Waamuzi 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
Waamuzi 5 (Swahili) Judges 5 (English)

Ndipo Debora, na Baraka mwana wa Abinoamu, wakaimba siku ile, wakisema; Waamuzi 5:1

Then sang Deborah and Barak the son of Abinoam on that day, saying,

Kwa sababu wakuu walitangulia katika Israeli, Kwa sababu watu walijitoa nafsi zao kwa hiari yao, Mhimidini Bwana. Waamuzi 5:2

For that the leaders took the lead in Israel, For that the people offered themselves willingly, Bless you Yahweh.

Sikieni, enyi wafalme; tegeni masikio, enyi wakuu; Mimi, naam mimi, nitamwimbia Bwana; Nitamhimidi Bwana, Mungu wa Israeli. Waamuzi 5:3

Hear, you kings; give ear, you princes; I, [even] I, will sing to Yahweh; I will sing praise to Yahweh, the God of Israel.

Bwana, ulipotoka katika Seiri, Ulipokwenda vitani kutoka mashamba ya Edomu, Nchi ilitetema, mbingu nazo zikadondoza maji, Naam, mawingu yakadondoza maji. Waamuzi 5:4

Yahweh, when you went forth out of Seir, When you marched out of the field of Edom, The earth trembled, the sky also dropped, Yes, the clouds dropped water.

Milima ikayeyuka mbele za uso wa Bwana, Naam hata Sinai ule mbele za uso wa Bwana, Mungu wa Israeli. Waamuzi 5:5

The mountains quaked at the presence of Yahweh, Even yon Sinai at the presence of Yahweh, the God of Israel.

Katika siku za Shamgari, mwana wa Anathi, Siku za Yaeli, njia kuu zilikuwa hazina watu; Nao wenye kusafiri walipita kwa njia za kando. Waamuzi 5:6

In the days of Shamgar the son of Anath, In the days of Jael, the highways were unoccupied, The travelers walked through byways.

Maliwali walikoma katika Israeli, walikoma, Hata mimi Debora nilipoinuka, Nilipoinuka mimi, mama katika Israeli. Waamuzi 5:7

The rulers ceased in Israel, they ceased, Until that I Deborah arose, That I arose a mother in Israel.

Walichagua miungu mipya, Ndipo kulikuwa na vita malangoni; Je! Ilionekana ngao au mkuki Katika watu elfu arobaini wa Israeli? Waamuzi 5:8

They chose new gods; Then was war in the gates: Was there a shield or spear seen Among forty thousand in Israel?

Moyo wangu unawaelekea maliwali wa Israeli, Waliojitoa nafsi zao kwa hiari yao miongoni mwa watu; Mhimidini Bwana. Waamuzi 5:9

My heart is toward the governors of Israel, Who offered themselves willingly among the people: Bless you Yahweh.

Itangazeni habari, ninyi mpandao punda weupe, Ninyi mketio juu ya mazulia ya thamani, Na ninyi mnaopita njiani kwa miguu. Waamuzi 5:10

Tell [of it], you who ride on white donkeys, You who sit on rich carpets, You who walk by the way.

Mbali na kelele za hao wapigao mishale, katika mahali pa kuteka maji, Hapo watatangaza matendo ya haki ya Bwana; Naam, matendo ya haki ya kutawala kwake katika Israeli. Ndipo watu wa Bwana waliposhuka malangoni. Waamuzi 5:11

Far from the noise of archers, in the places of drawing water, There shall they rehearse the righteous acts of Yahweh, [Even] the righteous acts of his rule in Israel. Then the people of Yahweh went down to the gates.

Amka, amka, Debora; Amka, amka, imba wimbo. Inuka, Baraka, wachukue mateka wao Waliokuchukua mateka, Ee mwana wa Abinoamu. Waamuzi 5:12

Awake, awake, Deborah; Awake, awake, utter a song: Arise, Barak, and lead away your captives, you son of Abinoam.

Ndipo walitelemka mabaki ya waungwana na ya watu; Bwana alishuka kwa ajili yangu apigane na mashujaa. Waamuzi 5:13

Then came down a remnant of the nobles [and] the people; Yahweh came down for me against the mighty.

Kutoka Efraimu walitelemka wao ambao shina lao ni katika Amaleki, Nyuma yako, Benyamini, kati ya watu wako. Kutoka Makiri walishuka maliwali, Na kutoka Zabuloni wao washikao fimbo ya mwandishi. Waamuzi 5:14

Out of Ephraim [came down] they whose root is in Amalek; After you, Benjamin, among your peoples; Out of Machir came down governors, Out of Zebulun those who handle the marshal's staff.

Na wakuu wa Isakari walikuwa pamoja na Debora. Kama alivyokuwa Isakari, ndivyo alivyokuwa Baraka. Waliingia bondeni kwa kasi miguuni pake. Kwenye vijito vya Reubeni Palikuwa na makusudi makuu mioyoni. Waamuzi 5:15

The princes of Issachar were with Deborah; As was Issachar, so was Barak; Into the valley they rushed forth at his feet. By the watercourses of Reuben There were great resolves of heart.

Mbona ulikaa katika mazizi ya kondoo, Kusikiliza filimbi zipigwazo ili kuita makundi? Kwenye vijito vya Reubeni Palikuwa na makusudi makuu mioyoni. Waamuzi 5:16

Why sat you among the sheepfolds, To hear the whistling for the flocks? At the watercourses of Reuben There were great searchings of heart.

Gileadi alikaa ng'ambo ya Yordani, Na Dani, mbona alikaa katika merikebu? Asheri alikaa kimya penye bandari ya bahari, Alikaa katika hori zake. Waamuzi 5:17

Gilead abode beyond the Jordan: Dan, why did he remain in ships? Asher sat still at the haven of the sea, Abode by his creeks.

Zabuloni ndio watu waliohatirisha roho zao hata kufa; Nao Naftali mahali palipoinuka kondeni. Waamuzi 5:18

Zebulun was a people that jeopardized their lives to the death, Naphtali, on the high places of the field.

Wafalme walikuja wakafanya vita, Ndipo wafalme wa Kanaani walifanya vita. Katika Taanaki, karibu na maji ya Megido; Hawakupata faida yo yote ya fedha. Waamuzi 5:19

The kings came and fought; Then fought the kings of Canaan. In Taanach by the waters of Megiddo: They took no gain of money.

Walipigana kutoka mbinguni, Nyota katika miendo yao zilipigana na Sisera. Waamuzi 5:20

From the sky the stars fought, From their courses they fought against Sisera.

Mto ule wa Kishoni uliwachukua, Ule mto wa zamani, mto wa Kishoni. Ee roho yangu, endelea mbele kwa nguvu. Waamuzi 5:21

The river Kishon swept them away, That ancient river, the river Kishon. My soul, march on with strength.

Ndipo kwato za farasi zilikanyaga-kanyaga Kwa sababu ya kupara-para, Kupara-para kwao wenye nguvu. Waamuzi 5:22

Then did the horse hoofs stamp By reason of the prancings, the prancings of their strong ones.

Ulaanini Merozi, alisema malaika wa Bwana, Walaanini kwa uchungu wenyeji wake; Kwa maana hawakuja kumsaidia Bwana, Kumsaidia Bwana juu ya hao wenye nguvu. Waamuzi 5:23

Curse you Meroz, said the angel of Yahweh. Curse you bitterly the inhabitants of it, Because they didn't come to the help of Yahweh, To the help of Yahweh against the mighty.

Atabarikiwa Yaeli kuliko wanawake wote; Mkewe Heberi, Mkeni, Atabarikiwa kuliko wanawake wote hemani. Waamuzi 5:24

Blessed above women shall Jael be, The wife of Heber the Kenite; Blessed shall she be above women in the tent.

Aliomba maji, naye akampa maziwa. Akamletea siagi katika sahani ya heshima. Waamuzi 5:25

He asked water, [and] she gave him milk; She brought him butter in a lordly dish.

Akanyosha mkono wake akashika kigingi, Nao mkono wake wa kuume ukashika nyundo ya fundi; Akampiga Sisera kwa hiyo nyundo, akamtoboa kichwa chake. Naam, alimpiga akamtoboa kipaji chake. Waamuzi 5:26

She put her hand to the tent-pin, Her right hand to the workmen's hammer; With the hammer she struck Sisera, she struck through his head; Yes, she pierced and struck through his temples.

Miguuni pake aliinama, akaanguka, akalala. Miguuni pake aliinama, akaanguka. Hapo alipoinama, ndipo alipoanguka amekufa. Waamuzi 5:27

At her feet he bowed, he fell, he lay; At her feet he bowed, he fell; Where he bowed, there he fell down dead.

Alichungulia dirishani, akalia, Mama yake Sisera alilia dirishani; Mbona gari lake linakawia kufika? Mbona gurudumu za gari lake zinakawia? Waamuzi 5:28

Through the window she looked forth, and cried, The mother of Sisera [cried] through the lattice, Why is his chariot so long in coming? Why do the wheels of his chariots wait?

Mabibi yake wenye akili wakamjibu, Naam, alijipa nafsi yake jawabu. Waamuzi 5:29

Her wise ladies answered her, Yes, she returned answer to herself,

Je! Hawakupata mateka na kuyagawanya, Kijakazi, vijakazi wawili, kwa kila mtu? Kwa Sisera nyara ya mavazi ya rangi mbali mbali, Nyara za mavazi ya rangi mbali mbali ya darizi; Ya rangi mbali mbali ya darizi, pande zote mbili, Juu ya shingo za hao mateka. Waamuzi 5:30

Have they not found, have they not divided the spoil? A lady, two ladies to every man; To Sisera a spoil of dyed garments, A spoil of dyed garments embroidered, Of dyed garments embroidered on both sides, on the necks of the spoil?

Na waangamie vivyo hivyo adui zako wote, Ee Bwana.

Waamuzi 5:31

So let all your enemies perish, Yahweh: But let those who love him be as the sun when he goes forth in his might. The land had rest forty years.