Wafilipi 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Wafilipi 2 (Swahili) Philippians 2 (English)

Basi ikiwako faraja yo yote katika Kristo, yakiwako matulizo yo yote ya mapenzi, ukiwako ushirika wo wote wa Roho, ikiwako huruma yo yote na rehema, Wafilipi 2:1

If there is therefore any exhortation in Christ, if any consolation of love, if any fellowship of the Spirit, if any tender mercies and compassion,

ijalizeni furaha yangu, ili mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkinia mamoja. Wafilipi 2:2

make my joy full, by being like-minded, having the same love, being of one accord, of one mind;

Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Wafilipi 2:3

doing nothing through rivalry or through conceit, but in humility, each counting others better than himself;

Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. Wafilipi 2:4

each of you not just looking to his own things, but each of you also to the things of others.

Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; Wafilipi 2:5

Have this in your mind, which was also in Christ Jesus,

ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; Wafilipi 2:6

who, existing in the form of God, didn't consider it robbery to be equal with God,

bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; Wafilipi 2:7

but emptied himself, taking the form of a servant, being made in the likeness of men.

tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Wafilipi 2:8

And being found in human form, he humbled himself, becoming obedient to death, yes, the death of the cross.

Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; Wafilipi 2:9

Therefore God also highly exalted him, and gave to him the name which is above every name;

ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; Wafilipi 2:10

that at the name of Jesus every knee should bow, of those in heaven, those on earth, and those under the earth,

na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba. Wafilipi 2:11

and that every tongue should confess that Jesus Christ is Lord, to the glory of God the Father.

Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. Wafilipi 2:12

So then, my beloved, even as you have always obeyed, not only in my presence, but now much more in my absence, work out your own salvation with fear and trembling.

Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema. Wafilipi 2:13

For it is God who works in you both to will and to work, for his good pleasure.

Yatendeni mambo yote pasipo manung'uniko wala mashindano, Wafilipi 2:14

Do all things without murmurings and disputes,

mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu, Wafilipi 2:15

that you may become blameless and harmless, children of God without blemish in the midst of a crooked and perverse generation, among whom you are seen as lights in the world,

mkishika neno la uzima; nipate sababu ya kuona fahari katika siku ya Kristo, ya kuwa sikupiga mbio bure wala sikujitaabisha bure. Wafilipi 2:16

holding up the word of life; that I may have something to boast in the day of Christ, that I didn't run in vain nor labor in vain.

Naam, hata nikimiminwa juu ya dhabihu na ibada ya imani yenu, nafurahi; tena nafurahi pamoja nanyi nyote. Wafilipi 2:17

Yes, and if I am poured out on the sacrifice and service of your faith, I rejoice, and rejoice with you all.

Nanyi vivyo hivyo furahini, tena furahini pamoja nami. Wafilipi 2:18

In the same way, you also rejoice, and rejoice with me.

Walakini natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo afike kwenu karibu, nifarijiwe na mimi, nikiijua hali yenu. Wafilipi 2:19

But I hope in the Lord Jesus to send Timothy to you soon, that I also may be cheered up when I know how you are doing.

Maana sina mtu mwingine mwenye nia moja nami, atakayeiangalia hali yenu kweli kweli. Wafilipi 2:20

For I have no one else like-minded, who will truly care about you.

Maana wote wanatafuta vyao wenyewe, sivyo vya Kristo Yesu. Wafilipi 2:21

For they all seek their own, not the things of Jesus Christ.

Ila mwajua sifa yake, ya kuwa ametumika pamoja nami kwa ajili ya Injili, kama mwana na baba yake. Wafilipi 2:22

But you know the proof of him, that, as a child serves a father, so he served with me in furtherance of the Gospel.

Basi, natumaini kumtuma huyo mara, hapo nitakapojua yatakayonipata. Wafilipi 2:23

Therefore I hope to send him at once, as soon as I see how it will go with me.

Nami naamini katika Bwana ya kuwa nitakuja na mimi mwenyewe hivi karibu. Wafilipi 2:24

But I trust in the Lord that I myself also will come shortly.

Lakini naliona imenilazimu kumtuma kwenu Epafrodito, ndugu yangu, mtenda kazi pamoja nami, askari pamoja nami; tena ni mtume wenu na mhudumu wa mahitaji yangu. Wafilipi 2:25

But I counted it necessary to send to you Epaphroditus, my brother, fellow worker, fellow soldier, and your apostle and minister to my need;

Kwa kuwa alikuwa na shauku kwenu ninyi nyote, akahuzunika sana, kwa sababu mlisikia ya kwamba alikuwa hawezi. Wafilipi 2:26

since he longed for you all, and was very troubled, because you had heard that he was sick.

Kwa maana alikuwa hawezi kweli kweli, karibu na kufa; lakini Mungu alimhurumia; wala si yeye peke yake, ila na mimi pia; nisiwe na huzuni juu ya huzuni. Wafilipi 2:27

For indeed he was sick, nearly to death, but God had mercy on him; and not on him only, but on me also, that I might not have sorrow on sorrow.

Kwa hiyo nimefanya bidii nyingi zaidi kumtuma, ili mtakapomwona tena mpate kufurahi, nami nipunguziwe huzuni yangu. Wafilipi 2:28

I have sent him therefore the more diligently, that, when you see him again, you may rejoice, and that I may be the less sorrowful.

Mpokeeni, basi, katika Bwana, kwa furaha yote, mkawahesabu watu kama huyu kuwa watu wa kuheshimiwa. Wafilipi 2:29

Receive him therefore in the Lord with all joy, and hold such in honor,

Maana kwa ajili ya kazi ya Kristo alikaribia kufa akaponza roho yake; ili kusudi ayatimize yaliyopungua katika huduma yenu kwangu. Wafilipi 2:30

because for the work of Christ he came near to death, risking his life to supply that which was lacking in your service toward me.