Mtegemee Yesu Song Lyrics

Christ Ambassadors Sifa Music

Information for Artists

Watch Video for Mtegemee Yesu

Read lyrics

Mambo mengi yakupata ndugu yanayokuumiza moyo
hata ukimwomba Mungu waona
kama vile amekutenga
Maisha magumu shida tupu
wapepeshwa dunia nzima
unapapasa hapa na pale
bila kupata msaada

umeanza kukata tamaa, imani yako inayumbayumba
unajisikia upweke, umeachwa kama yatima
utokako ni mbali sana, kiasi kwamba huwezi rudi
mbele huenda kunako giza, umekosa matumaini;

magumu shida yakupatayo ndugu, ni ya muda kidogo
kamwe yasikutenganishe na yule, rafiki wa kweli
hebu itegemee ahadi yake, kwamba atakuwa nawe
hata kwenye wakati huo mgumu, mtegemee Yesu

Umesongwa nazo shida nyingi, lakini mkumbuke Ayubu
alivyozidiwa nayo majaribu, akasimama imara
japo yako imefanywa wimbo, nao waumini wenzako
sawa na wale marafiki za, Ayubu walivyomcheka
Usiiruhusu shida yako, kukunyakua mkononi mwa bwana
jibu lako ni yeye pekee, tegemeo na kimbilio
hata wenzako wakutenge, vumilia utayashinda ndugu
jipe moyo mtetezi yupo, magumu atarahisisha;

Magumu shida yakupatayo ndugu, ni ya muda kidogo
kamwe yasikutenganishe na yule, rafiki wa kweli
hebu itegemee ahadi yake, kwamba atakuwa nawe
hata kwenye wakati huo mgumu, mtegemee Yesu

Umeanza kukata tamaa, imani yako inayumbayumba
unajisikia upweke, umeachwa kama yatima
utokako ni mbali sana, kiasi kwamba huwezi rudi
mbele huenda kunako giza, umekosa matumaini
usiiruhusu shida yako, kukunyakua mkononi mwa bwana
jibu lako ni yeye pekee, tegemeo na kimbilio
hata wenzako wakutenge, vumilia utayashinda ndugu
jipe moyo mtetezi yupo, magumu atarahisisha

Magumu shida yakupatayo ndugu, ni ya muda kidogo
kamwe yasikutenganishe na yule, rafiki wa kweli
hebu itegemee ahadi yake, kwamba atakuwa nawe
hata kwenye wakati huo mgumu, mtegemee Yesu

Tags: Rwanda, Yesu, Ahadi, Mtegemee, Magumu, Sifa Lyrics

Other songs by Christ Ambassadors,

Kwetu Pazuri nimeshapakumbuka
Nimekupata Yesu -natamani nitembee
Moyoni Mwangu

Related songs:

Nyimbo za sifa - Swahili Praise Songs lyrics related to Mtegemee Yesu

Lihimidi Jina Lake
Sipati Picha - Natamani mbingu mpya nchi mpya
Ahadi za Bwana Yesu zitatimia
Sambaza gospel injili ya yesu iende isonge mbele
Kutoka Kwa Moyo Wangu

From the Bible

Categories