2 Mambo ya Nyakati 36 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Mambo ya Nyakati 36 (Swahili) 2nd Chronicles 36 (English)

Watu wa nchi wakamtwaa Yehoahazi mwana wa Yosia, wakamtawaza awe mfalme katika Yerusalemu badala ya babaye. 2 Mambo ya Nyakati 36:1

Then the people of the land took Jehoahaz the son of Josiah, and made him king in his father's place in Jerusalem.

Yehoahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitatu alipoanza kutawala; akatawala huko Yerusalemu miezi mitatu. 2 Mambo ya Nyakati 36:2

Joahaz was twenty-three years old when he began to reign; and he reigned three months in Jerusalem.

Naye mfalme wa Misri akamwondoa katika Yerusalemu, akaitoza nchi talanta mia za fedha, na talanta moja ya dhahabu. 2 Mambo ya Nyakati 36:3

The king of Egypt deposed him at Jerusalem, and fined the land one hundred talents of silver and a talent of gold.

Mfalme wa Misri akamtawaza Eliakimu nduguye awe mfalme juu ya Yuda na Yerusalemu, akambadilisha jina lake kuwa Yehoyakimu. Neko akamtwaa Yehoahazi nduguye, akamchukua mpaka Misri. 2 Mambo ya Nyakati 36:4

The king of Egypt made Eliakim his brother king over Judah and Jerusalem, and changed his name to Jehoiakim. Neco took Joahaz his brother, and carried him to Egypt.

Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka kumi na mmoja; akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, Mungu wake. 2 Mambo ya Nyakati 36:5

Jehoiakim was Twenty-five years old when he began to reign; and he reigned eleven years in Jerusalem: and he did that which was evil in the sight of Yahweh his God.

Juu yake akakwea Nebukadreza, 2 Mambo ya Nyakati 36:6

Against him came up Nebuchadnezzar king of Babylon, and bound him in fetters, to carry him to Babylon.

Nebukadreza akachukua baadhi ya vyombo vya nyumba ya Bwana mpaka Babeli, akavitia katika hekalu lake huko Babeli. 2 Mambo ya Nyakati 36:7

Nebuchadnezzar also carried of the vessels of the house of Yahweh to Babylon, and put them in his temple at Babylon.

Basi mambo yote ya Yehoyakimu yaliyosalia, na machukizo yake aliyoyafanya, nayo yaliyoonekana kwake, tazama, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda; na Yekonia 2 Mambo ya Nyakati 36:8

Now the rest of the acts of Jehoiakim, and his abominations which he did, and that which was found in him, behold, they are written in the book of the kings of Israel and Judah: and Jehoiachin his son reigned in his place.

Yekonia alikuwa na umri wa miaka kumi na minane alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miezi mitatu na siku kumi; akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana. 2 Mambo ya Nyakati 36:9

Jehoiachin was eight years old when he began to reign; and he reigned three months and ten days in Jerusalem: and he did that which was evil in the sight of Yahweh.

Mwaka ulipokwisha, Nebukadreza akatuma wajumbe, akamchukua mpaka Babeli; pamoja na vyombo vya thamani vya nyumba ya Bwana; akamtawaza Sedekia nduguye awe mfalme juu ya Yuda na Yerusalemu. 2 Mambo ya Nyakati 36:10

At the return of the year king Nebuchadnezzar sent, and brought him to Babylon, with the goodly vessels of the house of Yahweh, and made Zedekiah his brother king over Judah and Jerusalem.

Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja, alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka kumi na mmoja; 2 Mambo ya Nyakati 36:11

Zedekiah was twenty-one years old when he began to reign; and he reigned eleven years in Jerusalem:

akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, Mungu wake; wala hakujinyenyekesha mbele ya Yeremia nabii aliponena kwa kinywa cha Bwana. 2 Mambo ya Nyakati 36:12

and he did that which was evil in the sight of Yahweh his God; he didn't humble himself before Jeremiah the prophet [speaking] from the mouth of Yahweh.

Tena akamwasi mfalme Nebukadreza, aliyemwapisha kwa Mungu; lakini akajifanyia shingo ngumu, akajitia moyo nguvu asimgeukie Bwana, Mungu wa Israeli. 2 Mambo ya Nyakati 36:13

He also rebelled against king Nebuchadnezzar, who had made him swear by God: but he stiffened his neck, and hardened his heart against turning to Yahweh, the God of Israel.

Na zaidi ya hayo wakuu wote wa makuhani, na watu, wakakosa mno sawasawa na machukizo yote ya mataifa; wakainajisi nyumba ya Bwana aliyoitakasa katika Yerusalemu. 2 Mambo ya Nyakati 36:14

Moreover all the chiefs of the priests, and the people, trespassed very greatly after all the abominations of the nations; and they polluted the house of Yahweh which he had made holy in Jerusalem.

Naye Bwana, Mungu wa baba zao, akatuma kwao kwa mikono ya wajumbe wake, akiondoka mapema, na kutuma; kwa sababu aliwahurumia watu wake, na makao yake; 2 Mambo ya Nyakati 36:15

Yahweh, the God of their fathers, sent to them by his messengers, rising up early and sending, because he had compassion on his people, and on his dwelling-place:

lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na kuyadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, hata ilipozidi ghadhabu ya Bwana juu ya watu wake, hata kusiwe na kuponya. 2 Mambo ya Nyakati 36:16

but they mocked the messengers of God, and despised his words, and scoffed at his prophets, until the wrath of Yahweh arose against his people, until there was no remedy.

Kwa hiyo akaleta juu yao mfalme wa Wakaldayo, aliyewaua vijana wao kwa upanga nyumbani mwa patakatifu pao, asiwahurumie kijana wala mwanamwali, mzee wala mkongwe; akawatia wote mkononi mwake. 2 Mambo ya Nyakati 36:17

Therefore he brought on them the king of the Chaldeans, who killed their young men with the sword in the house of their sanctuary, and had no compassion on young man or virgin, old man or gray-headed: he gave them all into his hand.

Na vyombo vyote vya nyumba ya Mungu, vikubwa kwa vidogo, na hazina za nyumba ya Bwana, na hazina za mfalme, na za wakuu wake; vyote pia akavileta Babeli. 2 Mambo ya Nyakati 36:18

All the vessels of the house of God, great and small, and the treasures of the house of Yahweh, and the treasures of the king, and of his princes, all these he brought to Babylon.

Wakaiteketeza nyumba ya Mungu, wakaubomoa ukuta wa Yerusalemu, wakayateketeza kwa moto majumba yake yote, wakaviharibu vyombo vyake vyote vya thamani. 2 Mambo ya Nyakati 36:19

They burnt the house of God, and broke down the wall of Jerusalem, and burnt all the palaces of it with fire, and destroyed all the goodly vessels of it.

Na wale waliookoka na upanga akawachukua mpaka Babeli; wakamtumikia yeye na wanawe hata kulipoingia milki ya Uajemi; 2 Mambo ya Nyakati 36:20

Those who had escaped from the sword carried he away to Babylon; and they were servants to him and his sons until the reign of the kingdom of Persia:

ili kulitimiza neno la Bwana kwa kinywa cha Yeremia, hata nchi itakapofurahia sabato zake; kwa maana siku zote ilipokaa ukiwa ilishika sabato, kutimiza miaka sabini. 2 Mambo ya Nyakati 36:21

to fulfill the word of Yahweh by the mouth of Jeremiah, until the land had enjoyed its Sabbaths: [for] as long as it lay desolate it kept Sabbath, to fulfill seventy years.

Ikawa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la Bwana alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, Bwana akamwamsha roho yake Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia, akisema, 2 Mambo ya Nyakati 36:22

Now in the first year of Cyrus king of Persia, that the word of Yahweh by the mouth of Jeremiah might be accomplished, Yahweh stirred up the spirit of Cyrus king of Persia, so that he made a proclamation throughout all his kingdom, and [put it] also in writing, saying,

Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi; Bwana, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za dunia; naye ameniagiza nimjengee nyumba katika Yerusalemu, ulioko Yuda. Basi kila mtu katika ninyi nyote mlio watu wake, Bwana, Mungu wake, na awe pamoja naye, na akwee.

2 Mambo ya Nyakati 36:23

Thus says Cyrus king of Persia, All the kingdoms of the earth has Yahweh, the God of heaven, given me; and he has charged me to build him a house in Jerusalem, which is in Judah. Whoever there is among you of all his people, Yahweh his God be with him, and let him go up.