Mfalme wa Amani Song Lyrics

Solomon Mukubwa Sifa Music

Information for Artists

Watch Video for Mfalme wa Amani

Read lyrics

Daudi kasema, nilikuwa kijana sasa ni mzee
Daudi kasema, nilikuwa kijana sasa ni mzee
Sijawahi ona mwenye haki ameachwa mimi
Wala watoto wake kuombaomba mikate barabarani

Mungu ni mwaminifu, kwa ahadi zake wanadamu
Mungu ni mwaminifu, kwa ahadi zake si kama wanadamu
Akiongea Yesu ameongea,
Akikuahidia kitu, Baba ameahidi na ujasiri aah
Atatenda kwa wakati wake yoyoo
Ninamwita Bwana wa amani yeyeyee
Ninamwita mfalme wa amani bwaanaa
Ndio maana mimi ninaimba kwa sababu ya amani yake
Ni uwezo gani, uwezo gani unaompinga Yesu
Uwezo gani, uwezo gani, uwezo gani
Mfalme wa amani, mfalme wa amani uinuliwe
Wewe ni mwema, wewe ni mwema Bwana wangu

Usilie, usilie, usiliwe wewe
Usilie Bwana anakujua ndugu yangu
Amesikia kilio chako wewe mama
Unalia nini kwa wanadamu, mama yangu
Wanadamu hawatakusaidia na kitu
Wanadamu hawatakuwezesha kwa kitu chochote
Tunaye mmoja anayepanguza machozi ya watu wake
Ni yule mfalme wa amani
Ni yule aliyesema yote imekwisha
Mama unayoyapitia ni yeye anayeyaona
anajua shida yako mama yangu
Anajua magumu yako baba yangu
Ukiwa na shida usiende kwa waganga wa dunia
Ukiwa na magumu usiende kwa wafumu wa dunia

Muite mfalme wa amani, yeye anajibu maombi
Ni uwezo gani, uwezo gani unaompinga Baba
Uwezo gani, uwezo gani, uwezo gani

Mfalme wa amani, uinuliwe Bwana wangu
Yale unayotenda inashangaza dunia nzima
Wanaokosa amani ndani ya nyumba zao wape amani
Wanaokosa amani ndani ya kazi zao wape amani
Ni wewe Bwana wa amani ya kudumu
Ni wewe Bwana wa amani ya Afrika
Amerika wanalia amani
Tunawe Bwana mfalme wa amani
Hakuna kitu kile kinachokushinda Bwana

Yeye Mfalme wa Amani uinuliwe
Wewe ni mwema, wewe ni mwema Bwana wangu

Tags: King, Peace, Mfalme, Amani, Sifa Lyrics

Other songs by Solomon Mukubwa,

Mungu wetu Mwenye Nguvu Baba wa milele
Futa Machozi

Related songs:

Swahili worship Songs - Nyimbo za kuabudu lyrics related to Mfalme wa Amani

Naijulikane
Ainuliwe Yesu
Ametenda Maajabu
Uniongoze - Baraka zako ziwe na mimi Bila nguvu zako
Ebenezer Nani Kama Wewe

From the Bible

Mfalme wa Amani Katika Biblia

Waebrania 7: 2

ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;

Isaya 9: 6

Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.

Categories