2 Mambo ya Nyakati 26 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Mambo ya Nyakati 26 (Swahili) 2nd Chronicles 26 (English)

Na watu wote wa Yuda wakamtwaa Uzia, naye alikuwa mwenye miaka kumi na sita, wakamfanya awe mfalme mahali pa Amazia babaye. 2 Mambo ya Nyakati 26:1

All the people of Judah took Uzziah, who was sixteen years old, and made him king in the room of his father Amaziah.

Huyo akajenga Elathi, akaurudisha kwa Yuda, baada ya kulala mfalme pamoja na babaze. 2 Mambo ya Nyakati 26:2

He built Eloth, and restored it to Judah, after that the king slept with his fathers.

Uzia alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala; akatawala huko Yerusalemu miaka hamsini na miwili; na jina la mamaye aliitwa Yekolia wa Yerusalemu. 2 Mambo ya Nyakati 26:3

Sixteen years old was Uzziah when he began to reign; and he reigned fifty-two years in Jerusalem: and his mother's name was Jechiliah, of Jerusalem.

Akafanya yaliyo ya adili machoni pa Bwana, sawasawa na yote aliyoyafanya Amazia babaye. 2 Mambo ya Nyakati 26:4

He did that which was right in the eyes of Yahweh, according to all that his father Amaziah had done.

Akajitia nia amtafute Mungu katika siku za Zekaria, aliyekuwa na fahamu katika maono ya Mungu; na muda alipomtafuta Bwana, Mungu alimfanikisha. 2 Mambo ya Nyakati 26:5

He set himself to seek God in the days of Zechariah, who had understanding in the vision of God: and as long as he sought Yahweh, God made him to prosper.

Akatoka akapigana na Wafilisti, akauvunja ukuta wa Gathi, na ukuta wa Yabne, na ukuta wa Ashdodi; akajenga miji katika Ashdodi na katikati ya Wafilisti. 2 Mambo ya Nyakati 26:6

He went forth and warred against the Philistines, and broke down the wall of Gath, and the wall of Jabneh, and the wall of Ashdod; and he built cities in [the country of] Ashdod, and among the Philistines.

Mungu akamsaidia juu ya Wafilisti, na juu ya Waarabu waliokaa Gur-baali, na juu ya Wameuni. 2 Mambo ya Nyakati 26:7

God helped him against the Philistines, and against the Arabians who lived in Gur Baal, and the Meunim.

Na Waamoni wakampa Uzia zawadi; likaenea jina lake mpaka pa kuingilia Misri; kwa kuwa akaongezeka nguvu mno. 2 Mambo ya Nyakati 26:8

The Ammonites gave tribute to Uzziah: and his name spread abroad even to the entrance of Egypt; for he grew exceeding strong.

Tena Uzia akaujengea Yerusalemu minara, penye lango la pembeni, na penye lango la bonde, na ugeukapo ukuta, akaitia nguvu. 2 Mambo ya Nyakati 26:9

Moreover Uzziah built towers in Jerusalem at the corner gate, and at the valley gate, and at the turning [of the wall], and fortified them.

Akajenga minara tena nyikani, akachimba mabirika mengi, maana alikuwa na ng'ombe tele; katika Shefela pia, na katika nchi tambarare; tena alikuwa na wakulima na watunza mizabibu milimani, na katika mashamba ya neema; maana yeye alipenda ukulima. 2 Mambo ya Nyakati 26:10

He built towers in the wilderness, and hewed out many cisterns, for he had much cattle; in the lowland also, and in the plain: [and he had] farmers and vineyard keepers in the mountains and in the fruitful fields; for he loved farming.

Zaidi ya hayo Uzia alikuwa na jeshi la watu wa kupigana, waliokwenda vitani vikosi vikosi, sawasawa na hesabu walivyohesabiwa na Yeieli mwandishi, na Maaseya msimamizi, chini ya mkono wa Hanania, mmojawapo wa maakida wa mfalme. 2 Mambo ya Nyakati 26:11

Moreover Uzziah had an army of fighting men, who went out to war by bands, according to the number of their reckoning made by Jeiel the scribe and Maaseiah the officer, under the hand of Hananiah, one of the king's captains.

Hesabu yote ya wakuu wa nyumba za mababa, watu mashujaa, ilikuwa elfu mbili na mia sita. 2 Mambo ya Nyakati 26:12

The whole number of the heads of fathers' [houses], even the mighty men of valor, was two thousand and six hundred.

Na chini ya mkono wao kulikuwa na jeshi la askari, mia tatu na saba elfu, na mia tano, ambao walipigana vita kwa nguvu nyingi, kumsaidia mfalme juu ya adui. 2 Mambo ya Nyakati 26:13

Under their hand was an army, three hundred thousand and seven thousand and five hundred, who made war with mighty power, to help the king against the enemy.

Uzia akawafanyizia jeshi lote ngao na mikuki, na chapeo, na deraya za madini, na nyuta, na mawe ya kupiga kwa teo. 2 Mambo ya Nyakati 26:14

Uzziah prepared for them, even for all the host, shields, and spears, and helmets, and coats of mail, and bows, and stones for slinging.

Akafanya katika Yerusalemu mitambo ya vita, iliyobuniwa na watu wastadi, iwekwe juu ya minara na juu ya buruji, ili kutupa mishale na mawe makubwa. Jina lake likaenea mbali sana; kwa kuwa alisaidiwa mno ajabu, hata akapata nguvu. 2 Mambo ya Nyakati 26:15

He made in Jerusalem engines, invented by skillful men, to be on the towers and on the battlements, with which to shoot arrows and great stones. His name spread far abroad; for he was marvelously helped, until he was strong.

Lakini alipokuwa na nguvu, moyo wake ulitukuka, hata akafanya maovu, akamwasi Bwana, Mungu wake; kwani aliingia hekaluni mwa Bwana, ili afukize uvumba juu ya madhabahu ya kufukizia. 2 Mambo ya Nyakati 26:16

But when he was strong, his heart was lifted up, so that he did corruptly, and he trespassed against Yahweh his God; for he went into the temple of Yahweh to burn incense on the altar of incense.

Azaria kuhani akaingia nyuma yake, na pamoja naye makuhani themanini wa Bwana, mashujaa; 2 Mambo ya Nyakati 26:17

Azariah the priest went in after him, and with him eighty priests of Yahweh, who were valiant men:

wakamzuia Uzia mfalme, wakamwambia, Si haki yako, Uzia, kumfukizia Bwana uvumba, ila ni haki ya makuhani wana wa Haruni, waliofanywa wakfu, ili wafukize uvumba; toka katika patakatifu; kwa kuwa umekosa; wala haitakuwa kwa heshima yako kutoka kwa Bwana, Mungu. 2 Mambo ya Nyakati 26:18

and they withstood Uzziah the king, and said to him, It pertains not to you, Uzziah, to burn incense to Yahweh, but to the priests the sons of Aaron, who are consecrated to burn incense: go out of the sanctuary; for you have trespassed; neither shall it be for your honor from Yahweh God.

Akaghadhibika Uzia; naye alikuwa na chetezo mkononi cha kufukizia uvumba; naye hapo alipowaghadhibikia makuhani, ukamtokea ukoma katika paji la uso wake mbele ya makuhani nyumbani mwa Bwana karibu na madhabahu ya kufukizia. 2 Mambo ya Nyakati 26:19

Then Uzziah was angry; and he had a censer in his hand to burn incense; and while he was angry with the priests, the leprosy broke forth in his forehead before the priests in the house of Yahweh, beside the altar of incense.

Azaria kuhani mkuu na makuhani wote wakamtazama, na angalia, alikuwa na ukoma pajini mwa uso, wakamtoa humo upesi; hata na yeye mwenyewe akafanya haraka kutoka, kwa sababu Bwana amempiga. 2 Mambo ya Nyakati 26:20

Azariah the chief priest, and all the priests, looked on him, and, behold, he was leprous in his forehead, and they thrust him out quickly from there; yes, himself hurried also to go out, because Yahweh had struck him.

Uzia mfalme akawa na ukoma hata siku ya kufa kwake, akakaa katika nyumba ya pekee, kwa kuwa ni mwenye ukoma; maana alitengwa na nyumba ya Bwana; na Yothamu mwanawe alikuwa juu ya nyumba ya mfalme, akiwahukumu watu wa nchi. 2 Mambo ya Nyakati 26:21

Uzziah the king was a leper to the day of his death, and lived in a separate house, being a leper; for he was cut off from the house of Yahweh: and Jotham his son was over the king's house, judging the people of the land.

Basi mambo yote ya Uzia yaliyosalia, ya kwanza na ya mwisho, aliyaandika Isaya nabii, mwana wa Amozi. 2 Mambo ya Nyakati 26:22

Now the rest of the acts of Uzziah, first and last, did Isaiah the prophet, the son of Amoz, write.

Basi Uzia akalala na babaze; wakamzika pamoja na babaze katika konde la kuzikia la wafalme; kwa kuwa walisema, Huyu ni mwenye ukoma. Na Yothamu mwanawe akatawala mahali pake

2 Mambo ya Nyakati 26:23

So Uzziah slept with his fathers; and they buried him with his fathers in the field of burial which belonged to the kings; for they said, He is a leper: and Jotham his son reigned in his place.