazee ishirini na wanne, na wale wenye uhai wanne, wakasujudu na kumwabudu Mungu, aketiye katika kile kiti cha enzi, wakisema, Amina, Haleluya.

Matendo ya Mitume 24: 14

Ila neno hili naungama kwako ya kwamba kwa Njia ile ambayo waiita uzushi, ndivyo ninavyomwabudu Mungu wa baba zetu, nikiyaamini yote yanayopatana na torati na yaliyoandikwa katika vyuo vya manabii.

Matendo ya Mitume 18: 13

wakisema Mtu huyu huwavuta watu ili wamwabudu Mungu kinyume cha sheria.

Matendo ya Mitume 26: 7

ambayo kabila zetu kumi na mbili wanataraji kuifikia, wakimwabudu Mungu kwa bidii mchana na usiku. Nami ninashitakiwa na Wayahudi kwa ajili ya tumaini hilo, Ee Mfalme.

Kutoka 3: 12

Akasema, Bila shaka mimi nitakuwa pamoja nawe; na dalili ya kuwa nimekutuma ndiyo hii; utakapokuwa umekwisha kuwatoa hao watu katika Misri, mtamwabudu Mungu katika mlima huu.

Kutoka 34: 14

Maana hutamwabudu mungu mwingine, kwa kuwa Bwana, ambaye jina lake ni mwenye wivu, ni Mungu mwenye wivu.

1 Wakorintho 14: 25

siri za moyo wake huwa wazi; na hivyo atamwabudu Mungu, akianguka kifudifudi, na kukiri ya kuwa Mungu yu kati yenu bila shaka.

omba Katika Biblia

Zaburi 88: 2

Maombi yangu yafike mbele zako, Uutegee ukelele wangu sikio lako.

Zaburi 88: 13

Lakini mimi nimekulilia Wewe, Bwana, Na asubuhi maombi yangu yatakuwasilia.

Zaburi 42: 8

Mchana Bwana ataagiza fadhili zake, na usiku wimbo wake utakuwa nami, Naam, maombi kwa Mungu aliye uhai wangu.

Zaburi 61: 1

Ee Mungu, ukisikie kilio changu, Uyasikilize maombi yangu.

Zaburi 17: 1

Ee Bwana, usikie haki, ukisikilize kilio changu, Utege sikio lako kwa maombi yangu, Yasiyotoka katika midomo ya hila.

Zaburi 66: 19

Hakika Mungu amesikia; Ameisikiliza sauti ya maombi yangu.

Zaburi 66: 20

Na ahimidiwe Mungu asiyeyakataa maombi yangu, Wala kuniondolea fadhili zake.

Zaburi 35: 13

Bali mimi, walipougua wao, Nguo yangu ilikuwa gunia. Nalijitesa nafsi yangu kwa kufunga; Maombi yangu yakarejea kifuani mwangu.

Zaburi 80: 4

Ee Bwana, Mungu wa majeshi, hata lini Utayaghadhibikia maombi ya watu wako?

Zaburi 69: 13

Nami maombi yangu nakuomba Wewe, Bwana, Wakati ukupendezao; Ee Mungu, Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Katika kweli ya wokovu wako.

Zaburi 54: 2

Ee Mungu, uyasikie maombi yangu, Uyasikilize maneno ya kinywa changu.

Zaburi 84: 8

Bwana, Mungu wa majeshi, uyasikie maombi yangu, Ee Mungu wa Yakobo, usikilize,

Zaburi 6: 9

Bwana ameisikia dua yangu; Bwana atayatakabali maombi yangu.

Zaburi 72: 20

Maombi ya Daudi mwana wa Yese yamekwisha.

Zaburi 102: 17

Atakapoyaelekea maombi yake aliye mkiwa, Asiyadharau maombi yao.

Zaburi 86: 6

Ee Bwana, uyasikie maombi yangu; Uisikilize sauti ya dua zangu.

Zaburi 39: 12

Ee Bwana, usikie maombi yangu, Utege sikio lako niliapo, Usiyanyamalie machozi yangu. Kwa maana mimi ni mgeni wako, Msafiri kama baba zangu wote.

Yona 2: 7

Roho yangu ilipozimia ndani yangu, Nalimkumbuka Bwana; Maombi yangu yakakuwasilia, Katika hekalu lako takatifu.

Yeremia 3: 21

Sauti inasikiwa juu ya vilele vya milima, ni kulia kwao na maombi yao wana wa Israeli; kwa kuwa wameipotosha njia yao, wamemsahau Bwana, Mungu wao.

Yeremia 37: 20

Na sasa unisikilize, Ee bwana wangu mfalme; maombi yangu yakapate kibali mbele yako; usinirudishe nyumbani mwa Yonathani, mwandishi, nisije nikafa humo.

Yeremia 31: 9

Watakuja kwa kulia, na kwa maombi nitawaongoza; nitawaendesha penye mito ya maji, katika njia iliyonyoka; katika njia hiyo hawatajikwaa; maana mimi ni baba wa Israeli, na Efraimu ni mzaliwa wa kwanza wangu.

Yeremia 42: 2

wakamwambia Yeremia, nabii, Twakusihi, maombi yetu yakubaliwe mbele yako, ukatuombee kwa Bwana, Mungu wako, yaani, watu hawa wote waliosalia; maana tumesalia wachache tu katika watu wengi, kama macho yako yatuonavyo;

Yeremia 42: 9

akawaambia, Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye mlinituma kwake, ili niyaweke maombi yenu mbele yake, asema hivi;

Warumi 15: 30

Ndugu zangu, nawasihi kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa upendo wa Roho, jitahidini pamoja nami katika maombi yenu kwa ajili yangu mbele za Mungu;

Wakolosai 1: 9

Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni;

Wakolosai 4: 12

Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu katika maombi yake, ili kwamba msimame wakamilifu na kuthibitika sana katika mapenzi yote ya Mungu.

Waefeso 6: 18

kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;

Waebrania 5: 7

Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;

Ufunuo wa Yohana 5: 8

Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.

Ufunuo wa Yohana 8: 3

Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi.

Ufunuo wa Yohana 8: 4

Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu pamoja na maombi ya watakatifu, kutoka mkononi mwa malaika.

Nehemia 1: 6

tega sikio lako, macho yako yakafumbuke, upate kuyasikiliza maombi ya mtumishi wako, ninayoomba mbele zako wakati huu, mchana na usiku, kwa ajili ya wana wa Israeli, watumishi wako; hapo ninapoziungama dhambi za wana wa Israeli, tulizozifanya juu yako; naam, mimi na nyumba ya baba yangu tumefanya dhambi.

Nehemia 1: 11

Ee Bwana, nakusihi, litege sikio lako, uyasikilize maombi ya mtumishi wako, na maombi ya watumishi wako, wanaofurahi kulicha jina lako; nakuomba sana; unifanikishe mimi, mtumishi wako, leo, ukanijalie rehema mbele ya mtu huyu. (Maana, nalikuwa mnyweshaji wa mfalme).

Mithali 18: 23

Maskini hutumia maombi; Bali tajiri hujibu kwa ukali.

Mithali 15: 8

Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa Bwana; Bali maombi ya mtu mnyofu ni furaha yake.

Maombolezo 3: 8

Naam, nikilia na kuomba msaada, Huyapinga maombi yangu.

Maombolezo 3: 44

Umejifunika nafsi yako kwa wingu, Maombi yetu yasipite.

Isaya 19: 22

Naye Bwana atapiga Misri, akipiga na kuponya; nao wakirudi kwa Bwana, atakubali maombi yao na kuwaponya.

Isaya 1: 15

Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengi, sitasikia; mikono yenu imejaa damu.

Isaya 38: 5

Enenda ukamwambie Hezekia, Bwana, Mungu wa Daudi, baba yako, asema hivi, Mimi nimeyasikia maombi yako, nimeyaona machozi yako; tazama, nitaziongeza siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano.

Isaya 26: 16

Bwana, katika taabu zao walikwenda kwako; waliomba maombi mengi wakati adhabu yako ilipokuwa juu yao.

Filemoni 1: 4

Namshukuru Mungu wangu sikuzote, nikikukumbuka katika maombi yangu;

Filemoni 1: 22

Na pamoja na hayo uniwekee tayari mahali pa kukaa; maana nataraji ya kwamba kwa maombi yenu mtajaliwa kunipata.

Danieli 9: 3

Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu.

Danieli 9: 17

Basi sasa, Ee Mungu wetu, yasikilize maombi ya mtumishi wako, na dua zake, ukaangazishe uso wako juu ya patakatifu pako palipo ukiwa, kwa ajili ya Bwana.

Danieli 9: 18

Ee Mungu wangu, tega sikio lako, ukasikie; fumbua macho yako ukautazame ukiwa wetu, na mji ule ulioitwa kwa jina lako; maana hatukutolei maombi yetu kwa sababu ya haki yetu, lakini kwa sababu ya rehema zako nyingi.

Danieli 9: 23

Mwanzo wa maombi yako ilitolewa amri, nami nimekuja kukupasha habari; maana wewe unapendwa sana; basi itafakari habari hii, na kuyafahamu maono haya.

2 Wafalme 20: 5

Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, Bwana, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama, nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa Bwana.

2 Mambo ya Nyakati 33: 13

Akamwomba; naye akamtakabali, akayasikia maombi yake; akamrudisha tena Yerusalemu katika ufalme wake. Ndipo Manase akajua ya kwamba Bwana ndiye Mungu.

2 Mambo ya Nyakati 33: 18

Basi mambo yote ya Manase yaliyosalia, na maombi yake kwa Mungu wake, na maneno ya waonaji walionena naye kwa jina la Bwana, Mungu wa Israeli, tazama, yameandikwa kati ya mambo ya wafalme wa Israeli.

2 Mambo ya Nyakati 6: 19

Walakini umwangalie mtumwa wako anayoyaomba, na kusihi, Ee Bwana, Mungu wangu, usikie kilio na maombi anayoyaomba mtumwa wako mbele zako;

2 Mambo ya Nyakati 6: 20

ili macho yako yafumbuke kwa nyumba hii mchana na usiku, mahali uliponena, ndipo utakapoliweka jina lako; usikie maombi atakayoomba mtumwa wako, akikabili mahali hapa.

2 Mambo ya Nyakati 6: 40

Na sasa, Ee Mungu wangu, macho yako yafumbuke, nakusihi, masikio yako yakasikilize maombi yaombwayo mahali hapa.

2 Mambo ya Nyakati 7: 1

Basi Sulemani alipokwisha maombi hayo, moto ukashuka kutoka mbinguni, ukateketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu; utukufu wa Bwana ukaijaza nyumba.

2 Mambo ya Nyakati 7: 15

Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa.

1 Wathesalonike 1: 2

Twamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu nyote, tukiwataja katika maombi yetu.

1 Wafalme 8: 28

Walakini uyaelekee maombi ya mtumwa wako, na dua yake, Ee Bwana, Mungu wangu, uisikilize sauti na maombi ya mtumwa wako, aombayo mbele zako leo.

1 Wafalme 8: 29

Macho yako yafumbuke na kuielekea nyumba hii usiku na mchana, mahali hapa ulipopataja, ukasema, Hapa ndipo litakapokuwapo jina langu; ili uyasikie maombi ya mtumwa wako aombapo akikabili mahali hapa.

1 Wafalme 8: 38

maombi yo yote au dua yo yote ikifanywa na mtu awaye yote, au na watu wako Israeli wote pamoja, watakaojua kila mtu maradhi ya moyo wake, na kuikunjua mikono yake kuielekea nyumba hii;

1 Wafalme 8: 45

basi, uyasikie huko mbinguni maombi yao na dua yao, ukaitetee haki yao.

1 Wafalme 8: 49

basi, uyasikie maombi yao na dua yao, huko mbinguni, makao yako, ukaitetee haki yao;

1 Wafalme 8: 54

Hata ikawa, Sulemani alipokwisha kumwomba Bwana maombi hayo, na dua hiyo yote, akasimama na kuondoka hapo mbele ya madhabahu ya Bwana, hapo alipokuwa amepiga magoti, na kuikunjua mikono yake kuelekea mbinguni.

1 Wafalme 9: 3

Bwana akamwambia, Nimeyasikia maombi yako na dua zako, ulizotoa mbele zangu. Nimeitakasa nyumba hii uliyoijenga ili niweke jina langu humo milele; tena macho yangu na moyo wangu utakuwapo hapo siku zote;

1 Timotheo 5: 5

Basi yeye aliye mjane kweli kweli, ameachwa peke yake, huyo amemwekea Mungu tumaini lake, naye hudumu katika maombi na sala mchana na usiku.

1 Petro 3: 12

Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya.

1 Mambo ya Nyakati 5: 20

Wakapata msaada juu yao, nao Wahajiri walitiwa mikononi mwao, na wote waliokuwa pamoja nao; kwa kuwa walimlingana Mungu pale vitani; naye akayatakabali maombi yao, kwa sababu walimtumaini yeye.

Nguvu ya Mungu katika Biblia

2 Wakorintho 6: 7

katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto;

2 Timotheo 1: 8

Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wala usinionee haya mimi mfungwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu;

1 Wakorintho 1: 18

Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.

1 Wakorintho 1: 24

bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu.