Anajibu Maombi

Brenda B SifaMusic

Watch Video for Anajibu Maombi

Read lyrics while watching

Anajibu Maombi , anajibu maombi
Anajibu maombi yeye ni Mungu wa Miungu

Kama Paulo na Sila walivyofungwa gerezani
Waliomba na kusifu na akajibu maombi yao
Na yule lazaro alipokufa walikimbia kumwita Yesu
Yesu akawaambia amelala akamfufua lazaro

Anajibu Maombi, anajibu maombi
Anajibu maombi yeye ni Mungu wa miungu
Anajibu Maombi, anajibu maombi
Anajibu maombi yeye ni Mungu wa miungu

Kumbuka vile Sarah alivyoomba kwa miaka nyingi
Mungu akajibu hilo ombi lake, akambariki na Isaka
Na ile safari ya waisraeli, ilipotatizwa na wamisri
Mungu aliwapasulia bahari na akajibu maombi yao

Anajibu Maombi, anajibu maombi
Anajibu maombi yeye ni Mungu wa miungu
Anajibu Maombi, anajibu maombi
Anajibu maombi yeye ni Mungu wa miungu

Walipomletea Yule kipofu, Yesu alimuekelea mkono
Hapo upofu wake ukaisha, akamshukuru Mungu
Je wamkumbuka yule mwanamke alivyomwaga damu kwa miaka nyingi
Aligusa vazi la Yesu na akajibu ombi lake

Anajibu Maombi, anajibu maombi
Anajibu maombi yeye ni Mungu wa miungu
Anajibu Maombi, anajibu maombi
Anajibu maombi yeye ni Mungu wa miungu

Tags: Mungu, Maombi, Anajibu, Sifa Lyrics

Other songs by Brenda B,

Related songs:

Nyimbo za sifa - Swahili Praise Songs lyrics related to Anajibu Maombi

Tulia na ujue mimi ni Mungu wako
Ukiwa na Maono ya Mungu - Maono Yako
Anajibu Maombi
Afrika yote yakusifu (Africa Praises God)
Usiyeshindwa - mataifa yote yanakufahamu

From the Bible

Categories