2 Mambo ya Nyakati 21 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Mambo ya Nyakati 21 (Swahili) 2nd Chronicles 21 (English)

Yehoshafati akalala na babaze, akazikwa pamoja na babaze katika mji wa Daudi; akatawala Yehoramu mwanawe mahali pake. 2 Mambo ya Nyakati 21:1

Jehoshaphat slept with his fathers, and was buried with his fathers in the city of David: and Jehoram his son reigned in his place.

Naye alikuwa na ndugu, wana wa Yehoshafati, Azaria, na Yehieli, na Zekaria, na Azaria, na Mikaeli, na Shefatia; hao wote walikuwa wana wa Yehoshafati mfalme wa Israeli. 2 Mambo ya Nyakati 21:2

He had brothers, the sons of Jehoshaphat: Azariah, and Jehiel, and Zechariah, and Azariah, and Michael, and Shephatiah; all these were the sons of Jehoshaphat king of Israel.

Baba yao akawapa zawadi kubwa, za fedha, na za dhahabu, na za tunu, pamoja na miji yenye maboma katika Yuda; lakini ufalme akampa Yehoramu, kwa sababu alikuwa mzaliwa wa kwanza. 2 Mambo ya Nyakati 21:3

Their father gave them great gifts, of silver, and of gold, and of precious things, with fortified cities in Judah: but the kingdom gave he to Jehoram, because he was the firstborn.

Basi Yehoramu alipoinuliwa juu ya ufalme wa babaye, na kujitia nguvu, akawaua nduguze wote kwa upanga, na baadhi ya wakuu wa Israeli pia. 2 Mambo ya Nyakati 21:4

Now when Jehoram was risen up over the kingdom of his father, and had strengthened himself, he killed all his brothers with the sword, and various also of the princes of Israel.

Yehoramu alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipoanza kutawala, akatawala miaka minane huko Yerusalemu. 2 Mambo ya Nyakati 21:5

Jehoram was thirty-two years old when he began to reign; and he reigned eight years in Jerusalem.

Akaiendea njia ya wafalme wa Israeli, kama walivyofanya nyumba ya Ahabu; kwa kuwa alikuwa amemwoa binti Ahabu; akafanya maovu machoni pa Bwana. 2 Mambo ya Nyakati 21:6

He walked in the way of the kings of Israel, as did the house of Ahab; for he had the daughter of Ahab as wife: and he did that which was evil in the sight of Yahweh.

Walakini Bwana hakupenda kuiharibu nyumba ya Daudi, kwa sababu ya agano alilolifanya na Daudi, na kama alivyomwahidi kuwa atampa taa, yeye na wazao wake siku zote. 2 Mambo ya Nyakati 21:7

However Yahweh would not destroy the house of David, because of the covenant that he had made with David, and as he promised to give a lamp to him and to his children always.

Zamani zake Edomu wakaasi chini ya mkono wa Yuda, wakajifanyia mfalme. 2 Mambo ya Nyakati 21:8

In his days Edom revolted from under the hand of Judah, and made a king over themselves.

Ndipo akavuka Yehoramu na maakida wake, na magari yake yote pamoja naye; akaondoka usiku, akawapiga Waedomi waliomzunguka yeye na hao maakida wa magari. 2 Mambo ya Nyakati 21:9

Then Jehoram passed over with his captains, and all his chariots with him: and he rose up by night, and struck the Edomites who surrounded him, along with the captains of the chariots.

Hivyo Edomu wakaasi chini ya mkono wa Yuda, hata leo; wakaasi na Libna zamani zizo hizo chini ya mkono wake: kwa sababu alikuwa amemwacha Bwana, Mungu wa baba zake. 2 Mambo ya Nyakati 21:10

So Edom revolted from under the hand of Judah to this day: then did Libnah revolt at the same time from under his hand, because he had forsaken Yahweh, the God of his fathers.

Tena ndiye aliyefanya mahali pa juu milimani pa Yuda, na kuwaendesha katika uasherati wenyeji wa Yerusalemu, na kuwakosesha Yuda. 2 Mambo ya Nyakati 21:11

Moreover he made high places in the mountains of Judah, and made the inhabitants of Jerusalem to play the prostitute, and led Judah astray.

Likamjia andiko kutoka kwa Eliya nabii, kusema, Bwana, Mungu wa Daudi baba yako, asema hivi, Kwa sababu hukuziendea njia za Yehoshafati baba yako, wala njia za Asa mfalme wa Yuda; 2 Mambo ya Nyakati 21:12

There came a writing to him from Elijah the prophet, saying, Thus says Yahweh, the God of David your father, Because you have not walked in the ways of Jehoshaphat your father, nor in the ways of Asa king of Judah,

lakini umeiendea njia ya wafalme wa Israeli, ukawaendesha katika uasherati Yuda na wenyeji wa Yerusalemu, kama walivyofanya nyumba ya Ahabu; tena umewaua ndugu zako wa nyumba ya baba yako, waliokuwa wema kuliko wewe; 2 Mambo ya Nyakati 21:13

but have walked in the way of the kings of Israel, and have made Judah and the inhabitants of Jerusalem to play the prostitute, like as the house of Ahab did, and also have slain your brothers of your father's house, who were better than yourself:

tazama, Bwana atawapiga pigo kubwa watu wako, na watoto wako, na wake zako, na mali yako yote; 2 Mambo ya Nyakati 21:14

behold, Yahweh will strike with a great plague your people, and your children, and your wives, and all your substance;

nawe utakuwa na ugonjwa mkuu kwa maradhi ya matumbo, yatakapotokea matumbo yako kwa sababu ya ugonjwa huo siku kwa siku. 2 Mambo ya Nyakati 21:15

and you shall have great sickness by disease of your bowels, until your bowels fall out by reason of the sickness, day by day.

Bwana akawaamsha roho Wafilisti, na Waarabu waliowaelekea Wakushi juu ya Yehoramu, 2 Mambo ya Nyakati 21:16

Yahweh stirred up against Jehoram the spirit of the Philistines, and of the Arabians who are beside the Ethiopians:

nao wakakwea juu ya nchi ya Yuda, wakaipenya, wakaichukua mali yote iliyoonekama nyumbani mwa mfalme, na wanawe pia, na wakeze; asisaziwe mwana hata mmoja, ila Ahazia, aliyekuwa mdogo miongoni mwa wanawe. 2 Mambo ya Nyakati 21:17

and they came up against Judah, and broke into it, and carried away all the substance that was found in the king's house, and his sons also, and his wives; so that there was never a son left him, save Jehoahaz, the youngest of his sons.

Na baada ya hayo yote Bwana akampiga matumbo kwa ugonjwa usioponyeka. 2 Mambo ya Nyakati 21:18

After all this Yahweh struck him in his bowels with an incurable disease.

Ikawa baada ya siku, ikiisha miaka miwili, matumbo yake yakatokea kwa sababu ya ugonjwa wake, akafa akiugua vibaya. Wala watu wake hawakumfukizia mafukizo kama ya baba zake. 2 Mambo ya Nyakati 21:19

It happened, in process of time, at the end of two years, that his bowels fell out by reason of his sickness, and he died of sore diseases. His people made no burning for him, like the burning of his fathers.

Alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipoanza kutawala, akatawala huko Yerusalemu miaka minane; akafariki bila kutamaniwa; wakamzika mjini mwa Daudi, ila si katika makaburi ya wafalme. 2 Mambo ya Nyakati 21:20

Thirty-two years old was he when he began to reign, and he reigned in Jerusalem eight years: and he departed without being desired; and they buried him in the city of David, but not in the tombs of the kings.