2 Mambo ya Nyakati 22 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Mambo ya Nyakati 22 (Swahili) 2nd Chronicles 22 (English)

Nao wenyeji wa Yerusalemu walimfanya Ahazia mwanawe mdogo awe mfalme mahali pake; maana wakubwa wote wamekwisha kuuawa na kikosi cha watu waliokuja matuoni pamoja na Waarabu. Hivyo akatawala Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda. 2 Mambo ya Nyakati 22:1

The inhabitants of Jerusalem made Ahaziah his youngest son king in his place; for the band of men who came with the Arabians to the camp had slain all the eldest. So Ahaziah the son of Jehoram king of Judah reigned.

Ahazia alikuwa na umri wa miaka arobaini na miwili alipoanza kutawala; akatawala mwaka mmoja huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Athalia binti Omri. 2 Mambo ya Nyakati 22:2

Forty-two years old was Ahaziah when he began to reign; and he reigned one year in Jerusalem: and his mother's name was Athaliah the daughter of Omri.

Yeye naye akaziendea njia za nyumba ya Ahabu; kwa kuwa mamaye alikuwa mshauri wake katika kufanya maovu. 2 Mambo ya Nyakati 22:3

He also walked in the ways of the house of Ahab; for his mother was his counselor to do wickedly.

Akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana kama nyumba ya Ahabu; kwa kuwa hao walikuwa washauri wake, alipokwisha kufa babaye, hata aangamie. 2 Mambo ya Nyakati 22:4

He did that which was evil in the sight of Yahweh, as did the house of Ahab; for they were his counselors after the death of his father, to his destruction.

Naye akaenda kwa mashauri yao, akafuatana na Yoramu mwana wa Ahabu mfalme wa Israeli ili kupigana na Hazaeli mfalme wa Shamu huko Ramoth-Gileadi;nao Washami wakamjeruhi Yoramu. 2 Mambo ya Nyakati 22:5

He walked also after their counsel, and went with Jehoram the son of Ahab king of Israel to war against Hazael king of Syria at Ramoth-gilead: and the Syrians wounded Joram.

Akarudi Yezreeli ili aponye jeraha walizomjeruhi huko Rama, alipopigana na Hazaeli mfalme wa Shamu. Naye Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda ,akashuka amtazame Yoramu mwana wa Ahabu,katika Yezreeli,kwa sababu alikuwa hawezi. 2 Mambo ya Nyakati 22:6

He returned to be healed in Jezreel of the wounds which they had given him at Ramah, when he fought against Hazael king of Syria. Azariah the son of Jehoram king of Judah went down to see Jehoram the son of Ahab in Jezreel, because he was sick.

Basi kuangamia kwake Ahazia kulitokana na Mungu, kwa vile alivyomwendea Yoramu; kwa kuwa alipofika, akatoka pamoja na Yoramu juu ya Yehu mwana wa Nimshi, ambaye Bwana alimtia mafuta ili awakatilie mbali nyumba ya Ahabu. 2 Mambo ya Nyakati 22:7

Now the destruction of Ahaziah was of God, in that he went to Joram: for when he was come, he went out with Jehoram against Jehu the son of Nimshi, whom Yahweh had anointed to cut off the house of Ahab.

Ikawa, Yehu alipokuwa akiwafanyia hukumu nyumba ya Ahabu, aliwakuta wakuu wa Yuda, na wana wa nduguze Ahazia, wakimtumikia Ahazia, akawaua. 2 Mambo ya Nyakati 22:8

It happened, when Jehu was executing judgment on the house of Ahab, that he found the princes of Judah, and the sons of the brothers of Ahaziah, ministering to Ahaziah, and killed them.

Akamtafuta Ahazia, wakamkamata, (naye alikuwa amejificha Samaria,) wakamleta kwa Yehu, wakamwua; wakamzika, kwa maana wakasema, Huyu ni mwana wa Yehoshafati, huyo aliyemtafuta Bwana kwa moyo wake wote. Wala nyumba ya Ahazia hawakuwa na uwezo wa kuushika ufalme. 2 Mambo ya Nyakati 22:9

He sought Ahaziah, and they caught him (now he was hiding in Samaria), and they brought him to Jehu, and killed him; and they buried him, for they said, He is the son of Jehoshaphat, who sought Yahweh with all his heart. The house of Ahaziah had no power to hold the kingdom.

Basi Athalia, mama wa Ahazia, alipoona ya kuwa mwanawe amekufa, akainuka, akawaangamiza wazao wote wa kifalme wa nyumba ya Yuda. 2 Mambo ya Nyakati 22:10

Now when Athaliah the mother of Ahaziah saw that her son was dead, she arose and destroyed all the seed royal of the house of Judah.

Ila Yehosheba, binti mfalme, akamtwaa Yoashi, mwana wa Ahazia, akamwiba miongoni mwa wana wa mfalme waliouawa, akamweka yeye na yaya wake katika chumba cha kulala. Basi Yehosheba, binti mfalme Yehoramu, mkewe Yehoyada kuhani, (naye alikuwa umbu lake Ahazia,) akaficha usoni pa Athalia, asimwue. 2 Mambo ya Nyakati 22:11

But Jehoshabeath, the daughter of the king, took Joash the son of Ahaziah, and stole him away from among the king's sons who were slain, and put him and his nurse in the bedchamber. So Jehoshabeath, the daughter of king Jehoram, the wife of Jehoiada the priest (for she was the sister of Ahaziah), hid him from Athaliah, so that she didn't kill him.

Akawako pamoja nao, amefichwa nyumbani mwa Mungu, miaka sita. Na Athalia akaitawala nchi.

2 Mambo ya Nyakati 22:12

He was with them hid in the house of God six years: and Athaliah reigned over the land.