2 Mambo ya Nyakati 18 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Mambo ya Nyakati 18 (Swahili) 2nd Chronicles 18 (English)

Basi, Yehoshafati alikuwa na mali na heshima tele, tena akafanya ujamaa na Ahabu. 2 Mambo ya Nyakati 18:1

Now Jehoshaphat had riches and honor in abundance; and he joined affinity with Ahab.

Hata baada ya miaka kadha wa kadha akamshukia Ahabu huko Samaria. Ahabu akamchinjia kondoo na ng'ombe tele, yeye na watu waliokuwa pamoja naye, akamshawishi ili apande pamoja naye waende Ramoth-gileadi. 2 Mambo ya Nyakati 18:2

After certain years he went down to Ahab to Samaria. Ahab killed sheep and oxen for him in abundance, and for the people who were with him, and moved him to go up [with him] to Ramoth-gilead.

Ahabu, mfalme wa Israeli, akamwambia Yehoshafati, mfalme wa Yuda, Je! Utakwenda nami mpaka Ramoth-gileadi? Akamjibu, Mimi ni kama wewe, na watu wangu kama watu wako; nasi tutakuwa pamoja nawe vitani. 2 Mambo ya Nyakati 18:3

Ahab king of Israel said to Jehoshaphat king of Judah, Will you go with me to Ramoth-gilead? He answered him, I am as you are, and my people as your people; and [we will be] with you in the war.

Yehoshafati akamwambia mfalme wa Israeli, Uulize leo, nakusihi, kwa neno la Bwana. 2 Mambo ya Nyakati 18:4

Jehoshaphat said to the king of Israel, Please inquire first for the word of Yahweh.

Ndipo mfalme wa Israeli akawakusanya manabii, watu mia nne; akawaambia, Je! Tuende Ramoth-gileadi vitani, au niache? Wakasema, Kwea; kwa kuwa Mungu atautia mkononi mwa mfalme. 2 Mambo ya Nyakati 18:5

Then the king of Israel gathered the prophets together, four hundred men, and said to them, Shall we go to Ramoth-gilead to battle, or shall I forbear? They said, Go up; for God will deliver it into the hand of the king.

Lakini Yehoshafati akasema, Je! Hayupo hapa nabii wa Bwana tena, ili tumwulize yeye? 2 Mambo ya Nyakati 18:6

But Jehoshaphat said, Isn't there here a prophet of Yahweh besides, that we may inquire of him?

Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, Yupo mtu mmoja, ambaye tungeweza kumwuliza Bwana kwa yeye; lakini namchukia; kwa sababu hanibashirii mema kamwe, ila siku zote mabaya; naye ndiye Mikaya mwana wa Imla. Yehoshafati akasema, La! Mfalme asiseme hivi. 2 Mambo ya Nyakati 18:7

The king of Israel said to Jehoshaphat, There is yet one man by whom we may inquire of Yahweh: but I hate him; for he never prophesies good concerning me, but always evil: the same is Micaiah the son of Imla. Jehoshaphat said, Don't let the king say so.

Ndipo mfalme wa Israeli akamwita akida mmoja, akasema, Mlete hima Mikaya mwana wa Imla. 2 Mambo ya Nyakati 18:8

Then the king of Israel called an officer, and said, Get quickly Micaiah the son of Imla.

Basi, mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda walikuwa wamekaa kila mtu katika kiti chake cha enzi, wamevaa mavazi yao, wakikaa penye sakafu pa kuingilia lango la Samaria; nao manabii wote wakafanya unabii mbele yao. 2 Mambo ya Nyakati 18:9

Now the king of Israel and Jehoshaphat the king of Judah sat each on his throne, arrayed in their robes, and they were sitting in an open place at the entrance of the gate of Samaria; and all the prophets were prophesying before them.

Na Zedekia mwana wa Kenaana akajifanyia pembe za chuma, akasema, Bwana asema hivi, Kwa hizi utawasukuma Washami, hata watakapoangamia. 2 Mambo ya Nyakati 18:10

Zedekiah the son of Chenaanah made him horns of iron, and said, Thus says Yahweh, With these shall you push the Syrians, until they be consumed.

Na manabii wote wakatoa unabii huo, wakisema, Kwea Ramoth-gileadi, ukafanikiwe, kwa kuwa Bwana atautia mkononi mwa mfalme. 2 Mambo ya Nyakati 18:11

All the prophets prophesied so, saying, Go up to Ramoth-gilead, and prosper; for Yahweh will deliver it into the hand of the king.

Na yule mjumbe, aliyekwenda kumwita Mikaya, akamwambia, akasema, Angalia, maneno ya manabii kwa kinywa kimoja yasema mema kwa mfalme; neno lako basi na liwe kama mojawapo lao, ukaseme mema. 2 Mambo ya Nyakati 18:12

The messenger who went to call Micaiah spoke to him, saying, Behold, the words of the prophets [declare] good to the king with one mouth: let your word therefore, Please be like one of theirs, and speak you good.

Mikaya akasema, Kama aishivyo Bwana, neno lile atakalolinena Mungu wangu, ndilo nitakalolinena. 2 Mambo ya Nyakati 18:13

Micaiah said, As Yahweh lives, what my God says, that will I speak.

Na alipokuja kwa mfalme, mfalme akamwambia, Je! Mikaya, tuende Ramoth-gileadi vitani, au niache? Akasema, Kweeni, mkafanikiwe; nao watatiwa mikononi mwenu. 2 Mambo ya Nyakati 18:14

When he was come to the king, the king said to him, Micaiah, shall we go to Ramoth-gilead to battle, or shall I forbear? He said, Go up, and prosper; and they shall be delivered into your hand.

Mfalme akamwambia, Mara ngapi nikuapishe, usiniambie neno ila yaliyo kweli, kwa jina la Bwana? 2 Mambo ya Nyakati 18:15

The king said to him, How many times shall I adjure you that you speak to me nothing but the truth in the name of Yahweh?

Akasema, Naliwaona Waisraeli wote wametawanyika milimani, kama kondoo wasio na mchungaji; Bwana akasema, Hawa hawana bwana; na warudi kila mtu nyumbani kwake kwa amani. 2 Mambo ya Nyakati 18:16

He said, I saw all Israel scattered on the mountains, as sheep that have no shepherd: and Yahweh said, These have no master; let them return every man to his house in peace.

Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, Je! Sikukuambia, hatanibashiria mema, ila mabaya? 2 Mambo ya Nyakati 18:17

The king of Israel said to Jehoshaphat, Didn't I tell you that he would not prophesy good concerning me, but evil?

Mikaya akasema, Sikieni basi neno la Bwana; Nalimwona Bwana ameketi katika kiti chake cha enzi na jeshi lote la mbinguni wamesimama mkono wake wa kuume na wa kushoto. 2 Mambo ya Nyakati 18:18

[Micaiah] said, Therefore hear you the word of Yahweh: I saw Yahweh sitting on his throne, and all the host of heaven standing on his right hand and on his left.

Bwana akasema, Ni nani atakayemdanganya Ahabu mfalme wa Israeli, ili akwee Ramoth-gileadi akaanguke? Basi huyu akasema hivi; na huyu hivi. 2 Mambo ya Nyakati 18:19

Yahweh said, Who shall entice Ahab king of Israel, that he may go up and fall at Ramoth-gilead? One spoke saying after this manner, and another saying after that manner.

Akatoka pepo, akasimama mbele za Bwana, akasema, Mimi nitamdanganya. Bwana akamwambia, Jinsi gani? 2 Mambo ya Nyakati 18:20

There came forth a spirit, and stood before Yahweh, and said, I will entice him. Yahweh said to him, 'How?'

Akasema, Nitaondoka, na kuwa pepo wa uongo vinywani mwa manabii wake wote. Akasema, Utamdanganya, na kudiriki pia; ondoka, ukafanye hivyo. 2 Mambo ya Nyakati 18:21

He said, 'I will go forth, and will be a lying spirit in the mouth of all his prophets.' He said, 'You shall entice him, and shall prevail also: go forth, and do so.'

Basi sasa, angalia, Bwana ametia pepo wa uongo vinywani mwa manabii wako hawa; naye Bwana amenena mabaya juu yako. 2 Mambo ya Nyakati 18:22

Now therefore, behold, Yahweh has put a lying spirit in the mouth of these your prophets; and Yahweh has spoken evil concerning you.

Ndipo akakaribia Zedekia mwana wa Kenaana, akampiga Mikaya kofi la shavu, akasema, Alitokaje kwangu roho ya Bwana ili aseme na wewe? 2 Mambo ya Nyakati 18:23

Then Zedekiah the son of Chenaanah came near, and struck Micaiah on the cheek, and said, Which way went the Spirit of Yahweh from me to speak to you?

Mikaya akasema, Angalia utaona siku ile, utakapoingia katika chumba cha ndani ili ujifiche. 2 Mambo ya Nyakati 18:24

Micaiah said, Behold, you shall see on that day, when you shall go into an inner chamber to hide yourself.

Mfalme wa Israeli akasema, Mchukueni Mikaya mkamrudishe kwa Amoni mkuu wa mji, na kwa Yoashi mwana wa mfalme; 2 Mambo ya Nyakati 18:25

The king of Israel said, Take Micaiah, and carry him back to Amon the governor of the city, and to Joash the king's son;

mkaseme, Mfalme asema hivi, Mtieni huyu gerezani, mkamlishe chakula cha shida, na maji ya shida, hata nitakaporudi kwa amani. 2 Mambo ya Nyakati 18:26

and say, Thus says the king, Put this fellow in the prison, and feed him with bread of affliction and with water of affliction, until I return in peace.

Mikaya akasema, Ukirudi kabisa kwa amani, Bwana hakusema kwa mimi. Akasema, Sikieni, enyi watu wote. 2 Mambo ya Nyakati 18:27

Micaiah said, If you return at all in peace, Yahweh has not spoken by me. He said, Hear, you peoples, all of you.

Basi mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda wakakwea mpaka Ramoth-gileadi. 2 Mambo ya Nyakati 18:28

So the king of Israel and Jehoshaphat the king of Judah went up to Ramoth-gilead.

Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, Nitajibadilisha, na kuingia vitani; lakini wewe uvae mavazi yako. Mfalme wa Israeli akajibadilisha; nao wakaingia vitani. 2 Mambo ya Nyakati 18:29

The king of Israel said to Jehoshaphat, I will disguise myself, and go into the battle; but put you on your robes. So the king of Israel disguised himself; and they went into the battle.

Basi mfalme wa Shamu alikuwa amewaamuru maakida wa magari yake, akisema, Msipigane na mdogo wala mkuu, ila na mfalme wa Israeli peke yake. 2 Mambo ya Nyakati 18:30

Now the king of Syria had commanded the captains of his chariots, saying, Fight neither with small nor great, save only with the king of Israel.

Ikawa maakida wa magari walipomwona Yehoshafati, wakasema, Mfalme wa Israeli ni huyu. Basi wakamgeukia ili wapigane naye; lakini Yehoshafati akalia, na Bwana akamsaidia; Mungu akawafarakisha kwake. 2 Mambo ya Nyakati 18:31

It happened, when the captains of the chariots saw Jehoshaphat, that they said, It is the king of Israel. Therefore they turned about to fight against him: but Jehoshaphat cried out, and Yahweh helped him; and God moved them [to depart] from him.

Ikawa, maakida wa magari walipoona ya kuwa siye mfalme wa Israeli, wakageuka nyuma wasimfuate. 2 Mambo ya Nyakati 18:32

It happened, when the captains of the chariots saw that it was not the king of Israel, that they turned back from pursuing him.

Na mtu mmoja akavuta upinde kwa kubahatisha, akampiga mfalme wa Israeli mahali pa kuungana mavazi yake ya chuma; kwa hiyo akamwambia mwendesha gari, Geuza mkono wako, unichukue kutoka katika majeshi; kwa kuwa nimejeruhiwa sana. 2 Mambo ya Nyakati 18:33

A certain man drew his bow at a venture, and struck the king of Israel between the joints of the armor. Therefore he said to the driver of the chariot, Turn your hand, and carry me out of the host; for I am sore wounded.

Pigano likazidi siku ile; lakini mfalme wa Israeli akajitegemeza garini juu ya Washami hata jioni; akafa kama wakati wa kuchwa kwa jua. 2 Mambo ya Nyakati 18:34

The battle increased that day: however the king of Israel stayed himself up in his chariot against the Syrians until the even; and about the time of the going down of the sun he died.