2 Mambo ya Nyakati 17 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Mambo ya Nyakati 17 (Swahili) 2nd Chronicles 17 (English)

Na Yehoshafati mwanawe akatawala mahali pake, akajitia nguvu juu ya Israeli. 2 Mambo ya Nyakati 17:1

Jehoshaphat his son reigned in his place, and strengthened himself against Israel.

Akaweka jeshi katika miji yote yenye maboma ya Yuda, akatia na askari walinzi katika nchi ya Yuda, na katika miji ya Efraimu, aliyoitwaa Asa babaye. 2 Mambo ya Nyakati 17:2

He placed forces in all the fortified cities of Judah, and set garrisons in the land of Judah, and in the cities of Ephraim, which Asa his father had taken.

Naye Bwana alikuwa pamoja na Yehoshafati, kwa kuwa alikwenda katika njia za kwanza za Daudi babaye, asiyatafute mabaali; 2 Mambo ya Nyakati 17:3

Yahweh was with Jehoshaphat, because he walked in the first ways of his father David, and didn't seek the Baals,

lakini alimtafuta Mungu wa baba yake, akaenda katika amri zake, wala si katika matendo ya Israeli. 2 Mambo ya Nyakati 17:4

but sought to the God of his father, and walked in his commandments, and not after the doings of Israel.

Kwa hiyo Bwana akauthibitisha ufalme mkononi mwake; Yehoshafati akaletewa zawadi na Yuda wote; basi akawa na mali na heshima tele. 2 Mambo ya Nyakati 17:5

Therefore Yahweh established the kingdom in his hand; and all Judah brought to Jehoshaphat tribute; and he had riches and honor in abundance.

Ukainuliwa moyo wake katika njia za Bwana; na zaidi ya hayo akapaondoa mahali pa juu, na maashera, katika Yuda. 2 Mambo ya Nyakati 17:6

His heart was lifted up in the ways of Yahweh: and furthermore he took away the high places and the Asherim out of Judah.

Tena, katika mwaka wa tatu wa kutawala kwake, akawatuma wakuu wake, yaani, Ben-haili, na Obadia, na Zekaria, na Nethaneli, na Mikaya, ili kufundisha mijini mwa Yuda; 2 Mambo ya Nyakati 17:7

Also in the third year of his reign he sent his princes, even Ben Hail, and Obadiah, and Zechariah, and Nethanel, and Micaiah, to teach in the cities of Judah;

na pamoja nao Walawi, yaani, Shemaya, na Nethania, na Zebadia, na Asaheli, na Shemiramothi, na Yehonathani, na Adonia, na Tobia, na Tob-adonia, Walawi; na pamoja nao Elishama na Yehoramu, makuhani. 2 Mambo ya Nyakati 17:8

and with them the Levites, even Shemaiah, and Nethaniah, and Zebadiah, and Asahel, and Shemiramoth, and Jehonathan, and Adonijah, and Tobijah, and Tob-adonijah, the Levites; and with them Elishama and Jehoram, the priests.

Wakafundisha katika Yuda, wenye kitabu cha torati ya Bwana; wakazunguka katika miji yote ya Yuda, wakafundisha kati ya watu. 2 Mambo ya Nyakati 17:9

They taught in Judah, having the book of the law of Yahweh with them; and they went about throughout all the cities of Judah, and taught among the people.

Hofu ya Bwana ikaziangukia falme za nchi zote zilizozunguka Yuda, wasipigane vita na Yehoshafati. 2 Mambo ya Nyakati 17:10

The fear of Yahweh fell on all the kingdoms of the lands that were round about Judah, so that they made no war against Jehoshaphat.

Na baadhi ya Wafilisti walimletea Yehoshafati zawadi, na fedha ya kodi; Waarabu nao wakamletea makundi, kondoo waume saba elfu na mia saba, na mabeberu saba elfu na mia saba. 2 Mambo ya Nyakati 17:11

Some of the Philistines brought Jehoshaphat presents, and silver for tribute; the Arabians also brought him flocks, seven thousand and seven hundred rams, and seven thousand and seven hundred male goats.

Ukuu wake Yehoshafati ukazidi sana; akajenga katika Yuda ngome na miji ya hazina. 2 Mambo ya Nyakati 17:12

Jehoshaphat grew great exceedingly; and he built in Judah castles and cities of store.

Naye alikuwa na kazi nyingi katika miji ya Yuda; na watu wa vita, watu mashujaa humo Yerusalemu. 2 Mambo ya Nyakati 17:13

He had many works in the cities of Judah; and men of war, mighty men of valor, in Jerusalem.

Na hivi ndivyo walivyohesabiwa kwa mbari za baba zao; wa Yuda, maakida wa maelfu; Adna jemadari, na pamoja naye watu mashujaa mia tatu elfu; 2 Mambo ya Nyakati 17:14

This was the numbering of them according to their fathers' houses: Of Judah, the captains of thousands: Adnah the captain, and with him mighty men of valor three hundred thousand;

na wa pili wake Yehohanani akida, na pamoja naye mia mbili na themanini elfu; 2 Mambo ya Nyakati 17:15

and next to him Jehohanan the captain, and with him two hundred eighty thousand;

na baada yake Amasia mwana wa Zikri, aliyejitoa kwa Bwana kwa moyo, na pamoja naye mia mbili elfu, watu mashujaa; 2 Mambo ya Nyakati 17:16

and next to him Amasiah the son of Zichri, who willingly offered himself to Yahweh; and with him two hundred thousand mighty men of valor.

na wa Benyamini; Eliada mtu shujaa, na pamoja naye mia mbili elfu wenye nyuta na ngao; 2 Mambo ya Nyakati 17:17

Of Benjamin: Eliada a mighty man of valor, and with him two hundred thousand armed with bow and shield;

na wa pili wake Yehozabadi, na pamoja naye mia na themanini elfu waliojiweka tayari kwa vita. 2 Mambo ya Nyakati 17:18

and next to him Jehozabad and with him one hundred eighty thousand ready prepared for war.

Hao ndio waliomngojea mfalme, zaidi ya hao mfalme aliowaweka katika miji yenye maboma katika Yuda yote.

2 Mambo ya Nyakati 17:19

These were those who waited on the king, besides those whom the king put in the fortified cities throughout all Judah.