2 Mambo ya Nyakati 20 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Mambo ya Nyakati 20 (Swahili) 2nd Chronicles 20 (English)

Ikawa baadaye, wana wa Moabu, na wana wa Amoni, na pamoja nao baadhi ya Wameuni, wakaja juu ya Yehoshafati vitani. 2 Mambo ya Nyakati 20:1

It happened after this, that the children of Moab, and the children of Ammon, and with them some of the Ammonites, came against Jehoshaphat to battle.

Wakaja watu waliomwambia Yehoshafati, wakisema, Wanakuja jamii kubwa juu yako watokao Shamu toka ng'ambo ya bahari; na tazama, wako katika Hasason-tamari (ndio En-gedi). 2 Mambo ya Nyakati 20:2

Then there came some who told Jehoshaphat, saying, There comes a great multitude against you from beyond the sea from Syria; and, behold, they are in Hazazon Tamar (the same is En Gedi).

Yehoshafati akaogopa, akauelekeza uso wake amtafute Bwana; akatangaza mbiu ya watu kufunga katika Yuda yote. 2 Mambo ya Nyakati 20:3

Jehoshaphat feared, and set himself to seek to Yahweh; and he proclaimed a fast throughout all Judah.

Yuda wakakusanyika pamoja ili wamtafute Bwana; hata kutoka miji yote ya Yuda wakaja kumtafuta Bwana. 2 Mambo ya Nyakati 20:4

Judah gathered themselves together, to seek [help] of Yahweh: even out of all the cities of Judah they came to seek Yahweh.

Yehoshafati akasimama kati ya kusanyiko la Yuda na Yerusalemu, nyumbani mwa Bwana, mbele ya ua mpya; 2 Mambo ya Nyakati 20:5

Jehoshaphat stood in the assembly of Judah and Jerusalem, in the house of Yahweh, before the new court;

akasema, Ee Bwana, Mungu wa baba zetu, si wewe uliye Mungu mbinguni? Tena si wewe utawalaye falme zote za mataifa? Na mkononi mwako mna uweza na nguvu, asiweze mtu ye yote kusimama kinyume chako. 2 Mambo ya Nyakati 20:6

and he said, Yahweh, the God of our fathers, aren't you God in heaven? and aren't you ruler over all the kingdoms of the nations? and in your hand is power and might, so that none is able to withstand you.

Si wewe, Ee Mungu wetu, uliyewafukuza wenyeji wa nchi hii mbele ya watu wako Israeli, ukawapa wazao wa Ibrahimu rafiki yako hata milele? 2 Mambo ya Nyakati 20:7

Did not you, our God, drive out the inhabitants of this land before your people Israel, and give it to the seed of Abraham your friend forever?

Nao walikaa humo, wamekujengea patakatifu pa jina lako humo, wakisema, 2 Mambo ya Nyakati 20:8

They lived therein, and have built you a sanctuary therein for your name, saying,

Yakitujia mabaya, upanga, hukumu, au tauni, au njaa, tutasimama mbele ya nyumba hii, na mbele zako, (maana jina lako limo katika nyumba hii), na kukulilia katika shida yetu, nawe utasikia na kuokoa. 2 Mambo ya Nyakati 20:9

If evil come on us, the sword, judgment, or pestilence, or famine, we will stand before this house, and before you, (for your name is in this house), and cry to you in our affliction, and you will hear and save.

Na sasa, tazama, wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, ambao hukuwaacha Israeli waingie katika nchi yao, walipotoka nchi ya Misri; lakini wakawageukia mbali, wasiwaharibu; 2 Mambo ya Nyakati 20:10

Now, behold, the children of Ammon and Moab and Mount Seir, whom you would not let Israel invade, when they came out of the land of Egypt, but they turned aside from them, and didn't destroy them;

tazama, jinsi wanavyotulipa, wakija kututupa toka milki yako, uliyoturithisha. 2 Mambo ya Nyakati 20:11

behold, how they reward us, to come to cast us out of your possession, which you have given us to inherit.

Ee Mungu wetu, je! Hutawahukumu? Maana sisi hatuna uwezo juu ya jamii kubwa hii, wanaotujia juu yetu; wala hatujui tufanyeje; lakini macho yetu yatazama kwako. 2 Mambo ya Nyakati 20:12

Our God, will you not judge them? for we have no might against this great company that comes against us; neither know we what to do: but out eyes are on you.

Wakasimama Yuda wote mbele za Bwana, pamoja na wadogo wao, na wake zao, na watoto wao. 2 Mambo ya Nyakati 20:13

All Judah stood before Yahweh, with their little ones, their wives, and their children.

Ndipo Yahazieli mwana wa Zekaria, mwana wa Benaya, mwana wa Yeieli, mwana wa Matania, Mlawi, wa wana wa Asafu, akajiliwa na roho ya Bwana, katikati ya kusanyiko; 2 Mambo ya Nyakati 20:14

Then on Jahaziel the son of Zechariah, the son of Benaiah, the son of Jeiel, the son of Mattaniah, the Levite, of the sons of Asaph, came the Spirit of Yahweh in the midst of the assembly;

akasema, Sikieni, Yuda wote, nanyi mkaao Yerusalemu, na wewe mfalme Yehoshafati; Bwana awaambia hivi, Msiogope, wala msifadhaike kwa ajili ya jeshi kubwa hili; kwani vita si yenu bali ni ya Mungu. 2 Mambo ya Nyakati 20:15

and he said, Listen you, all Judah, and you inhabitants of Jerusalem, and you king Jehoshaphat: Thus says Yahweh to you, Don't be afraid you, neither be dismayed by reason of this great multitude; for the battle is not yours, but God's.

Kesho shukeni juu yao; tazameni, wanakwea kwa kupandia Sisi; nanyi mtawapata penye mwisho wa bonde, mbele ya jangwa la Yerueli. 2 Mambo ya Nyakati 20:16

Tomorrow go you down against them: behold, they come up by the ascent of Ziz; and you shall find them at the end of the valley, before the wilderness of Jeruel.

Hamtahitaji kupigana vita, jipangeni, simameni, mkauone wokovu wa Bwana ulio pamoja nanyi, enyi Yuda na Yerusalemu; msiogope, wala msifadhaike; kesho tokeni juu yao; kwa kuwa Bwana yu pamoja nanyi. 2 Mambo ya Nyakati 20:17

You shall not need to fight in this [battle]: set yourselves, stand you still, and see the salvation of Yahweh with you, O Judah and Jerusalem; don't be afraid, nor be dismayed: tomorrow go out against them: for Yahweh is with you.

Yehoshafati akainama kichwa, kifulifuli; wakaanguka mbele za Bwana Yuda wote na wakaao Yerusalemu, wakimsujudia Bwana. 2 Mambo ya Nyakati 20:18

Jehoshaphat bowed his head with his face to the ground; and all Judah and the inhabitants of Jerusalem fell down before Yahweh, worshipping Yahweh.

Na Walawi, wa wana wa Wakohathi na wa wana wa Wakorahi, wakasimama ili wamsifu Bwana, Mungu wa Israeli, kwa sauti kuu sana. 2 Mambo ya Nyakati 20:19

The Levites, of the children of the Kohathites and of the children of the Korahites, stood up to praise Yahweh, the God of Israel, with an exceeding loud voice.

Wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda nje katika jangwa la Tekoa; nao walipokuwa wakitoka, Yehoshafati akasimama, akasema, Nisikieni, enyi Yuda nanyi wenyeji wa Yerusalemu; mwaminini Bwana, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa. 2 Mambo ya Nyakati 20:20

They rose early in the morning, and went forth into the wilderness of Tekoa: and as they went forth, Jehoshaphat stood and said, Hear me, Judah, and you inhabitants of Jerusalem: believe in Yahweh your God, so shall you be established; believe his prophets, so shall you prosper.

Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia Bwana, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya jeshi, na kusema, Mshukuruni Bwana; kwa maana fadhili zake ni za milele. 2 Mambo ya Nyakati 20:21

When he had taken counsel with the people, he appointed those who should sing to Yahweh, and give praise in holy array, as they went out before the army, and say, Give thanks to Yahweh; for his loving kindness endures forever.

Nao walipoanza kuimba na kusifu, Bwana akaweka waviziao juu ya wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, waliokuja juu ya Yuda; nao wakapigwa. 2 Mambo ya Nyakati 20:22

When they began to sing and to praise, Yahweh set liers-in-wait against the children of Ammon, Moab, and Mount Seir, who had come against Judah; and they were struck.

Kwani wana wa Amoni na wa Moabu waliwaondokea wenyeji wa mlima Seiri kuwaulia mbali na kuwaharibu; nao walipokwisha kuwakomesha hao wakaao Seiri, wakajitia kuharibu kila mtu mwenziwe. 2 Mambo ya Nyakati 20:23

For the children of Ammon and Moab stood up against the inhabitants of Mount Seir, utterly to kill and destroy them: and when they had made an end of the inhabitants of Seir, everyone helped to destroy another.

Hata Yuda walipofika mnara wa kulindia wa jangwani, wakalitazama hilo jeshi; nao, angalia, walikuwa maiti walioanguka nchi, wala hapana aliyeokoka. 2 Mambo ya Nyakati 20:24

When Judah came to the watch-tower of the wilderness, they looked at the multitude; and, behold, they were dead bodies fallen to the earth, and there were none who escaped.

Nao Yehoshafati na watu wake walipokuja kuchukua nyara zao, wakaona kati yao wingi wa mali, na mavazi, na johari za thamani, walivyojivulia, zaidi kuliko wawezavyo kuchukua; wakawa siku tatu katika kuteka nyara, maana zilikuwa nyingi sana. 2 Mambo ya Nyakati 20:25

When Jehoshaphat and his people came to take the spoil of them, they found among them in abundance both riches and dead bodies, and precious jewels, which they stripped off for themselves, more than they could carry away: and they were three days in taking the spoil, it was so much.

Hata siku ya nne wakakusanyika katika bonde la Baraka; maana ndipo walipombarikia Bwana; kwa hiyo jina lake mahali pale pakaitwa Bonde la Baraka hata leo. 2 Mambo ya Nyakati 20:26

On the fourth day they assembled themselves in the valley of Beracah; for there they blessed Yahweh: therefore the name of that place was called The valley of Beracah to this day.

Kisha wakarudi, kila mtu wa Yuda na Yerusalemu, na Yehoshafati mbele yao, ili kuurudia Yerusalemu kwa furaha; kwa kuwa Bwana amewafurahisha juu ya adui zao. 2 Mambo ya Nyakati 20:27

Then they returned, every man of Judah and Jerusalem, and Jehoshaphat in the forefront of them, to go again to Jerusalem with joy; for Yahweh had made them to rejoice over their enemies.

Wakafika Yerusalemu wenye vinanda vinubi na mapanda kwenda nyumbani kwa Bwana. 2 Mambo ya Nyakati 20:28

They came to Jerusalem with psalteries and harps and trumpets to the house of Yahweh.

Ikawa hofu ya Mungu juu ya falme zote za nchi, waliposikia ya kuwa Bwana amepigana juu ya adui za Israeli. 2 Mambo ya Nyakati 20:29

The fear of God was on all the kingdoms of the countries, when they heard that Yahweh fought against the enemies of Israel.

Basi ukatulia ufalme wake Yehoshafati; kwa sababu Mungu wake alimstarehesha pande zote. 2 Mambo ya Nyakati 20:30

So the realm of Jehoshaphat was quiet; for his God gave him rest round about.

Yehoshafati akatawala juu ya Yuda; alikuwa na umri wa miaka thelathini na mitano alipoanza kutawala, akatawala miaka ishirini na mitano huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Azuba binti Shilhi. 2 Mambo ya Nyakati 20:31

Jehoshaphat reigned over Judah: he was thirty-five years old when he began to reign; and he reigned twenty-five years in Jerusalem: and his mother's name was Azubah the daughter of Shilhi.

Akaiendea njia ya Asa babaye, wala hakuiacha, akifanya yaliyo mema machoni pa Bwana. 2 Mambo ya Nyakati 20:32

He walked in the way of Asa his father, and didn't turn aside from it, doing that which was right in the eyes of Yahweh.

Lakini mahali pa juu hapakuondolewa; wala mioyo ya watu bado haijakazwa kwa Mungu wa baba zao. 2 Mambo ya Nyakati 20:33

However the high places were not taken away; neither as yet had the people set their hearts to the God of their fathers.

Na mambo yote ya Yehoshafati yaliyosalia, ya kwanza na ya mwisho, angalia, yameandikwa katika tarehe ya Yehu mwana wa Hanani, iliyotiwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli. 2 Mambo ya Nyakati 20:34

Now the rest of the acts of Jehoshaphat, first and last, behold, they are written in the history of Jehu the son of Hanani, which is inserted in the book of the kings of Israel.

Baada ya hayo Yehoshafati mfalme wa Yuda akapatana na Ahazia mfalme wa Israeli; naye huyo ndiye aliyefanya mabaya mno; 2 Mambo ya Nyakati 20:35

After this did Jehoshaphat king of Judah join himself with Ahaziah king of Israel; the same did very wickedly:

akapatana naye kufanya merikebu za kuendea Tarshishi; wakazifanya merikebu zile huko Esion-geberi. 2 Mambo ya Nyakati 20:36

and he joined himself with him to make ships to go to Tarshish; and they made the ships in Ezion Geber.

Ndipo Eliezeri mwana wa Dodavahu wa Maresha akatoa unabii juu ya Yehoshafati, akasema, Kwa sababu umepatana na Ahazia, Bwana amezivunja-vunja kazi zako. Zikavunjika merikebu, zisiweze kufika Tarshishi.

2 Mambo ya Nyakati 20:37

Then Eliezer the son of Dodavahu of Mareshah prophesied against Jehoshaphat, saying, Because you have joined yourself with Ahaziah, Yahweh has destroyed your works. The ships were broken, so that they were not able to go to Tarshish.