Waamuzi 15 Swahili & English

Listen/Download Audio
Waamuzi 15 (Swahili) Judges 15 (English)

Lakini ikawa baadaye, wakati wa mavuno ya ngano Samsoni akaenda kumtazama mkewe, akamchukulia mwana-mbuzi; akasema, Nitaingia chumbani kwa mke wangu. Lakini baba yake mwanamke hakumwacha kuingia. Waamuzi 15:1

But it happened after a while, in the time of wheat harvest, that Samson visited his wife with a kid; and he said, I will go in to my wife into the chamber. But her father wouldn't allow him to go in.

Baba yake akasema, Hakika mimi nalidhani ya kuwa umemchukia kabisa; basi nalimpa rafiki yako. Je! Ndugu yake mdogo mzuri kuliko yeye? Tafadhali, mtwae huyo badala yake. Waamuzi 15:2

Her father said, I most assuredly thought that you had utterly hated her; therefore I gave her to your companion: isn't her younger sister more beautiful than she? Please take her, instead.

Samsoni akasema, Safari hii nitakuwa sina hatia katika habari za hawa Wafilisti, hapo nitakapowadhuru. Waamuzi 15:3

Samson said to them, This time shall I be blameless in regard of the Philistines, when I do them a mischief.

Samsoni akaenda akakamata mbweha mia tatu; kisha akatwaa vienge vya moto akawafunga mbweha mkia kwa mkia, akatia kienge kati ya kila mikia miwili. Waamuzi 15:4

Samson went and caught three hundred foxes, and took firebrands, and turned tail to tail, and put a firebrand in the midst between every two tails.

Alipokwisha kuviwasha moto vile vienge, akawaachia mbweha kati ya ngano ya Wafilisti, akayateketeza matita, na ngano, hata na mashamba ya mizeituni. Waamuzi 15:5

When he had set the brands on fire, he let them go into the standing grain of the Philistines, and burnt up both the shocks and the standing grain, and also the olive groves.

Ndipo Wafilisti wakasema, Ni nani aliyetenda hivi? Wakasema, Ni huyo Samsoni, mkwewe yule Mtimna, kwa sababu alimchukua mkewe akampa mwenzake. Wafilisti wakaenda wakamteketeza yeye na baba yake kwa moto. Waamuzi 15:6

Then the Philistines said, Who has done this? They said, Samson, the son-in-law of the Timnite, because he has taken his wife, and given her to his companion. The Philistines came up, and burnt her and her father with fire.

Samsoni akawaambia, Ikiwa ninyi mnafanya mambo kama hayo, hakika nitajilipiza kisasi juu yenu, na baadaye nitakoma. Waamuzi 15:7

Samson said to them, If you do after this manner, surely I will be avenged of you, and after that I will cease.

Akawapiga upeo, mapigo makuu sana, kisha akatelemka akakaa katika ufa wa jabali la Etamu. Waamuzi 15:8

He struck them hip and thigh with a great slaughter: and he went down and lived in the cleft of the rock of Etam.

Basi Wafilisti wakapanda wakapiga kambi yao katika Yuda, wakajieneza katika Lehi. Waamuzi 15:9

Then the Philistines went up, and encamped in Judah, and spread themselves in Lehi.

Watu wa Yuda wakasema, Mbona mmekuja kupigana nasi? Wakasema, Tumepanda ili kumfunga Samsoni, kumtenda yeye kama alivyotutenda sisi. Waamuzi 15:10

The men of Judah said, Why are you come up against us? They said, To bind Samson are we come up, to do to him as he has done to us.

Ndipo watu elfu tatu wa Yuda wakatelemka hata ule ufa wa jabali la Etamu, wakamwambia Samsoni, Je! Hujui ya kuwa Wafilisti wanatutawala? Ni nini hii, basi, uliyotutenda? Akawaambia, Kadiri ile walivyonitenda mimi, ndivyo nilivyowatenda wao. Waamuzi 15:11

Then three thousand men of Judah went down to the cleft of the rock of Etam, and said to Samson, "Don't you know that the Philistines are rulers over us? What then is this that you have done to us?" He said to them, As they did to me, so have I done to them.

Wakamwambia, Tumeshuka ili kukufunga, tupate kukutia katika mikono ya Wafilisti. Samsoni akawaambia, Niapieni ya kwamba ninyi wenyewe hamtaniangukia. Waamuzi 15:12

They said to him, We have come down to bind you, that we may deliver you into the hand of the Philistines. Samson said to them, Swear to me that you will not fall on me yourselves.

Wakamwambia, wakisema, Vema, lakini tutakufunga sana, na kukutia katika mikono yao; lakini hakika hatutakuua. Basi wakamfunga kwa kamba mbili mpya, wakamchukua kutoka huko jabalini. Waamuzi 15:13

They spoke to him, saying, No; but we will bind you fast, and deliver you into their hand: but surely we will not kill you. They bound him with two new ropes, and brought him up from the rock.

Alipofika Lehi, Wafilisti wakapiga kelele walipokutana naye; ndipo roho ya Bwana ikamjia kwa nguvu, na zile kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa kama kitani iliyoteketezwa kwa moto, na vile vifungo vyake vikaanguka mikononi mwake. Waamuzi 15:14

When he came to Lehi, the Philistines shouted as they met him: and the Spirit of Yahweh came mightily on him, and the ropes that were on his arms became as flax that was burnt with fire, and his bands dropped from off his hands.

Naye akaona mfupa mbichi wa taya ya punda, akautwaa, akapiga watu elfu kwa mfupa huo; Waamuzi 15:15

He found a fresh jawbone of a donkey, and put forth his hand, and took it, and struck a thousand men therewith.

Samsoni akasema, Kwa taya ya punda chungu juu ya chungu, Kwa taya ya punda nimepiga watu elfu. Waamuzi 15:16

Samson said, With the jawbone of a donkey, heaps on heaps, With the jawbone of a donkey I have struck a thousand men.

Ikawa, alipokuwa amekwisha kunena akautupa ule mfupa wa taya mkononi mwake; na mahali pale pakaitwa Ramath-lehi. Waamuzi 15:17

It happened, when he had made an end of speaking, that he cast away the jawbone out of his hand; and that place was called Ramath Lehi.

Kisha akaona kiu sana, akamwita Bwana akasema, Wewe umetupa wokovu huu kwa mkono wa mtumishi wako; na sasa nitakufa kwa kiu, na kuanguka katika mikono ya watu wasiotahiriwa. Waamuzi 15:18

He was very thirsty, and called on Yahweh, and said, You have given this great deliverance by the hand of your servant; and now shall I die for thirst, and fall into the hand of the uncircumcised.

Lakini Mungu akapasua mahali penye shimo palipo katika Lehi, pakatoka maji; naye alipokwisha kunywa, roho yake ikamrudia, akaburudika; kwa hiyo jina la mahali pale likaitwa Enhakore, napo pa katika Lehi hata hivi leo. Waamuzi 15:19

But God split the hollow place that is in Lehi, and water came out of it. When he had drunk, his spirit came again, and he revived: therefore the name of it was called En Hakkore, which is in Lehi, to this day.

Naye akawa mwamuzi wa Israeli: katika siku za Wafilisti muda wa miaka ishirini. Waamuzi 15:20

He judged Israel in the days of the Philistines twenty years.