Patakatifu pako Song Lyrics

Eric Smith Sifa Music

Information for Artists

Watch Video for Patakatifu pako

Read lyrics

Patakatifu pako, hapo ndipo nahitaji
Mahali Baba, juu ya yote
Katika mikono yako mimi najiweka,
nizungukwe mimi na uwepo wako

Niambie utakalo Bwana
Nipe nguvu ya kushinda majaribu Yesu
Nakuhitaji Bwana maishani mwangu
Niambie utakalo Bwana
Nipe nguvu ya kushinda majaribu Yesu
Nakuhitaji Bwana maishani mwangu

Nachohitaji nikufurahisha roho yako
Wewe rafiki mwema uliyenipenda.
Kwa ajili yako Yesu sisi tumekombolewa
Kuwa na wewe Yesu yashinda yote (rudia)

Niambie utakalo Bwana
Nipe nguvu ya kushinda majaribu Yesu
Nakuhitaji Bwana maishani mwangu

Nahitaji mkono wako niongozwe na wewe Bwana
Kimbilio msaada wa karibu, ni wewe.
Nahitaji mkono wako niongozwe na wewe Bwana
Kimbilio msaada wa karibu, niwe, niwe, niwewe.
Nahitaji mkono wako niongozwe na wewe Bwana
Kimbilio msaada wa karibu, uinuliwe.

Niambie utakalo Bwana
Nipe nguvu ya kushinda majaribu Yesu
Nakuhitaji Bwana maishani mwangu

Tags: Patakatifu, Niambie utakalo, Sifa Lyrics

Other songs by Eric Smith,

Wewe ni zaidi - Yale umetenda Baba
Si ya Kawaida
Merciful God

Related songs:

Swahili worship Songs - Nyimbo za kuabudu lyrics related to Patakatifu pako

Tunainua Mikono yetu wewe Watosha
Nikufahamu Zaidi Bwana
Wanishangaza
Juu Yako Bwana Naishi
Ahadi Zake

From the Bible

Patakatifu pako Katika Biblia

Zaburi 74: 7

Wamepatia moto patakatifu pako; Wamelinajisi kao la jina lako hata chini.

Zaburi 28: 2

Uisikie sauti ya dua yangu nikuombapo, Nikipainulia patakatifu pako mikono yangu.

Zaburi 68: 35

Mungu ni mwenye kutisha Kutoka patakatifu pako. Ndiye Mungu wa Israeli; Yeye huwapa watu wake nguvu na uwezo. Na ahimidiwe Mungu.

Isaya 63: 18

Watu wako watakatifu waliumiliki kwa kitambo tu; adui zetu wamepakanyaga patakatifu pako.

Danieli 9: 17

Basi sasa, Ee Mungu wetu, yasikilize maombi ya mtumishi wako, na dua zake, ukaangazishe uso wako juu ya patakatifu pako palipo ukiwa, kwa ajili ya Bwana.

Categories