2 Mambo ya Nyakati 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Mambo ya Nyakati 3 (Swahili) 2nd Chronicles 3 (English)

Ndipo Sulemani akaanza kuijenga nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, juu ya mlima Moria, pale Bwana alipomtokea Daudi babaye alipotengeza mahali pale alipoagiza Daudi, katika kiwanja cha kupuria cha Arauna Myebusi. 2 Mambo ya Nyakati 3:1

Then Solomon began to build the house of Yahweh at Jerusalem on Mount Moriah, where [Yahweh] appeared to David his father, which he made ready in the place that David had appointed, in the threshing floor of Ornan the Jebusite.

Akaanza kujenga siku ya pili ya mwezi wa pili katika mwaka wa nne wa kutawala kwake. 2 Mambo ya Nyakati 3:2

He began to build in the second [day] of the second month, in the fourth year of his reign.

Basi hii ndiyo misingi ya majengo ya nyumba ya Mungu aliyoiweka Sulemani. Urefu wake kwa mikono ya cheo cha kwanza ulikuwa mikono sitini, na upana wake mikono ishirini. 2 Mambo ya Nyakati 3:3

Now these are the foundations which Solomon laid for the building of the house of God. The length by cubits after the first measure was sixty cubits, and the breadth twenty cubits.

Na ukumbi uliokuwa mbele yake, urefu wake kadiri ya upana wa nyumba ulikuwa mikono ishirini, na kwenda juu kwake mia na ishirini; akaufunikiza ndani kwa dhahabu safi. 2 Mambo ya Nyakati 3:4

The porch that was before [the house], the length of it, according to the breadth of the house, was twenty cubits, and the height one hundred twenty; and he overlaid it within with pure gold.

Nayo nyumba kubwa akaifunika miti ya miberoshi, aliyoifunikiza kwa dhahabu safi, akaifanyizia mitende na minyororo. 2 Mambo ya Nyakati 3:5

The greater house he made a ceiling with fir-wood, which he overlaid with fine gold, and worked thereon palm trees and chains.

Akaipamba nyumba kwa vito iwe na uzuri; nayo dhahabu ilikuwa dhahabu ya Parvaimu. 2 Mambo ya Nyakati 3:6

He garnished the house with precious stones for beauty: and the gold was gold of Parvaim.

Tena, akaifunikiza kwa dhahabu nyumba, na boriti, na vizingiti, na kuta zake, na milango yake; akachora makerubi kutani. 2 Mambo ya Nyakati 3:7

He overlaid also the house, the beams, the thresholds, and the walls of it, and the doors of it, with gold; and engraved cherubim on the walls.

Akaifanya nyumba ya patakatifu pa patakatifu; urefu wake kadiri ya upana wa nyumba, ulikuwa mikono ishirini, na upana wake mikono ishirini; akaifunikiza kwa dhahabu safi, ya talanta mia sita. 2 Mambo ya Nyakati 3:8

He made the most holy house: the length of it, according to the breadth of the house, was twenty cubits, and the breadth of it twenty cubits; and he overlaid it with fine gold, amounting to six hundred talents.

Na uzani wa misumari ulikuwa shekeli hamsini za dhahabu. Akazifunikiza orofa zake za juu kwa dhahabu. 2 Mambo ya Nyakati 3:9

The weight of the nails was fifty shekels of gold. He overlaid the upper chambers with gold.

Na ndani ya nyumba ya patakatifu pa patakatifu akafanyiza makerubi mawili ya kuchonga; wakayafunikiza kwa dhahabu. 2 Mambo ya Nyakati 3:10

In the most holy house he made two cherubim of image work; and they overlaid them with gold.

Na mabawa ya makerubi hayo urefu wake ulikuwa mikono ishirini; bawa moja mikono mitano, likiufikilia ukuta wa nyumba; na bawa la pili mikono mitano, likishikana na bawa la kerubi la pili. 2 Mambo ya Nyakati 3:11

The wings of the cherubim were twenty cubits long: the wing of the one [cherub] was five cubits, reaching to the wall of the house; and the other wing was [likewise] five cubits, reaching to the wing of the other cherub.

Na bawa la kerubi la pili lilikuwa mikono mitano, likiufikilia ukuta wa nyumba; na bawa la pili mikono mitano, likishikana na bawa la kerubi la kwanza. 2 Mambo ya Nyakati 3:12

The wing of the other cherub was five cubits, reaching to the wall of the house; and the other wing was five cubits [also], joining to the wing of the other cherub.

Yakaenea mabawa ya makerubi hayo mikono ishirini; yakasimama juu ya miguu yao, na nyuso zao ziliielekea nyumba. 2 Mambo ya Nyakati 3:13

The wings of these cherubim spread themselves forth twenty cubits: and they stood on their feet, and their faces were toward the house.

Akalifanya pazia la samawi na urujuani na nyekundu, na kitani safi, akaifanyizia makerubi. 2 Mambo ya Nyakati 3:14

He made the veil of blue, and purple, and crimson, and fine linen, and worked cherubim thereon.

Tena akafanya mbele ya nyumba nguzo mbili za mikono thelathini na tano kwenda juu kwake, na taji iliyokuwa juu yake moja moja ilikuwa mikono mitano. 2 Mambo ya Nyakati 3:15

Also he made before the house two pillars of thirty-five cubits high, and the capital that was on the top of each of them was five cubits.

Akafanya minyororo ndani ya chumba cha ndani, akaiweka juu ya vichwa vya nguzo; akafanya makomamanga mia, akayaweka juu ya hiyo minyororo. 2 Mambo ya Nyakati 3:16

He made chains in the oracle, and put [them] on the tops of the pillars; and he made one hundred pomegranates, and put them on the chains.

Akazisimamisha nguzo hizo mbele ya hekalu, moja upande wa kuume, na ya pili upande wa kushoto; akaliita jina la ile ya kuume Yakini, na jina la ile ya kushoto Boazi. 2 Mambo ya Nyakati 3:17

He set up the pillars before the temple, one on the right hand, and the other on the left; and called the name of that on the right hand Jachin, and the name of that on the left Boaz.