Msaidizi Song Lyrics

Gloria Muliro Sifa Music

Information for Artists

Watch Video for Msaidizi

Read lyrics

Tuma Baba tuma msaidizi
Tuma Yesu, tuma msaidizi

Yesu uliahidi wanafunzi wako
Kwamba hautawaacha kama yatima
Bali utawatumia msaidizi
Awafunze, awape nguvu
Awafariji mioyo
Nami naja mbele zako
Baba niko mbele zako
Naomba unitumie msaidizi
Anifunze, anipe nguvu
Aniongoze kwa kazi yako
Baba tuma msaidizi

Refrain:
Tuma msaidizi

Naomba Baba, nisaidie
Nataka nguvu mpya

Kila usiku ninapoenda kulala
Nafungua bila mpango ukurasa wowote
Ninasoma mistari michache tu naanza sinzia
Nafunga Biblia naanza kuomba
Kinachofuata naamka asubuhi kusema amina
Baba nisaidie,
Tuma nguvu zako, Tuma uwezo wako
Tuma roho wako ndani yangu Baba

Naomba, Nataka nguvu

Baba mimi siwezi chochote bila wewe
Naomba nguvu zako Baba

Baba tuma, Nakuomba Baba,
Tuma roho wako ndani yangu
Anifunze, aniongoze, anitawale
Mienenendo yangu aitawale
Maombi yangu, kufunga kwangu aitawale
Naomba tuma Baba
Roho wako anifunze neno, aombe, aimbe ndani yangu

Lord send me your holy spirit to me,
to teach, guide, reign,
in my character, prayer and fasting
Lord send your spirit
to teach me your word, to pray, to sing in me.

@Gloria Muliro - Msaidizi

Tags: Faith, Msaidizi, Sifa Lyrics

Other songs by Gloria Muliro,

Nahitaji Ndio Yako Yesu Tu
Narudisha
Mpango wa Kando

Related songs:

Nyimbo za sifa - Swahili Praise Songs lyrics related to Msaidizi

Wastahili Bwana
napenda nione
Just A Way To Show How Much I Love You - Njia Ya Kusema
Ameni Amen Haleluya
Bwana ni Mchungaji Wangu

From the Bible

Msaidizi Katika Biblia

Zaburi 10: 14

Umeona, maana unaangalia madhara na jeuri, Uyatwae mkononi mwako. Mtu duni hukuachia nafsi yake, Maana umekuwa msaidizi wa yatima.

Zaburi 30: 10

Ee Bwana, usikie, unirehemu, Bwana, uwe msaidizi wangu.

Zaburi 118: 7

Bwana yuko upande wangu, msaidizi wangu, Kwa hiyo nitawaona wanaonichukia wameshindwa.

Zaburi 107: 12

Hata akawadhili moyo kwa taabu, Wakajikwaa wala hakuna msaidizi.

Zaburi 22: 11

Usiwe mbali nami maana taabu i karibu, Kwa maana hakuna msaidizi.

Zaburi 72: 12

Kwa maana atamkomboa mhitaji aliapo, Na mtu aliyeonewa iwapo hana msaidizi.

Yohana 14: 16

Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;

Yohana 14: 26

Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

Yohana 15: 26

Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia.

Yohana 16: 7

Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu.

Categories