2 Mambo ya Nyakati 9 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Mambo ya Nyakati 9 (Swahili) 2nd Chronicles 9 (English)

Na malkia wa Sheba aliposikia habari za Sulemani, alikuja ili amjaribu Sulemani kwa maswali ya fumbo huko Yerusalemu, mwenye wafuasi wengi, na ngamia wachukuao manukato, na dhahabu nyingi sana, na vito vya thamani; alipomfikilia Sulemani, akamwambia mambo yote aliyokuwa nayo moyoni mwake. 2 Mambo ya Nyakati 9:1

When the queen of Sheba heard of the fame of Solomon, she came to prove Solomon with hard questions at Jerusalem, with a very great train, and camels that bore spices, and gold in abundance, and precious stones: and when she was come to Solomon, she talked with him of all that was in her heart.

Naye Sulemani akamfumbulia maswali yake yote; wala halikuwako neno alilofichiwa Sulemani, asimwambie. 2 Mambo ya Nyakati 9:2

Solomon told her all her questions; and there was not anything hid from Solomon which he didn't tell her.

Naye malkia wa Sheba alipoona hekima ya Sulemani, na nyumba aliyoijenga, 2 Mambo ya Nyakati 9:3

When the queen of Sheba had seen the wisdom of Solomon, and the house that he had built,

na vyakula vya mezani mwake, na kikao cha watumishi wake, na usimamizi wao wangoje wake, na mavazi yao; na wanyweshaji wake, na mavazi yao; na daraja yake ya kupandia mpaka nyumba ya Bwana; roho yake ilizimia. 2 Mambo ya Nyakati 9:4

and the food of his table, and the sitting of his servants, and the attendance of his ministers, and their clothing, his cup bearers also, and their clothing, and his ascent by which he went up to the house of Yahweh; there was no more spirit in her.

Akamwambia mfalme, Ndizo kweli habari zile nilizozisikia katika nchi yangu za mambo yako na za hekima yako. 2 Mambo ya Nyakati 9:5

She said to the king, It was a true report that I heard in my own land of your acts, and of your wisdom.

Lakini mimi sikuyasadiki maneno yao, hata nilipokuja na kuona kwa macho yangu; wala, tazama, ukuu wa hekima yako sikuambiwa nusu; wewe umezidi kuliko habari nilizozisikia. 2 Mambo ya Nyakati 9:6

However I didn't believe their words, until I came, and my eyes had seen it; and, behold, the half of the greatness of your wisdom was not told me: you exceed the fame that I heard.

Heri watu wako, na heri hawa watumishi wako, wasimamao mbele yako sikuzote, wakisikia hekima yako. 2 Mambo ya Nyakati 9:7

Happy are your men, and happy are these your servants, who stand continually before you, and hear your wisdom.

Na ahimidiwe Bwana, Mungu wako, aliyependezwa nawe, ili akuweke juu ya kiti chake cha enzi, kuwa mfalme wake Bwana, Mungu wako; kwa kuwa Mungu wako amewapenda Israeli, kuwathibitisha milele, kwa hiyo amekufanya kuwa mfalme juu yao, ufanye hukumu na haki. 2 Mambo ya Nyakati 9:8

Blessed be Yahweh your God, who delighted in you, to set you on his throne, to be king for Yahweh your God: because your God loved Israel, to establish them forever, therefore made he you king over them, to do justice and righteousness.

Basi akampa mfalme talanta mia na ishirini za dhahabu, na manukato mengi mengi sana, na vito vya thamani; wala haukuja wingi wa manukato, kama hayo aliyopewa mfalme Sulemani na malkia wa Sheba. 2 Mambo ya Nyakati 9:9

She gave the king one hundred and twenty talents of gold, and spices in great abundance, and precious stones: neither was there any such spice as the queen of Sheba gave to king Solomon.

Tena watumishi wa Hiramu, pamoja na watumishi wa Sulemani, walioleta dhahabu kutoka Ofiri, wakaleta miti ya msandali, na vito vya thamani. 2 Mambo ya Nyakati 9:10

The servants also of Huram, and the servants of Solomon, who brought gold from Ophir, brought algum trees and precious stones.

Mfalme akayafanya kwa miti hiyo ya msandali madari ya nyumba ya Bwana, na nyumba ya mfalme, na vinubi na vinanda vya hao waimbaji; wala haijatokea kama hiyo katika nchi ya Yuda. 2 Mambo ya Nyakati 9:11

The king made of the algum trees terraces for the house of Yahweh, and for the king's house, and harps and psalteries for the singers: and there were none such seen before in the land of Judah.

Mfalme Sulemani akampa malkia wa Sheba haja yake yote, kila alilotaka, zaidi ya vile alivyomletea mfalme. Basi akarudi, akaenda zake katika nchi yake, yeye na watumishi wake. 2 Mambo ya Nyakati 9:12

King Solomon gave to the queen of Sheba all her desire, whatever she asked, besides that which she had brought to the king. So she turned, and went to her own land, she and her servants.

Basi uzani wa dhahabu iliyomfikia Sulemani mwaka mmoja, ndio talanta mia sita sitini na sita za dhahabu; 2 Mambo ya Nyakati 9:13

Now the weight of gold that came to Solomon in one year was six hundred and sixty-six talents of gold,

mbali na ile waliyoileta wachuuzi na wafanya biashara; tena wafalme wote wa Arabuni, na maliwali wa nchi wakamletea Sulemani dhahabu na fedha. 2 Mambo ya Nyakati 9:14

besides that which the traders and merchants brought: and all the kings of Arabia and the governors of the country brought gold and silver to Solomon.

Mfalme Sulemani akafanya ngao mia mbili za dhahabu iliyofuliwa; ngao moja hupata shekeli mia sita za dhahabu iliyofuliwa. 2 Mambo ya Nyakati 9:15

King Solomon made two hundred bucklers of beaten gold; six hundred [shekels] of beaten gold went to one buckler.

Na vigao mia tatu vya dhahabu iliyofuliwa; kigao kimoja hupata shekeli mia tatu za dhahabu; mfalme akaviweka katika nyumba ya mwitu wa Lebanoni. 2 Mambo ya Nyakati 9:16

[he made] three hundred shields of beaten gold; three hundred [shekels] of gold went to one shield: and the king put them in the house of the forest of Lebanon.

Tena mfalme akafanya kiti cha enzi kikubwa cha pembe, akakifunikiza kwa dhahabu iliyo safi. 2 Mambo ya Nyakati 9:17

Moreover the king made a great throne of ivory, and overlaid it with pure gold.

Kiti kile kilikuwa na daraja sita, tena na kikao cha miguu cha dhahabu, navyo vilikuwa vimeshikamana na kiti; na mikono huko na huko mahali pa kuketi, na simba wawili wakisimama kando ya hiyo mikono. 2 Mambo ya Nyakati 9:18

nd there were six steps to the throne, with a footstool of gold, which were fastened to the throne, and stays on either side by the place of the seat, and two lions standing beside the stays.

Na simba kumi na wawili wamesimama juu ya daraja sita, huko na huko; wala hakikufanyika kwa mfano wake katika ufalme wo wote. 2 Mambo ya Nyakati 9:19

Twelve lions stood there on the one side and on the other on the six steps: there was nothing like it made in any kingdom.

Na vyombo vyote vya kunywea vya mfalme Sulemani vilikuwa vya dhahabu, na vyombo vyote vya nyumba ya mwitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu iliyosafika; fedha haikuhesabiwa kuwa kitu siku za Sulemani. 2 Mambo ya Nyakati 9:20

All king Solomon's drinking vessels were of gold, and all the vessels of the house of the forest of Lebanon were of pure gold: silver was nothing accounted of in the days of Solomon.

Kwa kuwa mfalme alikuwa na merikebu zilizokwenda Tarshishi pamoja na watumishi wa Hiramu; mara moja katika miaka mitatu huja merikebu za Tarshishi, zikileta dhahabu, na fedha, na pembe, na nyani, na tausi. 2 Mambo ya Nyakati 9:21

For the king had ships that went to Tarshish with the servants of Huram; once every three years came the ships of Tarshish, bringing gold, and silver, ivory, and apes, and peacocks.

Basi mfalme Sulemani akawapita wafalme wote wa duniani kwa mali, na kwa hekima. 2 Mambo ya Nyakati 9:22

So king Solomon exceeded all the kings of the earth in riches and wisdom.

Wafalme wote wa duniani wakamtafuta Sulemani uso wake, ili waisikie hekima yake, Mungu aliyomtia moyoni. 2 Mambo ya Nyakati 9:23

All the kings of the earth sought the presence of Solomon, to hear his wisdom, which God had put in his heart.

Wakaleta kila mtu zawadi yake, vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na mavazi, na silaha, na manukato, na farasi, na nyumbu, hesabu yake ya mwaka kwa mwaka. 2 Mambo ya Nyakati 9:24

They brought every man his tribute, vessels of silver, and vessels of gold, and clothing, armor, and spices, horses, and mules, a rate year by year.

Sulemani akawa na mazizi ya farasi na magari elfu nne, na wapandao farasi kumi na mbili elfu, aliowaweka katika miji ya magari, na pamoja na mfalme huko Yerusalemu. 2 Mambo ya Nyakati 9:25

Solomon had four thousand stalls for horses and chariots, and twelve thousand horsemen, that he bestowed in the chariot cities, and with the king at Jerusalem.

Akatawala juu ya wafalme wote toka Mto hata nchi ya Wafilisti, na hata mpaka wa Misri. 2 Mambo ya Nyakati 9:26

He ruled over all the kings from the River even to the land of the Philistines, and to the border of Egypt.

Mfalme akafanya fedha humo Yerusalemu kuwa kama mawe, na mierezi akaifanya kuwa kama mikuyu iliyomo Shefela, kwa kuwa mingi. 2 Mambo ya Nyakati 9:27

The king made silver to be in Jerusalem as stones, and cedars made he to be as the sycamore trees that are in the lowland, for abundance.

Wakamletea Sulemani farasi kutoka Misri, na kutoka nchi zote. 2 Mambo ya Nyakati 9:28

They brought horses for Solomon out of Egypt, and out of all lands.

Basi mambo yake Sulemani yaliyosalia, ya kwanza, na ya mwisho, je! Hayakuandikwa katika tarehe ya Nathani nabii, katika unabii wa Ahiya, Mshiloni, na katika maono ya Ido mwonaji juu ya Yeroboamu mwana wa Nebati? 2 Mambo ya Nyakati 9:29

Now the rest of the acts of Solomon, first and last, aren't they written in the history of Nathan the prophet, and in the prophecy of Ahijah the Shilonite, and in the visions of Iddo the seer concerning Jeroboam the son of Nebat?

Akatawala Sulemani katika Yerusalemu juu ya Israeli wote miaka arobaini. 2 Mambo ya Nyakati 9:30

Solomon reigned in Jerusalem over all Israel forty years.

Naye Sulemani akalala na baba zake, akazikwa mjini mwa Daudi babaye; akatawala Rehoboamu mwanawe badala yake.

2 Mambo ya Nyakati 9:31

Solomon slept with his fathers, and he was buried in the city of David his father: and Rehoboam his son reigned in his place.