2 Mambo ya Nyakati 35 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Mambo ya Nyakati 35 (Swahili) 2nd Chronicles 35 (English)

Naye Yosia akamfanyia Bwana pasaka huko Yerusalemu; wakachinja pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza. 2 Mambo ya Nyakati 35:1

Josiah kept a Passover to Yahweh in Jerusalem: and they killed the Passover on the fourteenth [day] of the first month.

Akawasimamisha makuhani katika malinzi yao, akawatia moyo kufanya utumishi wa nyumba ya Bwana. 2 Mambo ya Nyakati 35:2

He set the priests in their offices, and encouraged them to the service of the house of Yahweh.

Akawaambia Walawi, waliowafundisha Israeli wote, waliotakasika kwa Bwana, Wekeni sanduku takatifu katika nyumba aliyoijenga Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli; hamtakuwa tena na mzigo mabegani; sasa mtumikieni Bwana, Mungu wenu, na watu wake Israeli. 2 Mambo ya Nyakati 35:3

He said to the Levites who taught all Israel, who were holy to Yahweh, Put the holy ark in the house which Solomon the son of David king of Israel did build; there shall no more be a burden on your shoulders: now serve Yahweh your God, and his people Israel.

Mkajiweke tayari kwa kadiri ya nyumba za baba zenu, kwa zamu zenu, kama alivyoandika Daudi mfalme wa Israeli, na kama alivyoandika Sulemani mwanawe. 2 Mambo ya Nyakati 35:4

Prepare yourselves after your fathers' houses by your divisions, according to the writing of David king of Israel, and according to the writing of Solomon his son.

Mkasimame katika patakatifu, kama walivyogawanyika ndugu zenu, wana wa watu, kufuata nyumba za mababa, kadiri ya mgawanyiko wa kila nyumba ya baba, ya Walawi. 2 Mambo ya Nyakati 35:5

Stand in the holy place according to the divisions of the fathers' houses of your brothers the children of the people, and [let there be for each] a portion of a fathers' house of the Levites.

Mkachinje pasaka, mkajitakase, mkawatengenezee ndugu zenu, kutenda sawasawa na neno la Bwana kwa mkono wa Musa. 2 Mambo ya Nyakati 35:6

Kill the Passover, and sanctify yourselves, and prepare for your brothers, to do according to the word of Yahweh by Moses.

Tena Yosia akawapa wana wa watu, matoleo ya makundi, wana-kondoo na wana-mbuzi, yote yawe kwa ajili ya matoleo ya pasaka, wote waliokuwako, wakipata thelathini elfu, na ng'ombe elfu tatu; hao walitoka katika mali za mfalme. 2 Mambo ya Nyakati 35:7

Josiah gave to the children of the people, of the flock, lambs and kids, all of them for the Passover offerings, to all who were present, to the number of thirty thousand, and three thousand bulls: these were of the king's substance.

Na wakuu wake wakawapa watu, na makuhani na Walawi matoleo ya hiari. Hilkia na wana na Yehieli, wakubwa wa nyumba ya Mungu, wakawapa makuhani, kuwa matoleo ya pasaka, wana-kondoo elfu mbili na mia sita, na ng'ombe mia tatu. 2 Mambo ya Nyakati 35:8

His princes gave for a freewill-offering to the people, to the priests, and to the Levites. Hilkiah and Zechariah and Jehiel, the rulers of the house of God, gave to the priests for the Passover offerings two thousand and six hundred [small cattle], and three hundred oxen.

Konania naye, na Shemaya, na Nethaneli, ndugu zake, na Hashabia, na Yeieli, na Yozabadi, wakuu wa Walawi, wakawapa Walawi, kuwa matoleo ya pasaka, wana-kondoo elfu tano, na ng'ombe mia tano. 2 Mambo ya Nyakati 35:9

Conaniah also, and Shemaiah and Nethanel, his brothers, and Hashabiah and Jeiel and Jozabad, the chiefs of the Levites, gave to the Levites for the Passover offerings five thousand [small cattle], and five hundred oxen.

Hivyo huduma ikatengenezwa, wakasimama makuhani mahali pao, na Walawi kwa zamu zao, kama alivyoamuru mfalme. 2 Mambo ya Nyakati 35:10

So the service was prepared, and the priests stood in their place, and the Levites by their divisions, according to the king's commandment.

Wakachinja pasaka, nao makuhani wakamimina damu waliyopokea mikononi mwao, Walawi wakachuna. 2 Mambo ya Nyakati 35:11

They killed the Passover, and the priests sprinkled [the blood which they received] of their hand, and the Levites flayed them.

Wakaziondoa sadaka za kuteketezwa, wawape wana wa watu, kama walivyogawanyika kufuata nyumba za mababa, ili wamtolee Bwana, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Musa. Nao ng'ombe wakawafanya vivyo hivyo. 2 Mambo ya Nyakati 35:12

They removed the burnt offerings, that they might give them according to the divisions of the fathers' houses of the children of the people, to offer to Yahweh, as it is written in the book of Moses. So did they with the oxen.

Wakaioka moto pasaka kama ilivyo sheria; wakatokosa matoleo matakatifu vyunguni, na masufuriani, na makaangoni, wakawachukulia upesi wana wa watu wote. 2 Mambo ya Nyakati 35:13

They roasted the Passover with fire according to the ordinance: and the holy offerings boiled they in pots, and in caldrons, and in pans, and carried them quickly to all the children of the people.

Baadaye wakajiandalia wenyewe, na makuhani; kwa sababu makuhani, wana wa Haruni, walikuwa na kazi ya kutoa sadaka za kuteketezwa, na mafuta hata usiku; kwa hiyo Walawi wakajiandalia wenyewe, na makuhani, wana wa Haruni. 2 Mambo ya Nyakati 35:14

Afterward they prepared for themselves, and for the priests, because the priests the sons of Aaron [were busied] in offering the burnt offerings and the fat until night: therefore the Levites prepared for themselves, and for the priests the sons of Aaron.

Nao waimbaji, wana wa Asafu wakasimama mahali pao, kama alivyoamuru Daudi, na Asafu, na Hemani, na Yeduthuni mwonaji wa mfalme; nao mabawabu walikuwa katika kila lango; hawakuhitaji kuondoka katika huduma yao, kwa kuwa ndugu zao Walawi wakawaandalia. 2 Mambo ya Nyakati 35:15

The singers the sons of Asaph were in their place, according to the commandment of David, and Asaph, and Heman, and Jeduthun the king's seer; and the porters were at every gate: they didn't need to depart from their service; for their brothers the Levites prepared for them.

Basi huduma yote ya Bwana ikatengenezwa siku ile ile, kuifanya pasaka, na kutoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya Bwana, kama alivyoamuru mfalme Yosia. 2 Mambo ya Nyakati 35:16

So all the service of Yahweh was prepared the same day, to keep the Passover, and to offer burnt-offerings on the altar of Yahweh, according to the commandment of king Josiah.

Wana wa Israeli waliokuwapo wakafanya pasaka wakati ule, na sikukuu ya mikate isiyochachwa muda wa siku saba. 2 Mambo ya Nyakati 35:17

The children of Israel who were present kept the Passover at that time, and the feast of unleavened bread seven days.

Wala haikufanyika pasaka kama ile katika Israeli tangu siku za nabii Samweli; wala wafalme wa Israeli hawakufanya hata mmoja wao pasaka kama ile Yosia aliyoifanya, pamoja na makuhani, na Walawi, na Yuda wote na Israeli waliokuwapo, na wenyeji wa Yerusalemu. 2 Mambo ya Nyakati 35:18

There was no Passover like that kept in Israel from the days of Samuel the prophet; neither did any of the kings of Israel keep such a Passover as Josiah kept, and the priests, and the Levites, and all Judah and Israel who were present, and the inhabitants of Jerusalem.

Katika mwaka wa kumi na nane wa kutawala kwake Yosia ikafanyika pasaka hiyo. 2 Mambo ya Nyakati 35:19

In the eighteenth year of the reign of Josiah was this Passover kept.

Baada ya hayo yote, alipokwisha Yosia kulitengeneza hekalu, Neko, mfalme wa Misri, akakwea ili kupigana Karkemishi karibu na Frati; naye Yosia akatoka juu yake. 2 Mambo ya Nyakati 35:20

After all this, when Josiah had prepared the temple, Neco king of Egypt went up to fight against Carchemish by the Euphrates: and Josiah went out against him.

Lakini yeye akatuma kwake wajumbe, kusema, Ni nini niliyo nayo mimi na wewe, Ee mfalme wa Yuda? Sikuja juu yako leo, lakini juu ya nyumba niliyo na vita nayo; naye Mungu ameniamuru nifanye haraka; acha basi kumpinga Mungu, aliye pamoja nami, asikuharibu. 2 Mambo ya Nyakati 35:21

But he sent ambassadors to him, saying, What have I to do with you, you king of Judah? [I come] not against you this day, but against the house with which I have war; and God has commanded me to make haste: forbear you from [meddling with] God, who is with me, that he not destroy you.

Walakini Yosia hakukubali kumgeuzia uso mbali, akajibadilisha apate kupigana naye, asiyasikilize maneno ya Neko, yaliyotoka kinywani kwa Mungu, akaja kupigana bondeni mwa Megido. 2 Mambo ya Nyakati 35:22

Nevertheless Josiah would not turn his face from him, but disguised himself, that he might fight with him, and didn't listen to the words of Neco from the mouth of God, and came to fight in the valley of Megiddo.

Nao wapiga upinde wakampiga Yosia; naye mfalme akawaambia watumishi wake, Niondoeni; kwani nimejeruhiwa sana. 2 Mambo ya Nyakati 35:23

The archers shot at king Josiah; and the king said to his servants, Have me away; for I am sore wounded.

Basi watumishi wake wakamtoa garini, wakamtia katika gari la pili alilokuwa nalo, wakamleta Yerusalemu; naye akafa, akazikwa makaburini mwa babaze. Wakamlilia Yosia Yuda wote na Yerusalemu. 2 Mambo ya Nyakati 35:24

So his servants took him out of the chariot, and put him in the second chariot that he had, and brought him to Jerusalem; and he died, and was buried in the tombs of his fathers. All Judah and Jerusalem mourned for Josiah.

Naye Yeremia akamlilia Yosia; na waimbaji wote waume kwa wake wakamtaja Yosia katika maombolezo yao, hata leo; hata wakayafanya kuwa ada kwa Israeli; nayo, tazama, yameandikwa katika maombolezo. 2 Mambo ya Nyakati 35:25

Jeremiah lamented for Josiah: and all the singing men and singing women spoke of Josiah in their lamentations to this day; and they made them an ordinance in Israel: and, behold, they are written in the lamentations.

Basi mambo yote ya Yosia yaliyosalia, na matendo yake mema, sawasawa na yote yaliyoandikwa katika torati ya Bwana, 2 Mambo ya Nyakati 35:26

Now the rest of the acts of Josiah, and his good deeds, according to that which is written in the law of Yahweh,

na mambo yake, ya kwanza na ya mwisho, tazama, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda. 2 Mambo ya Nyakati 35:27

and his acts, first and last, behold, they are written in the book of the kings of Israel and Judah.