Waamuzi 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
Waamuzi 3 (Swahili) Judges 3 (English)

Basi haya ndiyo mataifa ambao Bwana aliwaacha, ili awajaribu Israeli kwa hao, yaani, awajaribu hao wote ambao hawakuvijua vita vyote vya Kanaani; Waamuzi 3:1

Now these are the nations which Yahweh left, to prove Israel by them, even as many [of Israel] as had not known all the wars of Canaan;

ili kwamba vizazi vya wana wa Israeli wapate kujua ili kuwafundisha vita, hasa wao ambao hawakujua vita kabla ya wakati ule; Waamuzi 3:2

only that the generations of the children of Israel might know, to teach them war, at the least such as before knew nothing of it:

aliwaacha wakuu watano wa Wafilisti, na Wakanaani wote, na Wasidoni, na Wahivi waliokaa katika kilima cha Lebanoni, toka mlima wa Baal-hermoni mpaka kuingia Hamathi. Waamuzi 3:3

[namely], the five lords of the Philistines, and all the Canaanites, and the Sidonians, and the Hivites who lived on Mount Lebanon, from Mount Baal Hermon to the entrance of Hamath.

Naye aliwaacha ili awajaribu Israeli kwa hao, apate kujua kwamba watasikiliza amri za Bwana, alizowaamuru baba zao, kwa mkono wa Musa. Waamuzi 3:4

They were [left], to prove Israel by them, to know whether they would listen to the commandments of Yahweh, which he commanded their fathers by Moses.

Basi wana wa Israeli wakaketi kati ya Wakanaani; hao Wahiti, na hao Waamori, na hao Waperizi, na hao Wahivi na hao Wayebusi; Waamuzi 3:5

The children of Israel lived among the Canaanites, the Hittites, and the Amorites, and the Perizzites, and the Hivites, and the Jebusites:

wakawaoa binti zao, na binti zao wenyewe wakawaoza wana wao waume, na kuitumikia miungu yao. Waamuzi 3:6

and they took their daughters to be their wives, and gave their own daughters to their sons and served their gods.

Wana wa Israeli walifanya yaliyo maovu mbele za macho ya Bwana, nao wakamsahau Bwana, Mungu wao, nao wakawatumikia Mabaali na Maashtorethi. Waamuzi 3:7

The children of Israel did that which was evil in the sight of Yahweh, and forgot Yahweh their God, and served the Baals and the Asheroth.

Kwa hiyo hasira za Bwana ziliwaka juu ya Israeli, naye akawauza na kuwatia mikononi mwa Kushan-rishathaimu mfalme wa Mesopotamia; na wana wa Israeli wakamtumikia huyo Kushan-rishathaimu muda wa miaka minane. Waamuzi 3:8

Therefore the anger of Yahweh was kindled against Israel, and he sold them into the hand of Cushan Rishathaim king of Mesopotamia: and the children of Israel served Cushan Rishathaim eight years.

Kisha wana wa Israeli walipomlingana Bwana, Bwana akawainulia wana wa Israeli mwokozi, aliyewaokoa, yaani, Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu. Waamuzi 3:9

When the children of Israel cried to Yahweh, Yahweh raised up a savior to the children of Israel, who saved them, even Othniel the son of Kenaz, Caleb's younger brother.

Roho ya Bwana ikamjilia juu yake, naye akawa mwamuzi wa Israeli; akatoka kwenenda vitani, naye Bwana akamtia huyo Kushan-rishathaimu, mfalme wa Mesopotamia, mkononi mwake; na mkono wake ukamshinda Kushan-rishathaimu. Waamuzi 3:10

The Spirit of Yahweh came on him, and he judged Israel; and he went out to war, and Yahweh delivered Cushan Rishathaim king of Mesopotamia into his hand: and his hand prevailed against Cushan Rishathaim.

Nayo nchi ikawa na amani muda wa miaka arobaini. Kisha Othnieli, mwana wa Kenazi, akafa. Waamuzi 3:11

The land had rest forty years. Othniel the son of Kenaz died.

Basi wana wa Israeli walifanya yaliyo maovu tena mbele za Bwana; naye Bwana akamtia nguvu Egloni mfalme wa Moabu juu ya Israeli, kwa sababu walikuwa wameyafanya yaliyo maovu mbele za macho ya Bwana. Waamuzi 3:12

The children of Israel again did that which was evil in the sight of Yahweh: and Yahweh strengthened Eglon the king of Moab against Israel, because they had done that which was evil in the sight of Yahweh.

Huyo Egloni akakutanisha kwake wana wa Amoni na Amaleki; akaenda na kuwapiga Israeli, nao wakauchukua huo mji wa mitende. Waamuzi 3:13

He gathered to him the children of Ammon and Amalek; and he went and struck Israel, and they possessed the city of palm trees.

Wana wa Israeli walimtumikia Egloni mfalme wa Moabu muda wa miaka kumi na minane. Waamuzi 3:14

The children of Israel served Eglon the king of Moab eighteen years.

Lakini wana wa Israeli walipomlilia Bwana, Bwana akawainulia mwokozi, Ehudi, mwana wa Gera, Mbenyamini, mtu aliyekuwa mwenye shoto; nao wana wa Israeli walimpelekea Egloni mfalme wa Moabu tunu mkononi mwa huyo Ehudi. Waamuzi 3:15

But when the children of Israel cried to Yahweh, Yahweh raised them up a savior, Ehud the son of Gera, the Benjamite, a man left-handed. The children of Israel sent tribute by him to Eglon the king of Moab.

Ehudi alijifanyia upanga uliokuwa na makali kuwili, urefu wake ulipata dhiraa moja; akaufunga huo upanga ndani ya nguo yake katika paja lake la mkono wa kuume. Waamuzi 3:16

Ehud made him a sword which had two edges, a cubit in length; and he girded it under his clothing on his right thigh.

Kisha akamsongezea Egloni, mfalme wa Moabu, hiyo tunu; basi Egloni alikuwa ni mtu aliyewanda sana. Waamuzi 3:17

He offered the tribute to Eglon king of Moab: now Eglon was a very fat man.

Naye hapo alipokuwa amekwisha kuisongeza hiyo tunu, akawapa ruhusa watu hao walioichukua tunu, wakaenda zao. Waamuzi 3:18

When he had made an end of offering the tribute, he sent away the people who bore the tribute.

Lakini yeye mwenyewe akageuka kutoka huko kwenye sanamu zilizokuwa karibu na Gilgali, akasema, Mimi nina ujumbe wa siri kwako wewe, Ee mfalme. Naye akasema, Nyamazeni kimya. Watu wote waliokuwa wanasimama karibu naye wakatoka na kumwacha. Waamuzi 3:19

But he himself turned back from the quarries that were by Gilgal, and said, I have a secret errand to you, king. He said, Keep silence. All who stood by him went out from him.

Basi Ehudi akamwendea; naye alikuwa anaketi peke yake katika chumba chake cha baridi. Ehudi akasema, Mimi nina ujumbe utokao kwa Mungu kwako wewe. Basi akainuka katika kiti chake. Waamuzi 3:20

Ehud came to him; and he was sitting by himself alone in the cool upper room. Ehud said, I have a message from God to you. He arose out of his seat.

Ehudi akaunyosha mkono wake wa kushoto, akaushika huo upanga kuutoa hapo katika paja lake la kuume, akamtia tumboni mwake; Waamuzi 3:21

Ehud put forth his left hand, and took the sword from his right thigh, and thrust it into his body:

hicho kipini nacho kikaingia ndani pamoja na huo upanga wenyewe; nayo mafuta yakashikamana tena juu ya upanga, kwani hakuutoa tena upanga tumboni; nao ukatokea kwa nyuma. Waamuzi 3:22

and the haft also went in after the blade; and the fat closed on the blade, for he didn't draw the sword out of his body; and it came out behind.

Ndipo Ehudi akatoka nje barazani, akamfungia milango ya hicho chumba na kuifunga kwa ufunguo. Waamuzi 3:23

Then Ehud went forth into the porch, and shut the doors of the upper room on him, and locked them.

Basi alipokuwa amekwisha toka nje, hao watumishi wake wakaenda; wakaona, na tazama, hiyo milango ya chumba ilikuwa imefungwa kwa ufunguo; nao wakasema, Hapana budi amejifunika miguu yake ndani ya chumba cha baridi. Waamuzi 3:24

Now when he was gone out, his servants came; and they saw, and, behold, the doors of the upper room were locked; and they said, Surely he is covering his feet in the upper chamber.

Wakangoja hata wakatahayari; na tazama, hakuifungua milango ya chumba; basi wakatwaa ufunguo, na kuifungua; na tazama, bwana wao alikuwa ameanguka nchi, naye amekufa. Waamuzi 3:25

They waited until they were ashamed; and, behold, he didn't open the doors of the upper room: therefore they took the key, and opened [them], and, behold, their lord was fallen down dead on the earth.

Naye Ehudi alikimbia hapo walipokuwa wakingoja, akapita huko kwenye sanamu, na kukimbilia Seira. Waamuzi 3:26

Ehud escaped while they waited, and passed beyond the quarries, and escaped to Seirah.

Ikawa, hapo alipofika akapiga tarumbeta katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu, ndipo wana wa Israeli wakatelemka pamoja naye kutoka huko milimani, naye akawatangulia. Waamuzi 3:27

It happened, when he had come, that he blew a trumpet in the hill-country of Ephraim; and the children of Israel went down with him from the hill-country, and he before them.

Akawaambia, Niandameni mimi; kwa kuwa Bwana amewatia adui zenu, Wamoabi, mikononi mwenu. Basi wakatelemka na kumfuata, wakavishika vivuko vya Yordani kinyume cha Wamoabi, wala hawakumwacha mtu kuvuka. Waamuzi 3:28

He said to them, Follow after me; for Yahweh has delivered your enemies the Moabites into your hand. They went down after him, and took the fords of the Jordan against the Moabites, and didn't allow a man to pass over.

Wakati huo wakapiga katika Wamoabi watu waume wapata kama elfu kumi, ambao wote walikuwa wanene, na wote mashujaa; hakupona hata mtu mmoja. Waamuzi 3:29

They struck of Moab at that time about ten thousand men, every lusty man, and every man of valor; and there escaped not a man.

Basi Moabu alishindwa siku hiyo chini ya mikono ya Israeli. Nayo nchi ikawa na amani muda wa miaka themanini Waamuzi 3:30

So Moab was subdued that day under the hand of Israel. The land had rest eighty years.

Tena baada yake huyo alikuwapo Shamgari mwana wa Anathi, aliyepiga katika Wafilisti watu mia sita kwa konzo la ng'ombe; yeye naye aliwaokoa Israeli. Waamuzi 3:31

After him was Shamgar the son of Anath, who struck of the Philistines six hundred men with an ox-goad: and he also saved Israel.